Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

IT siku hzi mbili tatu anapumua pushing za vijana zimepoaa sanaa dah au ndo tamati ya psrs kimenukiaa?
 
Kweli Hajui mbona kuna kazi kibao za Mkataba zimepitia Utumishi example Cereals and other produce Board(CPB),Tanroads Lakini pia ukisoma kanuni za Utumishi pia wanaeza kukaimisha usajili wao wakatuma wakaguzi.
Hizo kazi za mikataba zinazopitia utumishi si kama zile zinazosemwa NSSF. Kazi za mikataba zinazopitia utumishi mara nyingi ni kazi za kada ya juu na zile za muda mfupi kama miezi 3-6. Huko NSSF ni hizo mikataba mifupi mifupi na huwa wana-renew mara kwa mara!!
 
Hizo kazi za mikataba zinazopitia utumishi si kama zile zinazosemwa NSSF. Kazi za mikataba zinazopitia utumishi mara nyingi ni kazi za kada ya juu na zile za muda mfupi kama miezi 3-6. Huko NSSF ni hizo mikataba mifupi mifupi na huwa wana-renew mara kwa mara!!
Zilikua ni mkataba wa Mwaka mmoja, Ila mara nyingi ukifanikiwa kupenya ni renewable mara nyingi.
 
Tuendelee kuwa wavumilivu tu maana Kuna mwamba mmoja hvi Leo kalamba asali ila jamaa alishawah kufanya interview ya utumish mara Moja tu Tena mwaka Jana mwez 6

Imagine Leo kaitwa Tena na taasis ambayo hakuwahi kufanya interview yake...

kasbr Zaid ya mwaka na kitu na alkuwa ashasahau na anapga mishe zake tu..

Leo pdf imeshuka anashangaa kuona watu wanamtext nakumpa hongera..

Kwahyo Kuna ktu Cha kujifunza hapa.

Wakati wa Mungu ni wakat sahh...na kama ipo ipo tuu kama haipo ni haipo.
Duu hongera nyingi kwake
 
Hatimaye Nimelamba Asali ndugu zangu nawashukuru team ya hapa ndani kwa namna tulivyopeana moyo na kufarijiana na mimi niwape moyo kuwa it is just a matter of time. Nimekaa mtaani tangu 2014 mpaka sasa.

Mapambano yaendelee

Hongera sana ndugu,

Hakika Mungu ni mwema sana, daima wakati wa Mungu ndio wakati sahihi kabisa. Nakutakia majukumu mema katika kazi yako, pia zingatia kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji wako.

Mwisho, jipongeze kwa mafanikio hayo uliyopata pamoja na ndugu na jamaa zako na pia kumbuka kutoa shukrani kwa jamii kwani haikuwa rahisi mpaka kufika hapo.
 
Hawa wametoa makucha yao kabisa bila aibu liwalo na liwe!! Nafasi 392 zimehifadhiwa kwa ajili ya wateule!! Ni wateule tu (waliokuwa "wanajitolea" na waliokuwa wamepewa kazi "za mkataba") ndio wanaruhusiwa kuomba hizo kazi. Tangazo ni kwa ajili ya waliomo ndani!! yaani "INTERNAL VACANCY ANNOUNCEMENT". Hawa wameamua kutangulia, wengine (taasisi za asali ya nyuki wadogo) watafuata kama NSSF watafanikiwa. Bila shaka wanapima kina cha maji!! Yasipotokea makelele makubwa ya kulalamika, utakuwa ndio utaratibu wa ajira hapa TZ. Sehemu ya tangazo lao hili hapa:
INTERNAL VACANCY ANNOUNCEMENT
National Social Security Fund (NSSF) as part of our commitment to encourage growth anddevelopment within the Fund, we are excited to announce 392 internal job opportunities available for all Fund’s employees with specific task contracts. Only candidates who are inspecific task contract term within the Fund should apply.

Jambo hili lazima lipingwe kwa nguvu zote!! Kanuni inasema ni lazima fursa itolewe kwa usawa kwa wote wenye sifa stahiki kugombea kila nafasi ya ajira kama wanavyofanya PSRS. Napendekeza ufunguliwe uzi maalumu wa kupinga jambo hili kwa nguvu zote!!
Nitakusaidia kufungua uzi juu ya hili kwa sababu haikubaliki.
 
Back
Top Bottom