Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hiyo status imebadilika pote kwenye app na web ?
 
Pole sana, mdogo wangu alipigwa hizi not selected for oral interview hadi akakata tamaa na ilifikia hadi mtoto wa aunt yangu akawa anamtania binti wa not selected maandishi mekundu upo lakini selected for oral moja tu ilimpa kazi sa hivi yupo tra simiyu huko...na alipiga interview nyingi sana tangu 2019 kaja kupata 2023 hivyo usikate tamaa kiongozi haya mambo yanaumiza sana hata akiwa ndugu yako wa karibu anapitia.....
 
Nashukuru saana mkuu Kwa kunitia moyo
 
I assure you, usikate tamaa endelea kupambana.. utatoboa..cha msingi jifanyie tathmini ni kipi kilikufanya ukashindwa kupenya kwenda oral?
 
Jamani Mwifwa Twinawe na wengine na naomba kuuliza swali mwajiri anapokuambia urudi nyumbani baada ya kureport kazini alafu mwezi na wiki vinakatika bila kuitwa hii inakuwa na tafsiri gani?
Atakuita akimaliza taratibu za ajira yako.

Kuwa na subira, wewe tayari ni mtumishi wa umma. Wengine walipokea hadi mishahara ilihali wakiwa bado wapo nyumbani baada ya kuambiwa watapigiwa simu
 
Mkuu Mwifwa, nataka kujiunga na portal ya PSSSF,, hebu nisanue hapa nafanyaje
Sisi tuliletewa fomu tukajaza, zikakusanywa na kupelekwa.

Sijui ishu ya hiyo portal kabisa.

NOTE: Tujitajidi kujenga uchumi kwa kadri tuwezavyo hata kama tunakatwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, ili baadae tukijaliwa kufika umri wa kustaafu tusianze kuhangaika na Mafao badala yake uchumi tuliojenga ndio tuishi humo humo(yaani hata usipopata mafao isiwe shida kwa sababu kikokotoo ni miyeyusho sana nchi hii na hatujui huko mbeleni mambo yatakuwaje)
 
Asalaam aleikum Wapambanaji 💪,

Nawasalimu tu na kuwatia moyo kuwa kamwe msichoke kupambana na kuitafuta ridhiki huku ukimtanguliza Mungu kwenye kila hatua ili kuyafikia malengo.

Ukiona leo mwenzako kapata nafasi/asali unatakiwa kufanya ni kupiga moyo konde (kuwa na subira) huu ukijinenea kwa kujisema kuwa pdf ijayo bila shaka na Mimi nitakuwepo.

Mungu hawapi watu wote kwa kwa wakati mmoja bali kila mtu kwa wakati wake.

Kila la kheri na tuko pamoja.

Amin.
 
Hakika watu wasikate tamaa kabisa mda ukifika unalamba asali tu
 
Kuna siku taleta kisa changu humu Cha kupambana kutafuta ajira serikalini na kuachana na NG'Os na kampuni zozote,,,,,,,, ushauri tu kijina yoyote jitahidi sana upate kazi serikalini huko kwingine ni kwa hovyo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…