Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Nina imani ushapata ushauri, na mimi pia natoa kulingana na mtazamo wangu.

TRA

Hapa ni unatakiwa kuwa risk taker, ukikosa nafasi, hakuna cha database(yaani unapoteza pambano)

MDA & LGA.

Ni nafuu endapo ukifika hatua ya oral, kuna uwezekano wa kubaki Database(achilia mbali kupata nafasi moja kwa moja) na baadae utaweza kupata nafasi.

Nakuuliza swali: Je, kulingana na maelezo yangu haya, unaona wapi penye nafuu?

NOTE: Ukifanikiwa kutoboa TRA utakuwa umelamba Jackport, ingawa risk ni kubwa.

MDA & LGA, ni vigumu kujua kama utaangukia wapi(MDA) au LGA(Halmashauri) endapo ukitoboa ingawa hakuna risk sana kupita kama ilivyo TRA.

Hadi hapo unaweza kuamua mwenyewe njia ya kufuata
 
Achana na written wala practicals, komaa na Orals. Anza ya TRA waelezee mlangoni changamoto yako ili uwahi kuingia na kutoka. Ukitoka pitiliza mpaka Mbezi chukua gari, timuka. Hata ikiwa ni kwa kusafiri usiku hakikisha unaamkia kwenye Oral, Dodoma.
Hujamuelewa.

Tarehe 8/11/2023 ana Oral(TRA) inafanyikia Dar, pia hii hii tarehe ana Practical(MDA & LGA) inafanyikia Dom.

Ili afanye Oral (MDA & LGA) tarehe 9/11/2023 inabidi afanye na kufaulu Practical yake ambayo ni tarehe 8/11/2023.

Je atawezaje kuzifanya zote Oral(TRA) na Practical(MDA & LGA) kwa siku moja?
 
Kaka .

Mwifwa
Stelingi
@sawadogo


Mungu awatie nguvu huko mliko maana msoto wa kusubiri placement sio poa sijui mliwezaje kuvuka
 

Afanye LGA's maana ina DATABASE na imenyooka.
 
Ushauri wangu kafanye iyo written dodoma then rudi siku iyoiyo dsm jiandae na TRA huwa wanaweka iyo ratiba ya practical after matokeo ya written kutoka na huwa sio tarehe tajwa kama ratiba inavyosema
 
2.5 si ni Pass Mkuu au. Ikitangazwa ajira unayofit we omba. Serikalini kinachoangaliwa ni kwamba umefaulu kuanzia pass. Labda Kama unataka nafasi za Academician ndyo itakuwa kikwazo kwahiyo gpa yako.
Mimi naogopaga kuomba nikajua labda sitaitwa kwenye interview pia kwenye private sector hua naogopa kuapply kazi kumbe inawezekana jamniiii
 
Ushauri wangu kafanye iyo written dodoma then rudi siku iyoiyo dsm jiandae na TRA huwa wanaweka iyo ratiba ya practical after matokeo ya written kutoka na huwa sio tarehe tajwa kama ratiba inavyosema
Unamshauri upumbavu.

Yaani amalize written arudi Dar Kwa ajili ya oral wakati Ana practical kesho yake ushauli wa kimbuzi
 
Mimi ninakushauri haya,

1; kwakua TRA umeshafika nusu ya tukio wewe malizia hiyo oral, kwa sababu unaweza kwenda dodoma na ukafeli/ ukashindwa kutoboa kwenda kwenye practical/oral hivyo ukawa umepoteza Huku na Huku,

2; MDA & LGAs nafasi zinatoka Kila kukicha na unaweza kuomba wakati mwingine ukaitwa ila ukipoteza nafasi (kufika oral TRA) kuja kuipata tena itakua ni ngumu sana.

Ahsante.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Nadhani Huajui TRA mpaka unaongea hivyo TRA sio wakuwaamini.

Unaweza kukuta kwenye hiyo Oral wako Elfu 2 wanataka watu 30
 
We ndio hujamuelewa mdau Donrw jamaa ana Pepa dodoma tarehe 5 ndio Written ya MDA &LGA.
Mimi nimemshauri Apige Written MDA tar 5 ..

Utata uliopo Kwake ni hiyo tarehe 8 Maana kama atafaulu itabidi apige Practical Dodoma na siku hiyo hiyo ana oral Dsm TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…