Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Nina imani ushapata ushauri, na mimi pia natoa kulingana na mtazamo wangu.Nimejichanganya kwa kweli, kwenye ratiba wameandika zote tatu, usaili wa kuandika, vitendo na mahojiano. Nipo njia panda, baada ya TRA kubadili ratiba ya usaili wa mahojiano kuwa tarehe 08/11, na hapo jana nimekuwa shortlisted utumishi mda's & lga's
Saili nilizonazo
Tarehe 05/11 -MDA's & LGA's - Written interview -Dodoma
**Tarehe 08/11 -TRA Oral interview- Dar es salaam
**Tarehe 08/11 - MDA's & LGA's - Practical interview -Dodoma
Tarehe 09/11 - MDA's & LGA's - Oral interview -Dodoma
Ushauri wenu wakuu
TRA
Hapa ni unatakiwa kuwa risk taker, ukikosa nafasi, hakuna cha database(yaani unapoteza pambano)
MDA & LGA.
Ni nafuu endapo ukifika hatua ya oral, kuna uwezekano wa kubaki Database(achilia mbali kupata nafasi moja kwa moja) na baadae utaweza kupata nafasi.
Nakuuliza swali: Je, kulingana na maelezo yangu haya, unaona wapi penye nafuu?
NOTE: Ukifanikiwa kutoboa TRA utakuwa umelamba Jackport, ingawa risk ni kubwa.
MDA & LGA, ni vigumu kujua kama utaangukia wapi(MDA) au LGA(Halmashauri) endapo ukitoboa ingawa hakuna risk sana kupita kama ilivyo TRA.
Hadi hapo unaweza kuamua mwenyewe njia ya kufuata