Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Nina tender ya kusupply tani 45 za raw material xxx kila mwezi kiwanda fulani hivi ni na zina nipa 7M net profit mdogo wangu, tulia mdogo wangu watu wana mawe humu haugusi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mtaalamu wa TENDA YUPO JUKWAA LA AJIRA LA JOBLESS ila hii nchi watu wake wana vituko 🤣🤣
 
Mtaalamu wa TENDA YUPO JUKWAA LA AJIRA LA JOBLESS ila hii nchi watu wake wana vituko [emoji1787][emoji1787]

Dogo wewe ni kajinga sana, wenzako wapo humu kujifunza trick za waliofanikiwa interview mbali mbali na kujifunza kupitia shuhuda za watu, binafsi wapo ambao nawasiliana nao kwa simu wengine walikuwa na uhitaji wa nauli za kwenda kwenye interview,tumeshirikiana na wapo taasisi nyeti sana walitoa shuhuda zao humu na hakuna anayejua basic zao wala taasisi zao ila wewe chinga ndo umetisha.

Tumepata mashavu mazuri ila tumo kushauri na kusaidia panapowezekana, wewe haumuoni Mwifa na wenzake wanavyo heshimika kwenye uzi huu ila wewe sasa utafikiri ulikuwa na ugomvi na watu humu ndani.
 
Mkuu Punguza Ushauri kwenye masuala yanayozungumzia Hela... Mimi nipo likizo ya week mbili, After that week nitakuwa na majukumu ya kujenga taifa langu, kwa watu walioniamini.... So punguza ushauri TENDA YA 7M ,unashinda jukwaa la Jobless 🤣🤣 Nyieee
 

Jukwaa la ajira na tenda hili dogo GPA hiyo ulidesa nini?
Ni kuongezee hii ni Director wa kampuni yangu, unavyoambiwa watu wana CPA wana biashara zao nje ya ajira ndio maana yake dogo, hiyo hela ni kiduchu mno na kama unaijua utility curve na tabia zake jitulize.
 
Guys am so excited, natamani kuwaeleza jambo ila kwa furaha niliyonayo Ntaharibu. Nikitulia ntarudi

Ila tu niseme Nimetoboa pdfla leo.
nilipiga oral interview mwezi wa 10/18
TANAPA.

Hongera sana mkuu Wansakieki 👏👏

Nakutakia maisha mema katika Utumishi wa Umma, napige kazi kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za kazi yako, Pia katende haki.

Furahia ushindi huu pamoja na ndugu na jamaa zako wa karibu kusherekea mafanikio hayo kwan haikuwa rahisi mpaka kufika hapo.

Mwisho, kumbuka kutoa Shukrani kwa kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii kama watoto wenye ulemavu, watoto yatima, wagonjwa n.k

👊👊👊💯
 
NDUGU ZANGU MACHOZI YA FURAHA YAMENITIRIRIKA, HATIMAE MUNGU AMESIKIA DUA ZANGU 🙏🙏, WAKUU NIMETOBOA

Hongera mkuu Utumishi wako fair

Nakutakia mafanikio katika kazi yako uliyopata, katende haki. Pia zingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa umma pale unapotimiza majukumu yako.

Sherehekea mafanikio haya ukiwa na ndugu na jamaa zako wa karibu kuweka kumbukumbu hii nzuri katika maisha yako.

Mwisho, kumbuka kutoa Shukrani kwa kusaidia makundi yenye uhitaji toka katika jamii inayokuzunguka kama watoto yatima, wenye ulemavu, wagonjwa n.k

👊👊👊💯
 

Hongera sana mkuu👏👏 hii ndio maana halisi ya mpambanaji.

Hakika uzi huu umebarikiwa 🙏🙏🙏.
 
Hiyo GPA ya 4.1 sijui aliipata chuo gani wanareward honors grades Kwa wapumbav vilaza kama huyo .
Hicho chuo ni cha wapumbavu bila shaka
 
Ndugu yenu pia hii ni December to Remember Mungu amenitendea.

Nawasihi msikate tamaa pambaneni.

Hongera sana mkuu Muju4 👏👏💯

Nakutakia kila lenye kheri katika majukumu yako mapya, katende haki na kufanya kazi kwa bidii. Katimize majukumu yako kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Kumbuka kutoa Shukrani kwa kusaidia makundi yenye uhitaji kama vile watoto waliozaliwa na changamoto za viungo, watoto yatima, wagonjwa n.k.

Hakika mema mengi yatazidi kutiririka katika maisha yako.

👊👊👊💯
 
............ ........Nipo na IT hapa Makulu anauliza mnataka shuhuda kabla ya mwaka mpya au akaushe kwanza mwaka upinduke?
 
Jobless tunaish kwa matumain sana[emoji3]
Mkuu usijali, Kama ulifanya Oral Mungu atatenda miujiza kikubwa usikate tamaa na usipoteze imani kwake... Kila kitu kinawezekana...

Mimi nakumbuka nilianzaga kufanya interview 2021 ya TRC interview yangu ya kwanza nilipata 58, wakanikanda walichukua kuanzia 60. Ilikuwa ya System Administrator.... Niliumia sana kwa sababu aim ya kwenda kufanya haikuwa kufauru na kupata kazi balu kujifunza , sasa zile marks zili ni impress wangenichagua nikaenda practical nijue najifunza nini tena practical.

But sikukata tamaa, but sisi course zetu watu wa IT hazitoki nafasi mara kwa mara ni mara chache sana so ikikupita unaweza subira hata miezi 6 tena. Inshort watu wa IT kwa mwaka kafanya sanaaa interview ni tatu.... Hata range yetu ya kupata placement sio kubwa.... Unaweza kuta mwaka uliopita watu wa Tehama kuchukuliwa hawazidi 50.

Basi kama sikosei hiyo TRC , ilikuwa mwezi wa kwanza au wapili mwishoni.. nikakaaa miezi mingi takribani miezi sita ila nafasi zilikuwa zinatoka but ubaya yani IT ni kubwa.... Kuna networking, administrator , database, security, web developer ,programmer etc....

Sasa unatakiwa uwe umejitune unapoona unapaweza ukienda tu kila interview unakuwa unapoteza hela zako, cz mfano mimi najijua kabisa hapo Database siwezi kivile kwenda kubahatisha, so inabidi usubilie kile unachoweza ndio tangazo litoke ndio uende, but kuna watu wanajiweza wao zote twende.


Basi bwana ,mimi nikachagua za kufanya so nikawa nachukua material, pamoja na video tutorial huku nikajiunga group la watafutaji la utumishi, so watu wakienda wanashare leo maswali yalikuwa hivi ....basi ukiona hiyo topic naenda nasoma kidogo kidogo na practice hivyo yani....

Basi bwana:...... Kusoma ikawa daily routine yangu, sio kila siku but nikipata muda nasoma yani haiwezi pita week 2, sio kusoma ile serious viileeee ...no sometimes upo kitandani unacheck video tutorial na notes au una solve maswali hivyoooo... Mara unaingia website za maswali na majibu ili mradi kichwa kisipoe kikasahau...., Nilikuwa nasoma any useful material ambayo nilikuwa naona yanaweza nisaidia...

Pia nikawa nimenunua note book, pale mbele nikaweka target kuwa nikienda interview yoyote basi written nisishuke 75% ...practical pia niliweka nakumbuka na oral niliweka tu pass ...

So maisha yakawa yanendelea huku experience nyengine napata humu, kwenye hili jukwaaa.... Mimi hadi kujibu oral nilichukua humu technique kuna mtu aliwahi andika humu .... Hasa lile swali la Education background / tell us about yourself ....

So nikaendelea ,huku nasubiria tangazo la kazi litokeee.... Pia nilikuwa naombaga na private but kule ilikuwa kama tu nikipata nijishikize but my dream was serikalini kwa sababu ya Security pia nilikuwa naimani Carrier yangu itakuwa haraka sana....

Nakumbuka mpka mwaka 2021 unaisha hazikutoka kazi tena za system administrator baada ya zile za TRC ...tukaingia 2022........Itaendeleeaaaa

Nb: Watu wa tehama mnaweza chukua experience mkajaribu kupractice....
 
Endelea mkuu u jobless huu kaz kwelkwel...wakat mwngine unachoka ila ukiangalia nyuma una kund kubwa linakutegemea
Mke
Watoto
Bi mkubwa
Wadogo zako.
Yaan kwa kifupi ni shda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…