Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wakuu msaada ukiwa umesoma bachelor na ukaweka Cheri Cha bachelor ajira portal pale baadae ukasoma diploma ya kitu inawezekana kutoa Chet Cha bachelor kwenye qualifications na ukaweka Cha diploma na ukaweka kuapply kazi Kwa Chet Cha diploma msaada wakuu
 
Hautaweza kubadili, na hauruhusiwi kutoa qualifications uliyoiweka.

Labda uanze kwa kuweka cheti cha Diploma bila kuweka cheti cha Degree halafu ndio uombe kazi ya Diploma.

NB: Ukiweka cheti cha Diploma na Degree, utaweza kuomba nafasi za Degree pekee
 
Kwa mnaoendelea kuingia kundini, pindi unapoambiwa na mwajiri rudi kwanza home na utapigiwa simu/kujulishwa siku rasmi ya kwenda kuanza kazi.

Kama ulikuwa na kijiwe, usiage kijiweni kabla hujaitwa na Mwajiri kwenda kuanza kazi.

Waajiri wengine ni miyeyusho wanatumia muda mrefu kukamilisha taratibu za ajira.

Kutoacha kijiwe kabla hujaitwa itakuepusha na msoto ambao ungeupata pindi endapo ungeacha kijiwe.

Kuna watu waliwahi kufanya hivyo baadae wakaanza kujuta.
 
Mkuu hata nikienda ofisini kwao hawawezi kunisaidiakutoa Chet Cha bachelor nikaweka cha diploma au ndio inakuwai imeshatoka hiyo
 
Hii kweli kaka 🙌 Nimeuza Ghetto langu kabisa, sema Father House alikaza nimlipe kodi nzima miezi mitatu yote ijayo kuanzia jana
 
Naomba kuuliza , hivi huwa ni mpaka upigiwe simu au siku 14 za kusubiria zikiisha unaweza kwenda tu mwenyewe?

Mfano mimi nilivyoreport juzi juzi HR alisema hizo siku 14 ni za kusubiria hela ya kujikimu ukiona imechelewa unaweza kusubiria mpaka mshahara ukaingia,, lakini akasema hawalazimishi mtu kukaa nyumbani kama yeye anajiona anamzuka wa kazi unaweza kuanza tu kama hautaki kusubiria😄😀.

SWALI 1, Je kupata hizo pesa za kujikimu/mshahara ni mpaka akupigie simu au ikiingia unaweza kuona tu ukiwa bado nyumbani ndipo ukaanza safari ya kwenda?

2, Naomba pia kuuliza kuna watu waliowahi kupata pesa za kujikimu ndani ya hizo siku 14 kabisa kwa uaminifu? (Maana nasikia zinachelewaga sana na wengine wamekaa muda mrefu bila kulipwa)
 
Hebu tulia Kisha andika vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…