Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Utawala2025 aliandika mada kulalamika kwann wizara ya afya imeajiri watu wachache kuliko ilivyotangazwa, bila kusahau kuna wengine waliajiriwa wengi zaidi kuliko ilivyotangazwa 😂 ila kwakuwa jamaa ameshapata ajira atakuja hapa kupinga 😂
 
Hawa jamaa wanajua kuchanganya kwa kweli ngoja tukienda kuchukua barua tutajua ukweli.

Maana kada kama Afisa muuguzi msaidizi ANO nafasi zilitangazwa 1000+ wametoa 400.

Mpaka sasa Hatujaona Pdf ya CO ambao kwa kiasi kikubwa hawafanyi kazi wizara ya afya wao ni TAMISEMI.

kinachotia wasiwasi kuna kada zimezidisha kiwango na kuna kada chache hazijafika idadi.

Na kuna kada nyingi hazifanyi kazi wizara mpaka sasa pdf zao hazijatoka.

Watu wa afya wanajiuliza maswali yafuatayo.

Je kutakuwa na mikeka mingine ya LGA(tamisemi) ilhali idadi imekamilika na kupita.

Au mwajiri wizara amepewa jukumu la Ku allocate vituo vya afya kwa sasa tofauti na miaka ya zamani.

Kiukweli haya mambo yana maswali mengi
 
Wenyewe wangetolea ufafanuzi hili jambo, wamewaacha watu dilemma, sio makundi sogozi ya watsapp,sio jf, sio insta watu wanajiuliza, wangejibu ili watu watulie
 
Wenyewe wangetolea ufafanuzi hili jambo, wamewaacha watu dilemma, sio makundi sogozi ya watsapp,sio jf, sio insta watu wanajiuliza, wangejibu ili watu watulie
Nafasi za kada za afya zilikuwa zinatangazwa idadi yake kwa jumla, halafu zinagawiwa kimkoa. Kwa mfano Pharmacists zilikuwa jumla ya nafasi 128. Halafu hizi nafasi ziligawanywa kimkoa kama kilimanjaro 4, Lindi 9, Manyara 1, Mara 8, Mbeya 6 nk hadi mikoa yote. Ukijumlisha hizo nafasi za mikoa unapata 128.

Kila mkoa waweza kuwa na nafasi za MDA & LGA. Hospitali za rufaa za mikoa nafasi zake znaingia MDA, lakini hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati zinaingia kwenye LGA. Kwa maana hiyo kwa mawazo yangu (ambayo yanaweza yasiwe sahihi) hizo nafasi zinazotangazwa kujazwa huko wizara ya afya ni sehemu ya nafasi zilizotangazwa upande wa MDA, na baadaye kama LGA nao walikuwa na nafasi basi zitatangazwa pia baadaye. Kwa hiyo wahusika mnaweza kuendelea kusubiri kwa matumaini!
 
We vuka tuu boda
Maisha ni popote
 
Kwani afya wako chin ya wizara gani? Labda tuanzie hapo... Si wizara ya afya au?
 
Kwani afya wako chin ya wizara gani? Labda tuanzie hapo... Si wizara ya afya au?
Hapana,,

Wanaofanya kazi hospital za kanda,mkoa na vyuo vya Serikali vya kati hawa ndio wanaofahamika kama watumishi waliochini ya Wizara ya afya.

Wanaofanya kazi Hospital za wilaya ,zahanati na Vituo vya afya hawa wanakuwa chini ya Tamisemi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…