Mbaga Jr
JF-Expert Member
- May 28, 2018
- 29,028
- 69,666
Utawala2025 aliandika mada kulalamika kwann wizara ya afya imeajiri watu wachache kuliko ilivyotangazwa, bila kusahau kuna wengine waliajiriwa wengi zaidi kuliko ilivyotangazwa 😂 ila kwakuwa jamaa ameshapata ajira atakuja hapa kupinga 😂Hadi sasa kuna kada za afya ambazo zimeshapangiwa watu wengi zaidi kuliko nafasi zilizotangazwa:
1. Nursing officer II walitangaza nafasi 301 hadi sasa wameajiri 404 wizara ya afya!
2. Pharmacist II walitangaza nafasi 128 hadi sasa wameajiri 164 wizara ya afya
3. Health lab. scientist II walitangaza nafasi 57 hadi sasa wameajiri 214 wizara ya afya
4. Technologist pharmacist II walitangaza nafasi 128 hadi sasa wameajiri 236 wizara ya afya.
Lakini kuna kada ya afya ambayo imeajiri watu wanaolingana na nafasi zilizotangazwa: Medical Officer II walitangaza nafasi 726 hadi sasa wameajiri 726 (pdf mbili 681 na 45) wizara ya afya.
Swali: Ina maana na nafasi za mikoa(kwenye halmashauri) nazo zitatoka au ndio hao hao waliopangwa wizara ya afya?
Japo jambo hili limejadiliwa humu lakini tunaomba wahusika hasa waliomu humu jukwaani watupe ufafanuzi wa uhakika!