Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Jamaa anauliza kama ajapangiwa kituo cha kazi anaweza akaripoti huku akisubiri kazi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
mkuu tupe mrejesho huko TCRA watu mtaingia? au watu waandae mashamba walime. PSRS wamekujaje awamu hii au wamevaa helement kabisa
 
Mamlaka ya ajira iliyotangaza nafasi za ajira kada za afya ni sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali ya mtaa/LGA. Wizara ya afya kama mamlaka ya ajira haikutangaza nafasi za ajira!

Katibu wa Sekretarieti yaAjira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti zaMikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwaWatanzania wenyesifa na uwezo wa kujaza nafasi 9483 kama ilivyoainishwa katikatangazo hili.


NINAVYOFIKIRI: Baada ya usajili, na wizara ya afya ikiwa imeshapata kibali cha kuajiri iliamua kuchukua watu kutoka database! Waliokuwa wamewekwa database baada ya usajili wakajikuta wameokota dodo kwenye mwarobaini!! Wizara ikatoa placement kutoka database na waliokuwa wamefaulu zaidi wakiwa wanasubiria mamlaka zao za ajira zitoe placement na wengine kudhani hawakufaulu!! Kipindi hiki ndo LGA/halmashauri zimepamba moto kutoa placement!! Kwa maneno mengine watu kutoka database wamepangwa MDA/wizara na taasisi zake kama muhimbili, NIMR, nk wakati waliofaulu zaidi wameishia LGA!!
 
Kwanini watu hawataki kuishia LGA?😁
 
Za chini chini(sina uhakika) inasemekana wale walipelekwa Wizara ya Afya ndio walifaulu zaidi
 
Za chini chini(sina uhakika) inasemekana wale walipelekwa Wizara ya Afya ndio walifaulu zaidi
Walitakiwa kupangiwa walipoomba na kumbuka kibali kilikuwa cha tamisemi. Nadhani walioitwa tamisemi ndio walifaulu zaidi make hawa asilimia kubwa wanapangiwa walipoomba kama usahili ulivyowadirect ( sina uhakika)πŸ˜‚
 
Kwanini watu hawataki kuishia LGA?😁
Tatizo la LGA ni usumbufu wa madiwani!! Pia hofu ya wakurugenzi kuhusu usalama wa nafasi zao!! Akitembelea kiongozi kwenye kata husika watumishi wote wa halmashauri lazima wawepo hata kama ni jumapili!! Kwenye mikutano ya hadhara watumishi hulazimika kujibu kero za wananchi papo kwa papo! Ole wako usihudhurie mkutano wa hadhara halafu idara yako ikatakiwa kujibu hoja!! Mishahara ni sawa lakini usumbufu si sawa!!
 
Za chini chini(sina uhakika) inasemekana wale walipelekwa Wizara ya Afya ndio walifaulu zaidi
Kanuni za PSRS hazikubaliani na hoja hiyo!! Mamlaka ya ajira iliyoomba watumishi ndio inapewa kipaumbele!! Kumbuka PSRS wanafanya kwa niaba ya waajiri!! hawawezi kubadilisha!! Waliopangwa wizara ya afya na taasisi zake hao ndo walikuwa na alama za chini!! Kitu kibaya kilichotokea ni kuita watu wa database kabla ya waliokuwa wamechaguliwa!! Ni sawa ni kuita second selection mwazo kabla ya first selection kujiunga na form five au form one!! It was a grave mistake!
 
Baada ya placement za hal mashauri kutoka sasa ni dhahiri kuwa placement za wizara ya afya zilikuwa kutoka database!! Kwenye wizara watu hawakupangwa kutokana na machaguo yao. Lakini placement za halmashauri zimepangwa kulingana na machaguo ya mikoa ya waombaji!! Kwa mfano namfahamu mmoja aliyechagua mkoa wa mbeya na amepangwa mojawapo ya halmashauri za mkoa wa mbeya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…