Mimi siyo mzuri kuelezea maisha yangu mtandaoni, leo nitajitahidi.
Nilimaliza chuo 2016. Nikawa sina ajira, kwakua kozi yangu haitambuliki serikalini, nikajiajiri kwa kufungua game centre. Ilitoa pesa ya kutosha kabla ushindani haujaongezeka.
Hata hivyo kama binadamu wengine sikua nimeridhika na kujiajiri kwakua kujiajiri kunahitaji resources nyingi mno. Achana na wadau wa JF wanaodai ukijiajiri unaweza ukaamua usiende kazini, wakati usipoenda ujue siku hiyo huli (hii ni kwa mitaji ya chini ya 5M) na kujiajiri means faida na hasara zote ni matokeo ya juhudi zako.
So niliendelea kusaka ajira pia. Humu jF kuna watu wanaandika sana unaweza hisi ni msaada kwako lakini niamini mimi hakuna kitu kama hicho, sana sana utatapeliwa tu kama baadhi ya members.
Anyway, nishahudhuria interview TTCL wakanipigia simu kuconfirm taarifa zangu wakasema wataniita hiyo ni hadi leo. Ilikua 2019. Nilifanya training na Jamii media (JamiiForums) ambayo ililenga kua na online reporters ila sikurudi tena kutokana na sababu mbalimbali.
2019 mpaka 20 mwanangu aliumwa nikaua mtaji, nikaacha hata kutafuta ajira, nikawa nimefocus na mtoto.
Muda wote mama yangu ananiambia "Subiri wakati sahihi utafika zitakuja kazi mpaka hutajua uchague ipi" anyway 2022 ikaja nikapata ajira sehemu fulani mshahara laki 5 baada ya miezi miwili naambiwa mshahara inabidi upunguzwe.
Two kids, a wife na wazazi nikajikuta nanyong'onyea hata sikuaga pale, nikawa tu nashinda ndani, April nikaenda Dom kuhudhuria interview za utumishi, nikapita mpaka oral ila bahati mbaya post sikupata. May mwaka huu mshkaji wangu fulani akaniambia kuna ofisi yao mpya bado inataka watu. Nikaenda.
Ofisi ilikua na watu 20 tu mshahara wa kama nilipotoka. Ila tukaambiwa ina mpango wa kukua zaidi. Pale ofisini wakataka foremen, mi najamaa tukaapply, tukapita.
Mshahara ukapanda, na majukumu yakapanda na nikajikuta hata kuingia kwenye mitandao inakua ngumu. Hata hawa wanaodai hawawezi kuishi bila JF ni vile hawana majukumu tu, hata hawa wanaondika mada kila siku ni hawana majukumu au labda ni mabosi haswa ambao hawajali results za ofisi zao.
Ofisi imeajiri watu zaidi ya 200. Yaani naweza sema ni inakua kwa kasi, hivyo na mimi natarajia nikue nayo. Jumanne ya wiki hii nikatafutwa na rafiki yangu fulani akaniambia ofisini kwao kuna nafasi ipo wazi, hii nafasi ina mshahara mkubwa kuzidi hapa ila haina title kama niliyonayo hapa.
Halafu unajua kilichotokea? Kesho yake nafika ofisini nagewa barua ya kua appointed msimamizi wa kitengo kingine. Mshahara ukaongezwa ukafanana na nilipoambiwa kuna nafasi.
Leo mimi nakua na option ya kazi? Nikachoka.
Tangu siku hiyo nafikiria nini niamue? Ikiwa ofisi mpya entry level salary yao ni sawa msimamizi wa kitengo hichi this means nikifanya poa nikaenda juu salary itakua tamu zaidi.
Hapohapo naona kua hii kampuni ni mpya within five months mshahara umelingana na entry level wa kampuni kongwe but it means nikibaki na kukua nayo nitaweza structure vitu vingi.
Hapo ndiyo nikakumbuka usemi wa mama "Itafika siku kazi zitakuja utashindwa jua uchague ipi"
Wito wangu kwa mpambanaji mwenzagu. Usikate tamaa, danganya ikiwezekana, omba Mungu ukitaka nenda kwa waganga. Humu JF hakuna anayejua ulichokula wala mpango wako wa kula. Hakuna anayejua watoto wako ada italipwaje.
So dont stop. Yaani hata iweje, hawa mabrazameni na masista du wa JF wanaoandika kila siku niamini mimi hawana majukumu, ofisini kuna routers lakini hata kuangalia miziki youtube siwezi. Nimenyimwa huo muda.
Na pia nakuambia mpambanaji mwenzangu "Itafika muda kazi zitakua nyingi hutajua uchague ipi"
Pia kuna vitu nimeficha kwa sababu dhahiri.