Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mimi sizungumzii swala la barua ya mwajiri wako, nazungumzingia "vetting" kwamba utumishi wakupangie kituo cha kazi na hawajakufanyia vetting is it possible?!

Imenilazima kurudi huku kusoma tena comment baada ya kuona jamaa anasema kuwa mnabishanana kuhoji dhumuni la kubishana.

Sijaona manishano ila jamaa aliyefafanua kuhusu barua ya Placement(ambayo tunaichukulia Asha Rose Migiro halafu tunaipeleka kwa Mwajiri) na Barua ambayo utapewa na mwajiri(barua ya kazi). Huu ufafanunuzi uko sahihi.

Sasa nirudi kwenye maneno niliyobold hapo kwenye quote.

Ni sahihi mwajiri lazima ajiridhishe kama kaletewa mtu sahihi mwenye vigezo ambavyo anavitaka ndio maana ukipeleka barua kutoka PSRS unaenda kuacha nyaraka zako na kuambiwa watakupigia simu. Kwa kipindi hicho wanakufanyia crosschecking almaarufu kama Veting. Usipokidhi vigezo hawakuiti(unakosa kazi, jamaa kasema hili pia), ukikidhi vigezo vyao watakakuita.

Ukichaguliwa na PSRS sio gurantee ya mwajiri kukubali moja kwa moja.

Sijui kama nimeeleweka
@Chaldzosias Manucho90 Cvez
 
Wangapi waliwahi kukataliwa na waajiri?
 
Nakupongeza sana mkuu, kweli ni kama bahati

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Ewaaaa.... Upo sahihi sie wengine tuna experience ya haya mambo, nashangaa mtu kuja kubisha kitu ambacho hakijui
 
Nahitaji ushahidi ili kujiridhisha juu ya hili, majibu tafadhali? ili jobless niweke cheti kabatini nirudi geita kwenye machimbo ya wachimbaji wadogo wadogo
Kijana, jitahidi kuishi vizuri na uwe na tabia njema, mwadilifu etc

Haya mambo yapo. hapa kwenyewe ushapewa mwanga wa kutosha si sahihi kuongea hizi ishu basi tu kuna muda inabid ugusie juu juu kwa faida ya wengi ila kama huelewi basi yaache/yaachwe kama yalivyo.
 
Waheshimiwa, mimi na rafiki yangu tumekuja utumishi kuchukua barua zetu za kuitwa kazini.

Rafiki yangu amepata,
Na jamaa mwingine pia amepata.
Ila mimi wananiambia barua yangu hawaioni hivyo niache mawasiliano yangu kisha watanipigia ikishakuwa tayari ili nisafiri tena kutoka mkoa ninaoishi kuja Dodoma kuifuata.

Hii imekaaje wakuu, yaani barua za wengine zipo ila yangu haipo wakati sote tumepata kazi taasisi moja??

Ushauri wenu wadau.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Duh apo itabd uwabane vzuri isije ikawa nafas yako imeuzwa kwa mtu mwengine mana kama jina lako lilitoka kwenye pdf ya kuitwa kazin ni lazima barua yako iwepo pale sekretarieti kwaio kuwa makini sana kufatilia ilo jambo
 
Doh! Mbona tena mtihani huu kaka
 
Walifanyaa mchakato wowote kuitafuta?
 
Mhhhh ndio maana nasema haya mambo mpaka ukamilishe na uone mshaara umeingia ndio ufurahi, lakini Kuna mambo mengi yanaweza kutokea kabla ya kulamba asali
 
Walianza kuitafuta Kama kwa dakika 10 hivi,
Kisha nd'o wakanipa hayo majibu.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
Nahisi inaweza wamei-misplace, au wamempa mtu mwengine kimakosa na huyo mtu hakuikagua, au labda ile barua wameiweka kwenye bahasha yenye jina ambalo sio lako. Makosa ya kibinadamu ni kawaida hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…