Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hongera sana na pole pia kwa usumbufu. Namna hiyo ndivyo tunavyopaswa kupigania haki unayoona inaminywa.

Walikueleza nini siku wanakupatia, kiwa barua waliidisplace kimakosa? au ilipotea kabisa wakaiandaa upya?
Hawajanipa maelezo yoyote,
Na kwa nilivyoghadhibika sikutaka hata kuhoji.

Walipoiona ID. yangu tu wakanikumbuka, wakaniambia nitoke nikasubiri mapokezi, baada ya kama robo saa nikaitwa na kupewa barua yangu.
Ila kwa inavyoonekana ni document iliyoprintiwa siku nyingi kiasi.
 
Nimegundua kitu kuhusu hizi placements.

Yaani zinapitia hatua ndefu hadi zije zitoke ndio maana tunaona zinachelewa sana.

Barua zetu zimeandikwa tarehe 8/12/2022(mwezi mmoja baada ya Oral) halafu placement imetoka tarehe 9/1/2023(mwezi mmoja baada ya barua kauandaliwa).

Je hiyo interval ya mwezi mmoja mmoja, nini huwa kinafanyika?

Turejee kanuni zao.

Baada ya Oral matokeo hukusanywa/alama zinakusanywa zinakuwa compile sehemu moja kama oral ilifanyika sehemu tofauti tofauti(yaani PSRS na Zenji). Then Mwenyekiti wa jopo la Panelist atakabidhiwa hayo matokeo na yeye atayawasilisha kwenye Board ili placement zikapangwe kulingana na ufaulu wa oral.(hapo mwezi ushakatika).

Mwezi mwingine inakuja suala la kusainiwa, Hapa mzee Kitenge atatenga muda wa kuzisaini barua zote zilizoandaliwa, hadi kumaliza mwezi ushakatika.

Baada ya hapo ndio zamu ya placements inafika, ikitoka tu barua ziko tayari ndio maana kuchukua barua haichukui muda ni dk chache tu.

Kwa hiyo mnaosubiri placement inabidi mtambue hilo na subira ndio silaha ya kuishi nayo katika hicho chote
Barua huwa ina mambo Gani?
-kama issue ni mlolongo mrefu mbona higher learning institutions huwa wanamaliza mchakato faster na placement kufanyika faster?
 
umeikimbia pepa mkuu, sasa hpo utakuta passmark nikuanzia 90, si kwa ubaya lkn utumishi itabidi waweke marks ambazo mtu akifikisha basi atinge oral , sio kma saiz wanajiamulia tu, hii inavunja mioyo watafutaji wengi
Mkuu utumishi hawajiamulii tu wanafuata kanuni zinazowaongoza .Soma kanuni hizo utajifunza kitu. Nafasi moja inahitaji watu watu wa oral.
Mara nyingi paper rahisi zinasumbua sana unakuta mtu amefaulu lakini kaachwa kwa sababu ya uchache wa nafasi.
Tuliwahi kupiga paper moja hivi jamaa yangu alikuwa na 72 akaachwa walichukua mwisho 74 .
Tangia siku ile nikawa naomba bora nikutane na paper jiwe kuliko nyepesi.
 
umeikimbia pepa mkuu, sasa hpo utakuta passmark nikuanzia 90, si kwa ubaya lkn utumishi itabidi waweke marks ambazo mtu akifikisha basi atinge oral , sio kma saiz wanajiamulia tu, hii inavunja mioyo watafutaji wengi
Wanachokiangalia cha kwanza ni nafasi zilizopo/zinazogombaniwa.

Kwenye oral kila nafasi inabidi igombaniwe na watu 3 au 4 hata 5, pia wanaweza kufika hadi 6.

Sasa mkipata alama zaidi ya 80 watu wengi halafu nafasi zilizopo ni 4, watakaoingia oral ni 12 hadi 24.

Jalia watu 24 ndio wamepata alama zaidi ya 80, kwa hiyo panga lazima likatie huko juu. Wengine mliopata chini ya 80 mnaachwa.

Kanuni zao zimeelezea hii ishu ya selected for oral
 
Hawajanipa maelezo yoyote,
Na kwa nilivyoghadhibika sikutaka hata kuhoji.

Walipoiona ID. yangu tu wakanikumbuka, wakaniambia nitoke nikasubiri mapokezi, baada ya kama robo saa nikaitwa na kupewa barua yangu.
Ila kwa inavyoonekana ni document iliyoprintiwa siku nyingi kiasi.
Basi huenda waliidisplace
 
Barua huwa ina mambo Gani?
-kama issue ni mlolongo mrefu mbona higher learning institutions huwa wanamaliza mchakato faster na placement kufanyika faster?
Kiukweli bado hatujapata jibu sahihi la kwanini wanachelewesha kulingana na taasisi zinazoendesha sahili zao.

Hapa tunajaribu kujenga nadharia tu ila ukweli wa mambo ndio unajulikana kwa wakandaji wenyewe.
 
Hapana,mtihani ulikua simple sana mkuu,nimeshindwa kuelewa intention yao ni nini.ila ngoja tuone majibu watayatoaje

Hahaha. Mkuu mitihani ya aina hiyo majibu yake yanaweza kuja ya ya ovyo na ajabu mpaka uhisi matokeo uliyojaziwa ni ya mtu mwingine.

Ila yote kwa yote, Mungu atasaidia, kama ni wakati umefika, pepa nyepesi hivyo hivyo ndiyo ya kukupa kazi.
 
Back
Top Bottom