Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kama huna connection tuliza ball!...


Niliwahi kwenda sehemu moja(ni ofisi maarufu nchini)

Jamaa wana asili ya kiarabu ila wanaishi nchini na kujifanya na wao ni wabongo na kututukuza kinafki tuone ni wamoja wetu kumbe ni trick za kuendelea kufaidi mema ya nchi. Jamaa kapigiwa simu na ndugu/jamaa yake wa kike ila Mwarab mwenzie maongezi yalikuwa hivi...

BOSS: Naam hello... Saaleko!

NDUGU/JAMAA/CHAWA: waaleykoum salaam................ (maongezi mengine yakapita, kisha)

Si unajua mwanao kamaliza mwaka huu na sitaki akae mtaani apoteze tu muda azurule bila msingi hapa Kariakoo kwahiyo naomba aje aanze hapo....


BOSS: Hamna shida..., basi Insha'Allah mwambie Jumatatu aje..


MIMI nikabaki nalaumu wazazi, familia, ukoo, mababu,mpaka uafrika wangu.
 
Atakuwa kashajua maana hii kitu haifichiki.

Ila huku sio hotcake ni mwendo wa overload na maripoti hatari, muda wa kutoka kazini ni saa 9:30 ila watu wanapitiliza hadi saa 11 jioni wakiwa busy na maripoti.
Ila wakipitiliza si wanalipwa overtime?
 
2 Wafalme 2:21 BHN

Elisha akaenda kwenye chemchemi ya maji, akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa; tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba.”

Mkuu inafanya kazi.
Sawa mkuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ndio ukweli huo yaani, ukienda kwa ajili ya Oral kuna presha hatari hayo mazingira ila ukienda kuchukua barua unajiona na mtu mzito hivi[emoji3][emoji3]
Mkaguzi napitia hapa CPA(T) ili niweze kufika ulipo nikukague.
 
Suala la connection lipo, na huenda likaendelea kuwepo,

Lakini mpambanaji hutakiwi kukata tamaa, Kuna wakati connection haiwezi kutumika bali uwezo flani wa mtu.

Nakumbuka interview yetu pale IAE kulikuwa na wahitimu wengi wa pale chuoni. Wengi tulikata tamaa na kuamini watawachukua wahitimu wao ambao wanajuana na baadhi ya watu kwenye panel. Baada ya written ni watu wawili hivi ndio waliingia kwenye oral na mmoja ndio akafanikiwa kupata placement (Kwa wale wahitimu wao).

Mimi baada ya kupata placement, watu wengi waliniuliza unajuana na nani serikalini au utumishi? lakini hakuna hata naejuana nae, ni Mungu na jitihada tu. Marafiki zangu baadhi nao wamepata ajira kupitia Utumishi na naamini ni jitihada zao tu. Huu utaratibu wa utumishi ni mzuri sana na kama una mapungufu basi ni machache sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…