Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ict soma operating system na network nakutumia hapa notes za OS na network mfano pepar niliyofanya mie Ilikua na network na operating system Kawa yote mkuu ukisoma Hizo unatoboa nasikia hata interview ya Tra ilijaaga vitu hivyo
 

Attachments

Ict soma operating system na network nakutumia hapa notes za OS na network mfano pepar niliyofanya mie Ilikua na network na operating system Kawa yote mkuu ukisoma Hizo unatoboa nasikia hata interview ya Tra ilijaaga vitu hivyo
Ndugu hii placement ulochaguliwa…mlifanya interview mwezi gani?
 
#Wadau nami ipo siku jina langu litaappear kwa mkekawa Placement PSRS na nitakuja kuwaambia hapa tena nikiwa nimepata kazi kwenye Taasisi nzuri tu..
MUNGU NDIO KILA KITU IPO SIKU HAUSLTLING ZETU ATAZIONA NA KUZIBARIKI.
Tuseme INSHALLAH......[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Amen Mkuu, hili ni la kweli kabisa Mkuu. Usichoke na mapambano.
 
Inshallah kikubwa uzima tu

Mkuu, hongera sana. Naamini hata baada ya kupata kazi ukimsikia mtu anawasimanga wasio na ajira utaendelea kumchukia na hauta muunga mkono.

Hahaha, maana usijeangukia kwenye kundi la kuwasema vijana kwamba hawataki kujiajiri.
 
Vijana mnaotafuta kazi msichoke kupambana kutafuta kazi,na pia acheni kulalamika mnapoona mchakato wa kuitwa kwenye Interview au kuitwa kazini umechelewa,nimeona majina ya kuitwa kazini BUNGE ambapo mchakato wa Usaili ulifanyika mwezi uliopita tu,ni vizuri kutumia muda vizuri kujiandaa kwa Usaili KULIKO kutumia muda JF kufungua Nyuzi za kulalamika mchakato wa Usaili au kuitwa kazini kuchelewa,PSRS ni Taasisi inayofanya kazi kwa taratibu na si kwa pressure za JF,vijana mliopata nafasi Bunge na Taasisi nyingine HONGERENI na mkafanye kazi
Watu hawana uhakika wa kula wanawezaje kutumia muda vizuri kujiandaa na usaili? Mkiwa nacho acheni kuwaona wenzenu kama hawana juhudi zozote.
 
Hongereni wote mliotoboa na ambao bado tuendelee kukomaa…nilitaka kuuliza izo placements zilizotoka ni adi ifm?

Mkuu, kama ulifanya IFM kuwa na amani, mipango iliyopo ni muwe kazini kabla mwaka mpya wa masomo haujaanza. Kwa hiyo haitochukua muda mrefu mambo yatakuwa hadharani.
 
Habarini za muda waungwana,,,Napenda kutoa pongezi zangu kutoka moyoni kwa waliofanikiwa hakika sauti zetu zimefika mahala husika mungu watangulie sisi tunaendelea kupambana

Mwenye uzoefu naomba Kuliza:
Mfano Taasisi imetangaza nafasi tano (5) za kazi Kupitia Utumishi
Application ikapata watu (4) Ajira portal
Na tarehe ya usaili ikapangwa kwa hao wa nne (4)

Utumishi ikabidi ifanye Re -advertsed nafasi moja Ikapata watu (5) sababu walipunguza vigezo

Sasa wale wanne kwe Tangazo Mama hadi oral wameingia 2 wengine hawakufika hadi placement inatoka ni hao wawili tu ila kureport kwa muajiri ameriport mmoja na process za muajiri zimekamilika ni huyo mmoja tu (1)

Hawa wa Re-advertiseing ambao ni wa tano (5) ambao post yao ilikuwa moja wote wakaenda hadi oral na placement imetoka ni huyo mmoja anaetakiwa kureport kwa muajiri

Jee hii imekaaje inamana nafasi 3 zinakufa au kutakuwa na uchukuaji wa kanzi data kati ya hao wa nne(4) waliobaki

Au serikali kibali kitarudi wamekosa watu stahiki

Kwa alie na ulewa please,,,,
 
Hongera sana mkuu. Kila la kheri ukawe mtumishi mwema na bora, kazingatie maadili na miiko ya utumishi. Zile nyodo na majivuno siyatarajii kwa mpambanaji wa namna yako, hayo mambo waachie wanaovutwa kwa mserereko bila kujua msoto wa kupambana.

Usisahau kuja kutujulia hali humu tunaoendelea kupambana, kila mmoja ana siku yake ya kutoboa, hatuwezi kutoboa wote kwa siku moja. Tangulia tutakuja siku yetu ikifika!
Asante sana Mkuu, maneno kuntu sana nitayazingatia, lazima niingie huku kuwatia moyo kadri niwezavyo na nitatoa ushirikiano wa hali na mali pale inapobidi

Nayeyuka huku nikiweweseka kiutumishi tumishi
 
Back
Top Bottom