Sijasoma UDSM hivyo sina ufahamu huko inakuaje ila vyuo vingi TAs wanafundisha undergraduates. Plus UDSM ndio chuo kikubwa hapa Tanzania wana academic staff's wa kutosha hiyo inaweza isijitokeze.
Ila kwa vyuo vingi hapa Bongo wanafundisha at the same time wanajiendeleza.
Ndio hapo juu nimekueleza kwamba, inawezekana wanafanya hivyo kutokana na upungufu wa watumishi.
Fahamu kwamba TCU ndio wanaweka standards za mwenye qualifications zipi, afanye nini.
Sio suala la chuo tu kujiamulia kwamba mwenye degree moja amfundishe mwenye mwenye masters, au mwenye digrii moja amfundishe anayesoma digrii ya kwanza.
TCU wanapofanya assessment ya vyuo, na kufanya rankings, wanaangalia pia compliance kwenye watumishi, vigezo na majukumu.
Hakuna muongozo wowote, be it kwa vyuo vikuu, au kwa vyuo vya kati, unaoruhusu mtu mwenye digrii moja kufundisha wanafunzi wa digrii ya kwanza. Iwe ni TCU au NACTVET (zamani NACTE).
Wanafanya hivyo pengine kulingana na uhaba wa watumishi, lakini as per taratibu, hairushusiwi.
Ukitaka nitume documents ku sapoti maandiko kutoka TCU, Miongozo ya vyuo, NACTVET, mamlaka za ajira (PSRS), I can do that all day.