Habari za leo Wakuu.
Jana niliahidi kuleta mrejesho.
Nilifanya written Interview nane ,saba zote sikufika hata oral zote nilikuwa napata namba za viatu , yanane nikafika oral na ndo hii niliyopata placement.
Nilingia kwenye chumba cha wakandaji nikiwa nimevaa kadeti, shati na koti langu vizuri kabisa. Nilipoingia tu ndani nikawasalimia wakandaji wakaitikia then mmoja akasema karibu kiti.
Nilitumia muda mfupi sana nimetoka wadau wanashangaa mbona mapema sana nadhani walijua nimefukuzwa mle ndani😂😂
Baada ya hapo nilijiona mjinga sana maana nimeshindwa kujibu swali moja. Hamu ya kula ilikata kabisa niliona kama nimepoteza nafasi lakin Mungu ndo alijua.
Nimejifunza ili ufanikiwe lazima upite mambo magumu( Rejea wimbo wa Christina Shusho-Dhahabu)
1. Usikate tamaa jipe moyo ipo siku utatoboa bahati huwapata wale wanaojaribu.
2. Ukiitwa kwenye usaili fanya maandalizi haswa. Piga msuli yatima haswa pitia job descriptions zifuatilie moja baada ya nyingine. Saili nyingi za nyuma nilikuwa sijindai vizuri pia nilikuwa sifuatili trends za maswali. Unakuta unasoma research kumbe wameshaacha kutoa research.
3. Omba Mungu yeye ndo anajua ni lini atakupa.
4. Usibanduke kwenye huu Uzi. Jamii forums ni kila kitu imagine nimeanza kufuatilia huu uzi mwezi wa 10 nikapata hints kibao nikafufua matumani , mwezi wa 10 huo huo nikatoboa oral kwa mara ya kwanza. Hata uwe kipanga au kenge namna gani bila kujua trends na namna ya kujibu maswali kutoboa ningumu.
Natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote wa uzi huu (Mwifa, Wizy a.k.a Wkingz mzee wa status😂😂 na wengine wote) kwa michango yenu .
N.B: Mtoto wa masikini kabisa ametoboa bila connection acha kulalamika inawezekana.
Nilivyofurahi mimi wife amefurahi mara 10 yake🤣🤣🤣