Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Watu walioingia huko kwa jinsi yake ni wachache sana dhidi ya wengi walioingizwa huko kwa connection. Na nyie wachache hutumiwa kuwafumba watu macho!! Lakini hata hivyo, hoja ya msingi ni kutaka kuwatenga waombaji wengine walio nje ya NSSF kwa sasa!! Hao ma-intern wasiepushiwe ushindani kwa kuwatenga na kuwazuia waqombaji wengine!!
Kila mtu ana mawazo yake juu ya jambo fulani. Mawazo yako tunayaheshimu.
 
Halafu naona hii ndio itakuwa trend kuanzia sasa ,hii ya taasisi kuajiri wenyewe , na jinsi walivyo wanafiki . Institutions nyingi zenye mishahara minono na marupurupu ndio walikuwa wanajivuta kutangaza kazi muda wote huo ,wakati ambao Halmashauri na Tamisemi wanatangaza kazi kila siku ,kama sio makusudi ni nini hiyo ?
Wameamua kutuachia halmashauri tupambane nazo, vinono wale wao na familia zao
 
Mimi kupata INTERN nilipitiaTAESA . Nilifanya Interview nikapangiwa INTERN pale TRA, nikakomaa kwa miaka miwili. Mkataba ulipoisha tukaondolewa wakapatiwa vijana wengine nafasi ya INTERN. Ilikuwa mwaka 2020 hadi 2022. Ni utaratibu mzuri sana ambao unawapa vijana kuongeza CV yao.
Hili suala lina walengwa specifically,, hawa wa TAESA wa 1 year contract niwambie tu wasijipe matumaini san kma wanadhani hili lina wahusu.. wakati wew contarct yako iliisha na ikawa terminated kuna wenzako hao hao uliokuwa nao wameendelea ku renew contact year after year bila mgongo wa TAESA tena + walioingia bila ata mgongo wa TAESA. Hawa ndo wanatafutwa. Naongea kitu nilicho kishuhudia (case sturdy ni tra musoma)
Usilo lijua ni sawa na usiku wa giza

Toka TRA wameanza kuchukua interns kupitia TAESA, wanufaika wako wangap mpaka sasa?
Nafasi ziko ngapi?
Ndugu elewa tu hili suala la wanao jitolea wapewe kipaumbele lina walengwa specifically. Kuna watu wanatafutwa apo
 
watu waoga sana hata kwenye haki zao wanaogopa piaa.

kazi zao kusifia tu kwenye acount za utumishi fb twiter na......
tutoe mawazo wataalamu yasipotufaa sisi yatawafaa wanaokuja.
Noma sana mkuu ,aisee hii issue inabidi tuipambanie sana , huu uhuni utokomezwe , hata tusipofaidika sisi ,watafaidika wadogo zetu au watoto wetu.
Inatengenezwa future mbaya sana kwa madogo
 
Majitu yamejikausha kwenye hizo taasisi as if hayahitaji nguvu kazi mpya ,kumbe yanapiga timing kupenyeza ndugu na vimada wao .
Hawa NSSF wahuni sana tangu nianze kufuatia ajira psrs, sijawahi kuona wanatangaza kazi yeyote wala ata kuchukua database, nikawa najiuliza inamaana hawa jamaa wamejitosheleza kwa upande wa watumishi, kumbu magumashi tu.
 
Back
Top Bottom