Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

wakuu lazima tutoe mrejesho hapa
hatimaye nimeangukia halmashauri leo

Nawashukuru ndugu zangu
nawashukuru psrs
daaah hongera sana mkuu,hakika Mungu ni mwema,ukawe mtumishi mwema maana wewe ni mingoni mwa watu tulioanza na huu uzi tangu mwanzo mpaka leo nakumbuka jinsi ulivyo na moyo wa uvumilivu,sijalamba asali ila nina furaha sana juu yako.
 
wakuu lazima tutoe mrejesho hapa
hatimaye nimeangukia halmashauri leo

Nawashukuru ndugu zangu
nawashukuru psrs
Nyakati ngumu huwa hazidumu hata kama zitachukua muda mrefu ku exist, Subira na Uvumilivu ndio silaha pekee ya kupambana na nyakati hizo.

Juzi kati nilikuwa napitia comments za uzi huu za mwaka jana hususani miezi ya October hadi December ili kujikumbusha miongozo ya mikando ya written tuliyowahi kupeana maana kuna mtu nilikuwa nataka nimpe muongozo.

Nikawa nakutana na comments zako, huku moyoni najisemea "huyu mwamba kaanza kufight kitambo, siku yake ipo mbioni" nikawa nalinganisha na wengi wetu tuliokuwa active humu tangu mwaka jana na asilimia kubwa washaingia kundini.

Hongera sana, I'm happy for you Mkuu, Kila la kheri kwenye majukumu yako mapya. Ukawe mwema huko upande wa pili ili uweze kutimiza ndoto zako zaidi.
 
Dah! Mkuu mfwende sawadogo hongera sana. Nikiona watu tuliokuwepo muda mrefu kwenye huu uzi bila ya kupata shuhuda nao wanaleta shuhuda za kupata ajira namimi napata nguvu zaidi kwamba kuna siku dogo ninayemuhangaikia apate nafasi naye atapata.

Hongera tena, japo naamini inawezekana moyo wako uko kwenye vyombo vya ulinzi na usalama lakini huu sio mwisho wa mapambano, ndio njia zinazidi kufunguka kwa kasi.
Hakika jobless wamepoteza mtu muhimu. Nani atashikilia kijiti cha mfwende?
Duh Naona nmebaki pekeangu mkongwe humu kila MTU keshalamba asali
 
Database inafanya kazi wote tutafikiwa, jamaa yangu huyu kachomoka leo kupitia Database
IMG_3134.jpg


Selected for oral is real [emoji123]
 
Ndugu zangu Nashukuru kwa comments zenu, sijaweza ku reply kulingana kwamba ni nyingi sana ila nimehakikisha nai like kila comments,hakika ninyi ni familia yangu

nafahamu nimetoa somo la uvumilivu kwa watafutaji wengi, maana nimesubiri miezi nane coz placement zilitoka (february)

Namimi leo naamini selected for oral kwenye App yao ina maana kubwa katika kupata kazi kwa hiyo
tusikate tamaa.

nikweli nimepitia mengi, nilipenda majeshi hasa uhamiaji nilipokosa kule nikatilia mkazo huku.database imenitoa mtaani coz nikajua nimesahaulika.

nawatakia kheri ambao hamjapata ikiwezekana mpate taasis nzuri na kwa wakati.

mwisho ahsante psrs,mmenitoa jalalani (in proff kabudi voice)
 
Back
Top Bottom