Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

NAOMBA NIWATIE MOYO JOBLESS WOTE HUMU:-

Usiwaze na wala usikate Tamaa, Suala la ridhki hatupangi sisi.... Ila anayepanga ni Mungu...

So usikate Tamaa na wala usivunjike Moyo,Ridhki yako ipo na Itafika hata kama sio Utumishi ila sehemu nyingine.

Mifano ipo Mingi tuuu.... Unaweza ukapambania kitu kwa nguvu, mwisho ukakosa ila ukajikuta umepata kitu ambacho hata hukukusudia /kutarajia kukipata....So kikubwa DUA...kuna Pdf la watu 1000 kabla Mwaka haujaisha huu.
Subira ni rahisi kuisema ila kuitekeleza ni ngumu, lakini ni muhimu sana kuwa na subira.
Nakumbuka tuliitwa interview written kwenye taasisi moja pale udom (CIVE) tarehe 06/09/2022 nikapita, tukaitwa oral 08/09/2022 tukafanya lakini watu wakaitwa kazini mwezi wa 12/2022 jina langu halikuwepo. Nikapotezea nikawa nafanya mambo yangu mengine ya papatu papatu ili nipate kulipa kodi ya chumba nilichopanga mjini dsm. Mnamo tarehe 29/03/2023 utumishi wakatoa mkeka na mimi nimo tena taasisi taasisi moja kubwa ya serikali iliyoshika namba 2 kama mwajiri bora tanzania.
Sikuwa najua, siku sina hili wa lile jamaa tuliyekutana dodoma yeye ni mkazi wa mbeya ananipigia simu nikiwa kimara mwisho nataka nipande daraja niende ghetto ananipigia simu ananipa hii taarifa na kulalamika kuwa amenitafuta tokea asubuhi sipatikani, ni kweli nikiwa na heka heka simu huwa naweka kindege, lakini jioni huwa natoa nikiwa narudi nyumbani nikaftur kwangu.
Akaniambia oya jumatatu twende dodoma tukachukue barua tumeitwa kazini, sikuamini nikajua mzaha, akasema nakutumia pdf ingia Whatsapp, kweli naona jina langu na lake limo, siwafichi almanusura nigongwe ma gari maana nilikuwa natizama pdf karibu kabisa na lami sasa ile kupagawa nikajikuta naenda kwenywe lami kati kati ila msamalia alinivuta shati kwa nguvu kuikwepa bajaji.
Jumatatu tulienda mara moja na tukachukua barua zetu na j4 kuziwasilisha kwa mwajiri wetu. Ndipo tukaanza msoto mpya unaoitwa vetting mpaka tarehe 29/05/2023 tukapewa barua za kuripoti vituo vyetu vya kazi.
Jamani sekretarieti ya ajira ni mkombozi, sina babu, baba wala shangazi aliyeko huko na mimi ndio wa kwanza kupata kazi serikalini, kikubwa ukifika hatua ya oral basi ipo siku yako tu isiyo na jina jitahidi kutembelea psrs. Laiti kama tassisi zingekuwa zinaajiri zenyewe nakwambia kweli, ni wenye konekisheni tu ndio wangepata kazi ila hawa utumishi wanahakikisha keki hii ndogo tunaila wote hata wewe ambaye kwenu hakuna historia ya mtu hata mmoja aliyewahi kuketi meza kuu na wafalme. Asanteni sana
 
Screenshot unioneshe walipoonesha kama hauna vyeti vya kukutambulisha ufanye nini! Oukey I trust you written sitoboi kwasababu MUNGU anatokea kwenu. Yes level yangu ya uelewa ni ndogo kwa maana hata wewe mwenye level kubwa ya uelewa ulianza kuipata kwa kidogo kidogo...okey una level kubwa ya uelewa ebu nieleweshe sio kunisimanga na kunitupia LAANA zisizoweza kunigusa...kuusu bachelor degree is identification by pc of paper knowledge,skills and wisdom is in the brain ya mtu bila kujali level ya elimu..... kama nilivotoa testimony ya kufaulu baadhi ya interview zangu mwanzo basi ntakuja na testimony ya interview hii ntakapofeli ntakwambia ili uone dream yako ilivo come true

“Don’t Panic when you reply someone give him/her your exposure so that you will adapting yourself on some one else”

NAITAJI BARAKA ZAKO KUFAULU INTERVIEW HII mr it personel LOVE YOU MORE BRO[emoji3059][emoji1434][emoji1488]
Mjalaba mrefu mno kuusoma, kwenye interview usije ukajibu kirefu hivi utakoseshwa maksi, be brief as you can. [emoji3]
 
Subira ni rahisi kuisema ila kuitekeleza ni ngumu, lakini ni muhimu sana kuwa na subira.
Nakumbuka tuliitwa interview written kwenye taasisi moja pale udom (CIVE) tarehe 06/09/2022 nikapita, tukaitwa oral 08/09/2022 tukafanya lakini watu wakaitwa kazini mwezi wa 12/2022 jina langu halikuwepo. Nikapotezea nikawa nafanya mambo yangu mengine ya papatu papatu ili nipate kulipa kodi ya chumba nilichopanga mjini dsm. Mnamo tarehe 29/03/2023 utumishi wakatoa mkeka na mimi nimo tena taasisi taasisi moja kubwa ya serikali iliyoshika namba 2 kama mwajiri bora tanzania.
Sikuwa najua, siku sina hili wa lile jamaa tuliyekutana dodoma yeye ni mkazi wa mbeya ananipigia simu nikiwa kimara mwisho nataka nipande daraja niende ghetto ananipigia simu ananipa hii taarifa na kulalamika kuwa amenitafuta tokea asubuhi sipatikani, ni kweli nikiwa na heka heka simu huwa naweka kindege, lakini jioni huwa natoa nikiwa narudi nyumbani nikaftur kwangu.
Akaniambia oya jumatatu twende dodoma tukachukue barua tumeitwa kazini, sikuamini nikajua mzaha, akasema nakutumia pdf ingia Whatsapp, kweli naona jina langu na lake limo, siwafichi almanusura nigongwe ma gari maana nilikuwa natizama pdf karibu kabisa na lami sasa ile kupagawa nikajikuta naenda kwenywe lami kati kati ila msamalia alinivuta shati kwa nguvu kuikwepa bajaji.
Jumatatu tulienda mara moja na tukachukua barua zetu na j4 kuziwasilisha kwa mwajiri wetu. Ndipo tukaanza msoto mpya unaoitwa vetting mpaka tarehe 29/05/2023 tukapewa barua za kuripoti vituo vyetu vya kazi.
Jamani sekretarieti ya ajira ni mkombozi, sina babu, baba wala shangazi aliyeko huko na mimi ndio wa kwanza kupata kazi serikalini, kikubwa ukifika hatua ya oral basi ipo siku yako tu isiyo na jina jitahidi kutembelea psrs. Laiti kama tassisi zingekuwa zinaajiri zenyewe nakwambia kweli, ni wenye konekisheni tu ndio wangepata kazi ila hawa utumishi wanahakikisha keki hii ndogo tunaila wote hata wewe ambaye kwenu hakuna historia ya mtu hata mmoja aliyewahi kuketi meza kuu na wafalme. Asanteni sana

Hii story imenigusa nakuja inbox kukupa zawadi [emoji320][emoji23][emoji23]
 
Mjalaba mrefu mno kuusoma, kwenye interview usije ukajibu kirefu hivi utakoseshwa maksi, be brief as you can. [emoji3]

[emoji38][emoji38][emoji38] MUNGU MWENYEWE AMESHUSHA QURAN na BIBLE akiwa aja BRIEFLY na tunazinunua everyday...ajira so kila kitu MUNGU ndo mwongoza njia...JOBLESS tunafeli sana kuamini katika mifumo na si KANUNI.
 
Leo Kuna Pdf la placement before Saa 10 jioni... Na kesho pia kuna pdf la placement .... Watu watakuwa Si haba, hawatapungua 30 kwa kila Pfd so stay tunned ##Zandani kabisa
Binafsi nlishaanza kukuamin tangu pdf ile ya mwisho kaka,na leo tena imetoka kama ulivopost hapa asubuhi...big up kaka kwa info nzuri zinazotupa moyo na matumain sis jobless
 
Back
Top Bottom