Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Moyo unaumia kila nikifungia Uzi nakutana na majina ya mengi kwa kada yangu.

Najiuliza je mimi sistahili kuwepo hapo.

Mapambano yangu ni ya muda mrefu mpaka umefika sehemu watu wengine imekuwa kejeri kwao kwa kuniita mzee wa interview.

Dear Lord nakutegemea nakuamini.
Kusikitika na kuumia roho ni kama unataka kujihesabia haki ..nakushauri mimina tu moyo wako kwa Mwenyezi Mungu
 
Moyo unaumia kila nikifungia Uzi nakutana na majina ya mengi kwa kada yangu.

Najiuliza je mimi sistahili kuwepo hapo.

Mapambano yangu ni ya muda mrefu mpaka umefika sehemu watu wengine imekuwa kejeri kwao kwa kuniita mzee wa interview.

Dear Lord nakutegemea nakuamini.
Na mm napitia hayo hayo ndugu kwani umesomea kada gani
 
Ukisha ona unaingia k wenye mfumo haufunguki ujue kuna ka pdf ukiona inafunguka chapu 😆😆 hamna kitu wangetupa hata moja ya weekend
 
Yaani kila siku huwa najiuliza au kwasababu huwa napost humu JF kuhusu kupata ajira hizi za utumishi ndio maana kila pdf likitoka sioni jina langu.

Lakini bado sijakata tamaa naamini MUNGU atatenda miujiza na mm jina langu litatokea kwy pdf ya placement Ameen.

Utumishi pia kama kuna namna tunawakosea humu tunaombe mtusamehe sisi ni watoto wawakulima ni mihemko tu, tunaomba sana wakuu(PSRS) mtuonee huruma, inauma sana unapoona mliofanya nao interview wanapata ajira alafu ww kila pdf haoni jina lako.
Inaumiza sana mkuu. Ila wakati wa Mungu ni wakati sahihi. Amini utalamba asali siku sio nyingi
 
Back
Top Bottom