Wakuu naombeni ushauri, mimi nina kazi private sector (start up). Ni kazi ambayo haina mkataba wala pension (ni miaka miwili sasa), tuliongea tu kwa mdomo. Nalipwa kama 600k hivi, sasa naona startup yenyewe haitusui, na nina mke na mtoto mmoja. Nahisi kama napoteza muda. Nina diploma ya computer science, na kazi karibia 99% za IT PSRS zinahitaji degree.
Nime apply sehemu tatu LGA (mshahara 580,000 position (60)),
NIT (mshahara 860 hivi position moja), chuo cha bahari (mshahara 1,300,000 hivi kama sijakosea | position moja).
Sasa maswali yangu ni:-
- Nibaki startup, hoping for the best bila pension na umri unaenda kwa hope ya kutusua huko mbele?
- Niombe mkopo nisome degree. (Kama nitapata)
- Nisifanye interview ya LGA kwasababu mshahara ni uleule wa mateso?.
- Nifanye LGA at least nitakua na pension, bima ya afya na nitajiendeleza huko mbele?.
- Nifanye tu interview za taasisi (NIT, DMI)?.
- Nisitegemee sana position hizo moja moja?.