Kwanini uwanja wa ndege wa Julius Nyerere haukujengwa maeneo ya watu wa kipato cha juu kama ilivyojengwa Mlimani City Mall?

Kwanza unatakiwa utambue uwanja wa ndege unahitaji eneo kubwa la kutosha kwa ajili ya barabara ya kurukia na kupaki ndege.
Iisitoshe uwanja ulijengwa na wazungu enzi hizo Tanganyika haijapata uhuru hivo baada ya Uhuru Mwl Nyerere alikuja ongeza terminal 2 kwa kuwa tayari barabara ya kurukia ndege ilikuwepo na eneo lilikuwepo.

Pia tambua kuwa wakati uwanja huo unajengwa hakukuwa na makazi ya watu kama unavyoona.sasa ambapo watu ndiyo wamevamia eneo la karibu na uwanja.
 
For your information enzi hizo za ukoloni kipindi uwanja huo unajengwa, uzunguni ya Dar ilikuwa Kurasini, Kibasila na maeneo jirani.

Mbezi Beach, Masaki, sijui Mlimani City zilikuja baadaye sana. Airport haiwezi kuhama kufuata uzunguni mpya. Do your homework.
 
Duuh, uzunguni Kibasila??..
 
Duuh, uzunguni Kibasila??..
Kibasila pameharibiwa na waswahili nowadays hapakuwa pa kawaida enzi hizo pakiwa makazi mjerumani.

Au Kinondoni unapaonaje? Hii Kinondoni ukitoka mataa ya Morocco kuelekea Magomeni kushoto kwako. Huoni mitaa ilivyopangika? Ni kipindi mbunge wa eneo hilo akiwa mzungu. Leo hii hapafai sababu ya uswahili.
 
Ilala ndio kuna Uchumi mkubwa na wakati huo uwanja unajengwa huko unakokuita kwa matajiri ilikua ni mapori tu. Uwanja upo kabla ya uhuru.
 
High Income hawahitaji kelele za Mandege
 
Bora umejitetea nilishakuwa nimekuandalia mawe,pia labda nikupe mawazo yangu,ingefanyika hivyo huenda uwanja usingejengwa kabisa kwakuwa gharama ya ujenzi ingekuwa kubwa mno kumbuka wala kwa urefu wa kamba nawaongeza sifuri kumfidia akaridhika nakukubali nishughuli pevu kuliko kumfidia mzalendo halisi na mvuja jasho wa taifa letu.
 
Matajiri wa Dar wanaishi wapi??..
MO anakaa Ilala??..
Matajiri wengi waarabu/Wahindi wanaishi Upanga/Mjini

Familia ya Dewji asili yao ni Singida ila wana Nyumba kubwa tu Upanga, Oil Com, Gsm na wengineo wana makazi maeneo hayo.

Na kama mwengine alivyokujibu huko ndio wanaishi wafanyabiashara na watu wenye income Kubwa, ambao by average wanachangia pato kubwa kuliko eneo lolote lile Nchi hii,
 
Kwanza ni nchi gani ambapo Airport inajengwa wanapoishi matajiri? Airport hujengwa nje ya mji kiusalama,sehemu isiyo na makazi ya watu kwa kuwa ajali nyingi za ndege hutokea wakati wa kutua au wakati wa kupaa.Kuepuka madhara Airport nyingi duniani zipo mbali na makazi ya watu au nje ya mji
 
Ilala hakuna makazi ya watu pale Karakata na Kitunda??

Bunju na Boko Kinondoni sio nje ya Mji??..
 
Ilala hakuna makazi ya watu pale Karakata na Kitunda??

Bunju na Boko Kinondoni sio nje ya Mji??..
Watu ndio waliufuata uwanja, uwanja ulijengwa porini kabla ya uhuru , kule ilikuwa nje ya mji mbali na makazi ya watu.
 
Mapato ya Dar yanategemea Ilala.Ilala ndiyo kitovu cha uchumi wa Dar na ndiyo iliko serikali (Ikulu).pia ndiko ziliko bandari na Sgr.kinondoni ni starehe zaidi
 
Mapato ya Dar yanategemea Ilala.Ilala ndiyo kitovu cha uchumi wa Dar na ndiyo iliko serikali (Ikulu).pia ndiko ziliko bandari na Sgr.kinondoni ni starehe zaidi
Tunazungumzia pato la mtu mmoja mmoja wakazi wanaoishi eneo husika na sio mayumba ya biashara..
 
Hizi akili bado sana...
 
Wakati unajengwa Mlimani city lilikuwa pori lenye ngedere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…