Kwanini uzinzi ni dhambi? Arggghh!

Kwanini uzinzi ni dhambi? Arggghh!

kama huyo dada atakuwa hajaolewa atakuwa anafanya uasherati hali kadhalika mwanaume ila kama ameolewa/kuoa watakuwa wanafanya uzinzi sasa kwanini uzini huku unamke utakuwa hujamtendea haki mkeo.
 
Dhambi ni nini? Kuzini ni nini? kula tunda nini? Tamaaa ni nini? Njaa ni ipi na nini? Ni lini nawezapata "chakula"???? mmmmh haya narudi baadae ngoja nimfungulie mlango ndio kafika hapa sasa sijui hii thread imeanzishwa kwa makusudi ili inikatishe tamaa? sijui lengo lake mwaya; je nimwambie arudi? au nimwache akae hapa hapa tuangaliane tu? haya
 
Naona shetani yupo kazini kuwapotosha wanadamu,zinduka ee mwana jf,wengine ni freemasons humu.Tusali sana kumpiga vita huyu pepo mchafu
 
Buji kila kitu kizuri ni dhambi. Kuvaa vizuri, kula vizuri, gari kali, na mitungi eti vyote hivyo wanaviita anasa. Sielewi tatizo lilianzia wapi, kwenye siasa za ujamaa au kwenye dini
 
Kumbe ni dhambi?
Ukitaka kuishi vizuri jiwekee sheria wewe mwenyewe. Tatizo tunawaachia wengine wafikirie kwa ajili yetu then tunaanza kujishtukia.
 
Katika Mithali 6:32 Biblia inasema “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”

1 Corinthians 6: 9 Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi Utawala wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,

10 wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang`anyi, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu.

11 Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywa watakatifu, na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.
 
Kwa nini uzinzi ni dhambi? Watu tumekubaliana kwa ridhaa yetu kula raha, sijamchukua mke wa mtu. Huyu niliyemchukua mimi hana mume, bwana wala boyfriend. Kwanini kwa kulala naye niambiwe mimetenda dhambi? Mambo mengine yanaudhi kweli!!!!
Tamaa ndo inakusumbua!hakuna uhuru usio na mipaka, Mungu aliyeweka utaratibu huo ni mjanja na mwenye hekima kuliko wewe, je ulipokuwa mtoto kwenu hakukuwa na utaratibu wa kufuata? wazazi wako walipokwambia ni marufuku kurudi nyumbani usiku uliwaonaje? sasa je huoni faida ya kuwa nyumbani mapema baada ya kuwa mkubwa?we bado ni dogo kwa ufahamu mbele za muumba, acha ujinga, fuata maelekezo ya Muumba ili uishi.IPO NJIA IONEKANAYO KUWA NZURI MACHONI PA MTU LAKINI MWISHO WAKE NI MAANGAMIZI!
 
ulizaliwaje......? ulimkuta baba na mama yako wanaishi kihuni tu.? ama uliwakuta ktk ndoa. (waulize) upate jibu zuri.
 
Kwa nini uzinzi ni dhambi? Watu tumekubaliana kwa ridhaa yetu kula raha, sijamchukua mke wa mtu. Huyu niliyemchukua mimi hana mume, bwana wala boyfriend. Kwanini kwa kulala naye niambiwe mimetenda dhambi? Mambo mengine yanaudhi kweli!!!!

ili watu wahalalishe ndoa!vipi kama dadako watu wanajipigia au bi mkubwa wako angekuwa anapewa mikasi bila ndoa halafu mtu mzima ukazaliwa wakati wakali wanaendeleza libeneke!bila usingependa basi ndo maana uzinzi ni dhambi kwani unapeleka masononeko katika nyoyo za wanaopigiwa ndugu zao
 
Dah! hii sredi imenisibitishia kwamba tutakaouona ufalme wa mbinguni ni wachache sana.
Ama kweli nyinyi ni kizazi cha chatu. khaaa!

Nimemaliza kuhubiri.
 
Kwa nini uzinzi ni dhambi? Watu tumekubaliana kwa ridhaa yetu kula raha, sijamchukua mke wa mtu. Huyu niliyemchukua mimi hana mume, bwana wala boyfriend. Kwanini kwa kulala naye niambiwe mimetenda dhambi? Mambo mengine yanaudhi kweli!!!!

Ushapata jibu kama Yesu aliingia Kanisani au.
 
Kwa nini uzinzi ni dhambi? Watu tumekubaliana kwa ridhaa yetu kula raha, sijamchukua mke wa mtu. Huyu niliyemchukua mimi hana mume, bwana wala boyfriend. Kwanini kwa kulala naye niambiwe mimetenda dhambi? Mambo mengine yanaudhi kweli!!!!
zingatia:
1. uzinzi mmoja kwa mmoja unaashiria dhambi, kwa sababu kitendo hicho Mungu alikiweka duniani kwa ajili ya wanandoa tu.........
2. oa wa kwako ili huo uzinzi ubatilishwe na kuitwa tendo la ndoa ambalo ni takatifu kabisa

kumbuka pia tukiachana na maswala ya dini hata zamani wazee wetu waliyachukulia haya mambo ya kufanya nje ya noa kama vitendo vya aibu,
kwa wale wenye tamaa waliruhusiwa kuoa wanawake zaidi ya mmoja ili usionekane mzinzi ingawa kiuhalisia hali hiyo ilikuwa uzinzi wa dhati kabisa
 
Bila sheria mimi nisingejua dhambi ni nini. Hivya kwa vile vitabu vya Mungu vinasem tendo la ndoa bila kuoa ni dhambi kufanya hivyo ni kuvunja amri za mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom