Bueno
JF-Expert Member
- Sep 9, 2022
- 4,114
- 6,449
Wenye akili ambao hawazitumii akili zao km watu wengine walivyotarajiwa.
Wanaitwa Washamba.
Wanadharauliwa.
Wanaonekana hawafai kwenye jamii wanayoishi.
Hawasikilizwi hata kwenye kikao cha familia. Wakitaka kuchangia popote kwenye kikao wanaambiwa subiri amalize yule pale kichwa panzi mmoja wewe mwenye akili utatusumbua subiri ikiwezekana usichangie kabisa.
Vichwa Panzi wengi wasiojua vitu vingi sana ila wana ujanja ujanja mwiiingi kimuonekano wa mavazi na kujiweka ndio wanaitwa wajanja mno, hii nimeona hata nilipokua nasoma. Ila kichwani ni bila bila hawana kitu wanabebwa na exposure.
Mfano;
Kuna Mzee mmoja alifanya kazi kwenye kampuni fulani ya Malori iliyomilikiwa na Mr. X akafanya kazi km injinia asie na Cheti maana hakusoma Chuo ila alijifunza mtaani kwenye gereji bubu hizi, hakusoma hata VETA.
Basi kuna kipindi Gari km 15 zote zikawa na shida haziwaki zimezima hazitembei, ikabidi kampuni ilete mafundi wa ndani wakajiribu bila bila hakuna alieweza kuziamsha, kampuni ikaagiza fundi toka Ulaya akaja nae akahangaika nazo ila Chuma zikawa zimemdindia hazitaki.
Kampuni ikawa imenyoosha mikono juu kwamba km fundi msomi km huyu kutoka Ulaya ameshindwa kabisa kufufua haya magari basi hizi Gari hazifai tena na yule injinia toka nje akasema kweeli Gari hizi hazifai tena ni Screpa sasa, yule fundi asie na Cheti aliposikia vile akawapinga wakampuuza kwamba utatuambia nini wewe huyu mwenzio ni msomi wa magari mwenye PhD ya ufundi wa Magari kutoka Ulaya ameshindwa kuyaamsha haya Magari wewe utaweza?
Akaiomba kampuni impe magari yote 15 ayatengeneze na wampe siku 7 yaan wiki 1 magari yote yatakua yameamka km yametoka kiwandani, wakamshangaa sana basi wakakubari kwa shingo upande maana walifikiri hakuna atakachoweza kukifanya kwenye yale Magari yakaweza kufufuka. Akawaambia vifaa anavyohitaji wakampatia vyote. Akaanza kazi ndani ya siku 7 akawa amemaliza kutengeneza Gari zote 15 zinawaka na zinapiga kazi bila Chenga.
Kampuni ikashangaa sana kwamba huyu mboni vyeti hana na ameweza kutengeneza Gari zililokufa akazifufua na hakutokea Ulaya na hana hata PhD ya ufundi wa Magari hajaenda VETA wala wapi ila ni wa hapa hapa Bongo, pasina shaka huyu mtu atakua ni Mchawi. Kampuni ikaamua kumfukuza kazi badala ya kumpa kazi.
Kwanini watu wengi wenye akili na wanaoonekana wana akili huishia kupuuzwa mawazo yao, kudharauliwa, kutengwa, kutosikilizwa, kutokuzingatiwa, kutoheshimiwa, nk mara nyingi kuliko watu wasio na akili yaan Vichwa Panzi?
Kalamu imeisha wino....
Nakaribisha hoja zenu wakuu.