Kwanini vijana tusijitolee kulingana na Ujuzi tulio nao?

Kwanini vijana tusijitolee kulingana na Ujuzi tulio nao?

Joined
Nov 2, 2020
Posts
68
Reaction score
90
Kwa nini wasomi wengi hawapo tayari kujitolea?

Jamii ina imani kubwa na vijana wetu ambao wanafika ngazi za juu za kitaaluma, kiasi wakaaminika kupewa nafasi katika maeneo mbalimbali.

Lakini ni ngumu kwao waliopewa dhamana hiyo, kuwa tayari kuwakusanya hata baadhi tu ya wale wanaowazunguka ,Ili kuwasaidia japo kwa uchache tu wa maarifa yatakayokuwa na manufaa.

Ni swali ambalo kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza. Kipi kinachangia vijana kutojitolea, na badala yake wamekuwa wakilia juu ya ajira ambazo kiuhalisia ni chache kuliko idadi ya wahitimu wenyewe mtaani?

Mfano hata kuamua kuielimisha jamii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kama Facebook, TWITTER , Youtube na mfano wake.
 
Kuleimisha kupitia mitandao ya kijamii

Hivi unajua kweli msoto?

Hela ya kula tu shida

Bando hela unatoa wapi

Stress zimekujaa unakaa kwa shemeji hata geto huna harafu ukajitolee bure?

Aiseee
 
Ndugu yangu uhalisia hauko hivyo.Binafsi nimewahi kuomba kujitolea maeneo mbalimbali katika serikali na binafsi si rahisi kama unavyofikiria.Wengi hawataki kabisa kutokana na kulinda siri za taasisi ,kuficha udhaifu wa watendaji kwa hofu kuwa unawezaukawachomoa kwenye nafasi zao,lakini pia hawapendi kuwajibika katika kukusimamia.
Mkuu kama ulichonacho kina manufaa ya moja kwa moja na jamii,Kwa gharama yeyote ikiwemo ya muda wako,Utakuwa tayari kushare na wanaokuzunguka.

Hivyo usikate tamaa ,maana jambo zuri lina ugumu ndani yake,Ili siku likitimia upate cha kuhadithia.
 
Kuleimisha kupitia mitandao ya kijamii

Hivi unajua kweli msoto?

Hela ya kula tu shida

Bando hela unatoa wapi

Stress zimekujaa unakaa kwa shemeji hata geto huna harafu ukajitolee bure?

Aiseee
Ni kweli kabisa stress ni kikwazo cha mambo mengi,Hususan kwa mtu ambae hana wa kumpa mbadala au mchongo wa ziada.Kwa mfano mtu una access ya kuingia jamii forum na kushiriki katika majukwaa mbalimbali humu.

Baadhi yetu wamejizolea umaarufu kupitia jamii forum,Kitu ambacho ni silaha moja kubwa katika kumsaidia mtu kufikia malengo yake ya kutoka kimaisha.
 
Inaonekana inakaa kwa dada, ila ungekaa kwako,neno kijitolea isingetamani kisikia
Nashkuru mkuu kwa maoni yako,Itoshe kusema hata kama unakaa kwa nani,Kama hujataka kujitolea sidhani kama mtaelewana.

Maana kiukweli huezi kaa kwa dada pasi na kufanya kazi yeyote ambayo itaonesha unalenga kumfanyia wepesi.

Yani akulishe ,na wakati mwingine viela kidogo anakutoa,Halafu uje usema kuwa huwezi kufanya japo usafi wa uwanja tu kwa kuwa uko kwa dada!!!!!
 
Kwa nini wasomi wengi hawapo tayari kujitolea?

Jamii ina imani kubwa na vijana wetu ambao wanafika ngazi za juu za kitaaluma, kiasi wakaaminika kupewa nafasi katika maeneo mbalimbali.

Lakini ni ngumu kwao waliopewa dhamana hiyo, kuwa tayari kuwakusanya hata baadhi tu ya wale wanaowazunguka ,Ili kuwasaidia japo kwa uchache tu wa maarifa yatakayokuwa na manufaa.

Ni swali ambalo kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza. Kipi kinachangia vijana kutojitolea, na badala yake wamekuwa wakilia juu ya ajira ambazo kiuhalisia ni chache kuliko idadi ya wahitimu wenyewe mtaani?

Mfano hata kuamua kuielimisha jamii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kama Facebook, TWITTER , Youtube na mfano wake.
Mfumo wetu wa Elimu
Unamuandaa mtu kutafauta ajira zaidi na si kujitolea......

Mfumo huu dume,umewekwa kwa malengo....na waliouweka mfumo huu,wamefanikiwa

Utaalamu hakuna
Watu wana Makaratasi wakiyaita shahada

Huruma hakuna
Watu wametiwa uroho na uchu wa mali/madaraka

Kama utakuwa na kumbukumbu
Wakati upo chuo...ni wanafunzi wangapi uliowahi kuwasikia wakiulizana kuhusu mishahara kulingana na kile wanachokisomea.......!!!!

Dunia ya sasa haina huruma Bro
Mwenye huruma,anaonekanwa ni mpumbavu na wa ajabu ajabu
 
Siku hizi hata kujitolea kama huna connection utaambulia patupu, maeneo mengi wanapeana wenyewe au ndugu, sio rahisi kama unavyodhani maana wanajua wakikukubalia kujitolea unapata experience ambayo itakupa exposure ya kupata kazi huko mbeleni sasa nani anataka akufanikishe kirahisi badala ya kumfanikisha nduguye au rafikiye?! Nyoosha mkono upewe chance ya kujitolea au uwe na Mjomba au referees!

Siku hizi voluntary Sio rahisi kama unavyodhani. Utazunguka taasisi, makampuni na NGO's kibao bila mafanikio,
 
Back
Top Bottom