AMRANI NURUDINI SAMWAJA
Member
- May 21, 2019
- 14
- 24
KWANINI VIJANA WA TANZANIA WENYE NDOTO ZA KUPATA FURSA ZA AJIRA,ELIMU,KUJITOLEA KATIKA NCHIZA ZA UMOJA WA MATAIFA( NCHI ZA NJE) HUISHIA KUTAPELIWA,KUPATA VYUO VYA UCHOCHORONI AU KUKOSA NAFASI KABISA?
Tanzania ina vijana wasomi Tena wengi sana kutokana na wimbi la kukosekana ajira wanajikuta wanaranda mitaani kusaka fursa mbalimbali,ila pia tukumbuke katika nchi yetu Tanzania ina balozi nyingi sana karibia kila nchi hizi balozi zingekuwa zinasaidia vijana wake kusaka fursa za uhakika ikiwemo elimu,ajira na zinginezo itapunguza wimbi la vijana wasio na ajira nawenye ndoto za kusoma nje ya nchi.Pia Mashirika ya umoja wa mataifa mfano: FAO,WHO, na mengineyo hutoa fursa kwa vijana za kujitolea ila za kulipwa pia hufikishwa katika balozi zetu.
NI NINI SABABU YA MATATIZO YA VIJANA WETU KUKOSA AJIRA,KUTAPELIWA ?
1. UBINAFSI WA WATU WENYE MAMLAKA NA KUPELEKA NDUGU ZAO ( KUBANIA NAFASI).
2. KUKOSA UZALENDO KWA NCHI NA VIJANA WAKE.
3. RUSHWA.
NI NJIA GANI ZA KUTATUA HAYA YOTE?

- Chukulia nchi jirani( Kenya) Wana dawati la Wizara ya Mambo ya Nje ambalo linaratibu na kushughulikia fursa za elimu, ajira na nyinginezo kwa vijana wa taifa lao katika nchi za Umoja wa Mataifa , taasisi za kitaifa na katika balozi mbalimbali kumbuka sio tu kuwatafutia fursa pia kuwawezesha panapohitajika.
- Kwa hiyo miaka ya mbele kidogo nchi ya Kenya itakuwa imepenyesha maelfu na maelfu ya vijana wake wengi katika nafasi mbalimbali kwenye nchi za Umoja wa Mataifa na taasisi za kitaifa.Sisi Tanzania tutabaki kunaniana nafasi mpaka lini?
- Baadhi ya nchi wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuwekeza kwa vijana wao kwakuwapatia na kuwatafutia nafasi katika nchi za Umoja wa Mataifa na taasisi za kitaifa na balozi zake ili vijana warudi kuwekeza nchini kwao,tukumbuke wenye nyadhifa na wanaobania nafasi na waliokosa uzalendo huzeeka ( kuzeeka) na wataliacha taifa katika Giza badala wangewekeza kwa vijana ili waje wakomboe taifa lao baada ya kupata uzoefu wa kutosha kwa namna nchi nyingine zinavyofanya maendeleo mbalimbali.
NI NJIA GANI ZA KUTATUA HAYA YOTE?
- Balozi zetu zinafanya kazi nyingi sana ila wangeanzisha Dawati la wizara ya mambo ya nje ambalo litashughulikia na kuhabarisha vijana na wanachi wenye ujuzi mbalimbali kwa fursa za kiuchumi,elimu na ajira zinazopatikana katika balozi husika.Kuanzishwa kwa dawati Hilo liwe linaratubu na kufuatilia na kuchimbua fursa zilizopo katika nchi za Umoja wa Mataifa na wapa vijana na wanachi wenye ujuzi mbalimbali.
- Baada ya kuanzishwa dawati maalumu la kuhabarisha fursa mbalimbali za kiuchumi, elimu na ajira njia zifuatazo napendekeza zingetumika kama kuanzishwa Gazeti maalumu la kuchimbua na kuhabarisha fursa za kiuchumi, elimu na ajira kwa wanachi, Redio au TV( TBC) kuwa na kipindi maalumu Cha kuhabarisha vijana na wanachi kuhusu fursa zilizopo huko duniani( nchi za nje).Au njia zote zitumike ili kufikasha ujumbe kwa urahisi zaidi ili vijana wetu wajikite katika nafasi mbalimbali za kiuchumi, elimu na ajira walete uzoefu waje waendeshe nchi yetu.
- Wizara yetu ya Mambo ya Nje na Wizara ya Elimu ( TAMISEMI) walipaswa kuasisi idara maalumu " one top center" ambazo zingekuwa zinatoa ushauri,elimu na miongozo sahihi wa kufanya kwa vijana wenye ndoto za kwenda kusoma nchi za nje. Hivi Vituo (One top center) zinakuwa na ofisi zao katika ngazi za mikoa, halmashauri na kata ili kuwafikia wananchi kiurahisi.
Upvote
2