Pre GE2025 Kwanini vijana wengi hawapendi kushiriki chaguzi hasa kupiga kura?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

trojan92

Member
Joined
May 18, 2024
Posts
91
Reaction score
276
Heloo wana JF

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania na vioja vyake kwa muda mrefu. Ni kweli pasi na shaka kuwa vijana wengi hujitokeza kwenye kampeni lakini kwenye kupiga kura wengi hawaendi kabisa.

Hii inathiri upatikanaji wa matokeo tarajiwa sababu wanatarajia mshindi ambae hawajampigia kura.

Inawezekana vipi mtu ashinde bila kupigiwa kura?

Je kupiga kura ni jukumu la watu wa rika la kati na wazed tu?

Vijana kwanini hawapendi kupiga kura?

Ushauri wangu kwa vijana
Ikiwa tunataka viongozi fulani washinde basi tujitokeze siku za kupiga kura ili washinde wale tunaowataka kuliko kutokupiga kura na kutarajia mgombea fulani ashinde, atashindaje bila kura yako?
 
Heloo wana JF

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania na vioja vyake kwa muda mrefu. Ni kweli pasi na shaka kuwa vijana wengi hujitokeza kwenye kampeni lakini kwenye kupiga kura wengi hawaendi kabisa...
Hili liko wazi mkuu nahisi hata wewe tayar jibu unalo
 
honestly siwez kupoteza muda wangu nikaenda kupiga kura yani naenda kupiga kura iweje?? ni haki yangu but hapana
 
Heloo wana JF

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania na vioja vyake kwa muda mrefu. Ni kweli pasi na shaka kuwa vijana wengi hujitokeza kwenye kampeni lakini kwenye kupiga kura wengi hawaendi kabisa.

Hii inathiri upatikanaji wa matokeo tarajiwa sababu wanatarajia mshindi ambae hawajampigia kura.

Inawezekana vipi mtu ashinde bila kupigiwa kura?

Je kupiga kura ni jukumu la watu wa rika la kati na wazed tu?

Vijana kwanini hawapendi kupiga kura?

Ushauri wangu kwa vijana
Ikiwa tunataka viongozi fulani washinde basi tujitokeze siku za kupiga kura ili washinde wale tunaowataka kuliko kutokupiga kura na kutarajia mgombea fulani ashinde, atashindaje bila kura yako?
Wamekuwa wakipenda kupiga kura, lakini kura zao zikawa zinachezewa. Hakuna mtu anayejitambua ataendelea kushiriki kupiga kura ambayo haiheshimiwi.
 
Hata mimi nawaunga mkono hao vijana, its wastage of time and energy. Nimepiga kura once kwenye maisha yangu, naomba Mungu nisije kupiga kura tena.

When/if tukija kuwa na uchaguzi huru na wa haki basi nitapiga, sio hizi sarakasi.
 
Heloo wana JF

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania na vioja vyake kwa muda mrefu. Ni kweli pasi na shaka kuwa vijana wengi hujitokeza kwenye kampeni lakini kwenye kupiga kura wengi hawaendi kabisa.

Hii inathiri upatikanaji wa matokeo tarajiwa sababu wanatarajia mshindi ambae hawajampigia kura.

Inawezekana vipi mtu ashinde bila kupigiwa kura?

Je kupiga kura ni jukumu la watu wa rika la kati na wazed tu?

Vijana kwanini hawapendi kupiga kura?

Ushauri wangu kwa vijana
Ikiwa tunataka viongozi fulani washinde basi tujitokeze siku za kupiga kura ili washinde wale tunaowataka kuliko kutokupiga kura na kutarajia mgombea fulani ashinde, atashindaje bila kura yako?
Samia kashawaambia wakipiga au wasipopiga, CCM itatangazwa mshindi tu.

Wanaona haina maana yoyote kupiga kura.
 
Moja ya impact kubwa mno katika umri wa ujana ni tabia ya kutaka vitu vya harakaharaka. Ujana hauna kitu inaitwa subira. Ujana unataka matokeo ya papo kwa hapo. Ujana ni maswali mengi yasiyokuwa na majawabu . Ujana una tamaa kupita kiasi.
 
Kupiga kura tz haina maana yoyote

Ova
Samia kashawaambia wakipiga au wasipopiga, CCM itatangazwa mshindi tu.

Wanaona haina maana yoyote kupiga kura.
Mfumo mzima wa uchaguzi ni ukakasi tupu.
Nendeni mkapige kura asubuhi mapema mtu yeyote atakayefanya dhuruma hiyo ya kuiba kura hatoduma kwenye madaraka hayo
 
Tunatakiwa kufundisha watu wetu, vijana na watoto kufanya lile wanalolitaka kwa haki, kulisimamia kwa gharama yoyote wanavyoweza na mwisho watapata.

Habari ya kukatisha tamaa ni upuuzi usio na faida kwa jamii na taifa.

Kuna faida gani ya kuwa taifa la magoigoi yaliyokata tamaa? Watatawaliwa na mataifa mengine.

Lazima kujenga taifa la majasiri wanaopenda haki na maslahi mapana ya wengi.
 
Hata mkipiga kura kwingine CCM ndio inaenda kuunda serikali
 
Usitupangie maisha......
Na ukiendelea kutusema naweza anzisha fujo hapa ukajuta...
 
Ndo zao hasa wa kipande kile, hawapigi kabisa alafu ccm wakishinda wanasema wameibiwa kura
 
Labda kwenye foleni waweke mirinda nyeusi bariiiidiii
 
Wamekuwa wakipenda kupiga kura, lakini kura zao zikawa zinachezewa. Hakuna mtu anayejitambua ataendelea kushiriki kupiga kura ambayo haiheshimiwi.
Kijana ampigwe na jua kwenye foleni (kumbuka wazee hawakai kwenye foleni), achafuliwe na ule wino ili hali MSHINDI ANAJULIKANA hata wa 2030.
 
Kuna vijana wanasema hawata piga kura tena baada ya kuona uchafuzi uliopita
 
Back
Top Bottom