Kwanini Vijana wengi wanafanikiwa wakija Dar es Salaam kuliko mikoani?

Nakumbuka niko miaka 19-20, ndo fursa zime itika mkoani.
hahaha, mkoani for life.
 
Mikoani mishe nyingi Ni za musimu Ila Dar muda wote Ni pesa Na shuhuli za kila aina
 
Kutoboa mapena kweli dar ni rahisi ila kama unataks kufika mbali nenda tu mkoani
 
Mikoani mishe nyingi Ni za musimu Ila Dar muda wote Ni pesa Na shuhuli za kila aina
True na huu ndiyo ukweli,,Mfano mdogo Nipo mkoani na nina kigari cha abiria . Nimefanya tathmini nimekuja kugundua katika miezi 12 hii gari inafanya kazi miezi isiyozidi 6. Huku nilipo Kuanzia mwezi wa 11-3 ni miezi ambayo hakuna abiria kabisaa na mara nyingi gari inapaki home tu. Hii kitu inanivuruga akili sana.
 
Ukiwa Dar, unatandika kimkeka chako pale kimara mwisho kituoni unaweka zako ndizi mbivu maembe mawili matatu, asubuhi mpaka jioni mzigo umeisha, Kajaribu kufanya hivyo hapo Kilangeni Njombe ulete mrejesho 😀
 
Watakuita chizi Kufanya hivyo mkoa. By the way biashara kama hizo hata Dar ni za kichoko tu hufiki popote. Dar pesa ipo Tandika. mbagala na kariakoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…