Kwanini vijana wengine kutoka Mazingira magumu huibuka na kufanikiwa?

Kwanini vijana wengine kutoka Mazingira magumu huibuka na kufanikiwa?

Ingawa ni kweli akili, ujasiri, na kujituma ni muhimu, je, huoni kuwa wakati mwingine bahati pia inaweza kuwa kichocheo cha kufanikisha mipango?

Kuna wale ambao, licha ya juhudi na mipango yao, wanahitaji fursa fulani au mabadiliko ya hali ambayo yanaweza kuonekana kama bahati.

Pia, si kwamba tunapuuza umuhimu wa akili na juhudi, bali tunakubali kuwa wakati mwingine kuna mambo yasiyotegemewa yanayoweza kusaidia kufanikisha malengo.
bahati impate mwenye hivyo nilivyoorodhesha hapo ndo atafaulu lkn bahati naipa asilimia 10 tu!.
 
Kuna vijana wanaotoka kwenye mazingira magumu lakini wanashinda changamoto na kufanikiwa maishani.

Unadhani ni nini kinachowasaidia kufanikisha haya licha ya changamoto kubwa wanazopitia? Na sisi sote tunaweza kujifunza nini kutoka kwao?
Uwezekano wa masikini kufanikiwa ni mdogo sana ukilinganisha na watoto wa kishua..
 
Michael Jordan?
China?
Ukraine?
Facebook?
Donald Trump?
Halima Mdee?
Tiktok?
Fei Toto?
 
📌Wagumu hawana FAKE STANDARDS,pia hawana habari ya KURUDISHA MPIRA KWA KIPA,unakomaa na maisha mwanzo mwisho kwasababu unajua ukimess up kule kijijini kwenu MSOTO wake ni bora ufe👋so hawa wasongombikaji(WAGUMU) huwa wanapambania KOMBE kufa na kupona,nyuma mwiko mbele kwa mbele kitafahamika tu!!!

Wamjini/wakishua wao wanatest maji kwa ugoko akiona namna gani hapa huyo anarudi kwa WAZAZI anazeekea hapo kama yule babu wa TIKTOK.

Hi spirit ya kujua ukizingua kuna pa kuegemea inafanya hawa wakishua wanakuwa less AGGRESSIVE na mapambano ya kimafanikio.Zaidi zaidi wakishua wanategemea wizi na dili hawana muda wa kuumiza kichwa!!!
Wewe unafikiri bila wizi utatoboa
 
Mkuu, sasa mtoto wa kishua afanikiwe ili aende wapi tena?

Yaani mantiki yako ni sawa na kuuliza iwapo mtoto wa Elon Musk ameshawahi kupanda ndege.
Kati ya mtoto wa Elon Musk na mtoto wa uswazi ni nani yupo kwenye position kubwa ya kupata mtaji wa biashara kuanzia 5,000,000??
 
Uwezekano wa kufanikiwa hauangalii mtu ni maskini au tajiri. Uwezekano wa kufanikiwa unategemea na utayari wa mtu na bidii ya mtu.
Hivi ndivyo wanasiasa na motivational speakers wanavyowadanganya. Endelea kukariri tu mkuu. Maisha yanataka connections kubwa kubwa my dear brother..
 
Kati ya mtoto wa Elon Musk na mtoto wa uswazi ni nani yupo kwenye position kubwa ya kupata mtaji wa biashara kuanzia 5,000,000??
Kupata mtaji wa million 5 sio kufanikiwa. Kufanikiwa ni uwezo wako wa kuzizalisha zile million 5.
 
Takwimu zinaonyesha asilimia kubwa ya watoto wa maskini huwa maskini, na asilimia kubwa ya watoto wa matajiri huwa matajiri. Moto wa kimasikini kufanikiwa ni mpaka ahustle kupita uwezo wa kawaida, au kwa wachache apate bahati.
 
Kuna vijana wanaotoka kwenye mazingira magumu lakini wanashinda changamoto na kufanikiwa maishani.

Unadhani ni nini kinachowasaidia kufanikisha haya licha ya changamoto kubwa wanazopitia? Na sisi sote tunaweza kujifunza nini kutoka kwao?
Kuna fate halaf kuna character ya mtu, motive and drive. Wengi hawatoboi but wale wachache wana kitu extra ambacho wengine hawana
 
Back
Top Bottom