Kwanini vijana wengine kutoka Mazingira magumu huibuka na kufanikiwa?

Kwanini vijana wengine kutoka Mazingira magumu huibuka na kufanikiwa?

Kwani wakina Bakhresa, Lugumi na Mengi walipewa connections na nani?
Hujui wewe. Wewe endelea tu kuamini kuwa fulani alikuwaga shoe shiner kabla ya kuwa billionaire. They'll tell you the truth..
 
Kama ni hivyo masikini wasinhekiwepo maana karibia watanzania wote wanaishi maisha magumu, Sasa hao vijana wako wawili kati ya laki moja ndiyo unatolea rejea kweli?
 
Mtoto ana miaka Tisa, lakini tayari anajitafutia Nguo, anatafuta mboga, akiachwa na wadogo zake hamna kinachoharibika.

Sembuse kufauli Maisha??.
 
Takwimu zinaonyesha asilimia kubwa ya watoto wa maskini huwa maskini, na asilimia kubwa ya watoto wa matajiri huwa matajiri. Moto wa kimasikini kufanikiwa ni mpaka ahustle kupita uwezo wa kawaida, au kwa wachache apate bahati.
Hapo sababu ni mazingira rafiki vs mazingira duni.
 
Baraka za MUNGU
Mungu ana nafasi kubwa katika mafanikio ya mtu, hasa kwa wale wanaomtegemea ili wafanikiwe.
Bidii na kujituma
Mafanikio ya wengi walio kwenye hali duni yanaletwa na bidii kwa kiasi kikubwa.
Mindset Nzuri
Wanaofanikiwa huwa wameweka malengo ya kufanikiwa na akili yao inawaza kufanikiwa ndio maana wanafanikiwa.
Good Timing
Ili kutoka katika hali ngumu vijana waliofanikiwa walijua kufanya jambo sahihi katika wakati sahihi wa kufanya hilo jambo.
Bahati na ngekewa binafsi
Japo wote tunahustle wakati mwingine wanaofanikiwa ni wale wenye bahati, aisee asikwambie mtu kuna watu wana bahati!
Kipaji na talanta
Vijana waliofanikiwa wapo wenye talent zao katika mambo walioyochagua kuyafanya. Wanatumia sauti zao, miguu yao, akili zao ipasavyo. Mifano ni mingi kina Nasibu Abdul,Samatta,Mwakinyo
Kwani kipaji na talanta vina tofauti gan? Hayo maneno yana maana moja em wacha ujuaji wa lugha
 
Attachments

  • Screenshot_20250121-191805~2.png
    Screenshot_20250121-191805~2.png
    83.9 KB · Views: 2
Kuna fate halaf kuna character ya mtu, motive and drive. Wengi hawatoboi but wale wachache wana kitu extra ambacho wengine hawana
Nakubaliana na wewe, Detective J kwamba kuna "character," "motive," na "drive" ambazo zinawatofautisha wale wanaofanikiwa na wengi.

Lakini je, unafikiri mambo haya huzaliwa nayo mtu au yanaweza kujengwa kwa muda kupitia mazingira na mafunzo?

Pia, umeongelea kuhusu wale "hard workers" wenye drive ya ndani. Je, unadhani mazingira magumu huwa na nafasi kubwa ya kuunda hii "drive" ya ndani? Au kuna mambo mengine?
 
Mtoto ana miaka Tisa, lakini tayari anajitafutia Nguo, anatafuta mboga, akiachwa na wadogo zake hamna kinachoharibika.

Sembuse kufauli Maisha??.
Umetoa mfano mzuri unaoonyesha nguvu ya kujitegemea hata katika umri mdogo.

Hali kama hizi mara nyingi zinawajenga kuwa na ustahimilivu na maarifa ya maisha yanayowasaidia kufanikisha mambo makubwa baadaye.
 
Nakubaliana na wewe, Detective J kwamba kuna "character," "motive," na "drive" ambazo zinawatofautisha wale wanaofanikiwa na wengi.

Lakini je, unafikiri mambo haya huzaliwa nayo mtu au yanaweza kujengwa kwa muda kupitia mazingira na mafunzo?

Pia, umeongelea kuhusu wale "hard workers" wenye drive ya ndani. Je, unadhani mazingira magumu huwa na nafasi kubwa ya kuunda hii "drive" ya ndani? Au kuna mambo mengine?
Drive inatengenezwa na experience mostly, mazingira anayokutana nayo mtu, lets say familia fukara, lakini familia hiyo hiyo ina ndugu ambao walipambana kutoka hapo

Mazingira magumu yakiendana na direct company , ndio yanajenga character ya mtu kutaka kwenda mbele zaidi

Lakini mazingira magumu pekee hayatoshi, wengi wanakuwa broken na mazingira magumu na ku give up the fight, haswa wakiwa wamezingukwa na familia, au jamii ambayo imesha give up

Lakini kwneye mazingira hayo hayo, akiwa amezungukwa na jamii, company au ndugu ambao ni wapambanaji, na ambao walitoka kwenye hali hiyo, yana mu inspire ku fight toward mafanikio
 
Back
Top Bottom