Kwanini vijiji vingi vya usukumani havina wezi kama kwingineko?

Kuna mdau wangu anaheka saba hapo, aliniarika nichukue eneo karibu yake ili tuwe na eneo hapo majirani, kumbe wale jamaa nao ni balaa. Nimewahi kukaa masaa kama 12 tu mama mmoja akapewa namba yangu..Kila siku ni kubeep na kunipigia hadi nikablock
 
1. Pesa/mali kila mtu anayo ya kutosha siyo kama zile sehemu za wazee wa sokoni 7days/week.
2. Hawana tamaa za hovyo hovyo juu ya mali ya mtu
3. Maadili mema ni jadi yao
Kuwa kabila moja kunasaidia mikoa mingine kama mkoa wa Mara wanaibiana sababu ni makabila tofauti na wana uadui kati ya kabila moja na lingine na wanapakana na wakenya wezi wakubwa wa mifugo
 
Wasukuma oyeee,
Kweli ni wachapa kazi, wakarimu, utani mwingi, na waanzilishi wa sungusungu. Ukujikanganya ukapelekwa kwenye mahakama yao utataja mpaka uhalifu aliofanya babu yako.
Mfumo wao wa utawala wa wanazengo uko vizuri sana kudhibiti uhalifu na kudhibiti mtu kuto behave kijijini kinyume na maratajio ya wanakijiji

Kuna mfanyabiashara alifungua duka kubwa tu kijijini aligoma kwenda kujitolea kutengeneza barabara wakati mkutano wa kijiji wa wanazengo ulikubaliana kuwa jumamosi waende kutengeneza watu waende na majembe nk

Akagoma akasema hiyo ni kazi ya serikali inayopokea kodi hataenda.Wanakijiji yaani wanazengo wakalima barabara baadaye kikaitishwa kikao kumjadili wakakubaliana kumuadhibu.Kuwa ni marufuku mtu yeyote kwenda kwenye duka lake au kumtembelea au kuajiriwa naye .Atakayeonekana kukaidi atalipishwa faini elfu 70 na kutengwa na jamii

Yeye akatakiwa alipe laki tano kama faini ya kukaidi maamuzi ya kijiji ya wanazengo na aombe msamaha kwenye mkutano wa kijiji ili watu waruhusiwe kwenda dukani kwake
Mwezi mzima hakuna mtu alikanyaga dukani kwake akaona eee hii kesi mbaya akawalipa laki tano yao wakaendelea kwenda dukani kwake Umoja wao kwenye vijiji vyao una uwezo mkubwa sana kuzuia uhalifu
 
Kweli wanaungwana sana japo wapo wenye tabia za hovyo lakini wengi ni watu wema tu
Wapo wabaya pia ila majority ni wema sana especially vijijini
Kuna minada nilikuwa naenda utakuta ni wao tu wanakuambia weka makoti na kila kitu hapo maana hakuna waizi hapa
Nikawauliza ikitokea nimeibiwa kitu ?
Akasema atasakwa mwizi na kuchomwa moto hii ni baada ya watu kuanza kuchanganyika
 
Hatari sana.
Nimeona kijiji kimoja walikuwa wanatii amri ya serikali kujenga maboma ya madarasa ili wao waje wamalizie. Jamaa walikomaa kila familia inaleta mchanga, kwa punda wengine wanabeba vichwani, wakachanga cement ufundi na vibarua wakajitolea yaani ndani ya mida mfupi madarasa ya kutosha na nyumba za waalimu maboma yakakamilika. Kijiji kimoja kiko mkoa wa geita.
 
Nimewahi kuishi usukumani,kule kuna ulinzi shirikishi aidha mgeni yeyote akija lazima areport kwa mwenyekiti wakijij na pia bado wanaheshimu mila na desturi (wazee wanaheshima bado mbele ya jamii).kuna jamaa mmoja akihisiwa kutunza wezi aiseeee nilishuhudia kwa macho yangu akicharazwa viboko hadi akajinyea mbele ya umati wawatu na akatozwa faini ya ng'ombe wawili palepale akatubu mbele ya halaiki yawatu kua hatarudia.
 
Mtu akitaka kujua nguvu za serikali za vijiji aende usukumani kule ndiko wanajua maana ya serikali ya kijiji ni nini.Kuwa ni serikali kamili na serikali kwelikweli sio utani
 
Mtu akitaka kujua nguvu za serikali za vijiji aende usukumani kule ndiko wanajua maana ya serikali ya kijiji ni nini.Kuwa ni serikali kamili na serikali kwelikweli sio utani
Jamaa wako siriasi sana. Hasa ukikuta wanajeshi la jadi sungusungu na kuongozi wao Sumbantale.😁😁
 
1. Pesa/mali kila mtu anayo ya kutosha siyo kama zile sehemu za wazee wa sokoni 7days/week.
2. Hawana tamaa za hovyo hovyo juu ya mali ya mtu
3. Maadili mema ni jadi yao
Watu wengi wachawi maeneo hayo mtu anajua akiiba nini kitatokea.
 
Hili la graduate kukosa mipango ya kusaka mahela ni suala linafikirisha sana. Nafikiri graduate wengi ni wachagua jembe, hivyo sio wakulima. Namaanisha wengi ni wachagua kazi badala ya kuwa direct kwenye kusaka noti. Graduates wabadili fikra!
 
Uchapakazi ndio unawafanya wasiwe wajanjawajanja kama Wazaramo! Kila mtu anaridhika na alichonacho!
 
ongw'ise ogonojwa na bhagokolo bhenabha,onsambo lokwe lofuu kwisha habar!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…