Kwanini vilabu vya Tanzania haviingizi sokoni jezi zenye majina ya mastaa wao? Je, ni ukosefu wa mipango ya kibiashara?

Kwanini vilabu vya Tanzania haviingizi sokoni jezi zenye majina ya mastaa wao? Je, ni ukosefu wa mipango ya kibiashara?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mauzo ya jezi ni miongoni mwa vyanzo vya mapato ya vilabu vya soka duniani, ingawa fedha zote zinazolipwa na mashabiki haziendi moja kwa moja kwa klabu.

Kwa kawaida, mapato hayo hugawanywa kati ya mtengenezaji wa jezi, wauzaji wa rejareja na klabu kulingana na makubaliano ya kibiashara. Hivyo, klabu hupata mapato kupitia mikataba ya udhamini na asilimia ya mauzo ya jezi (royalties), badala ya kuchukua thamani kamili ya kila jezi inayouzwa.

Mfano, vilabu vya Simba na Yanga vina nguvu kubwa ya ushawishi kutokana na kuwa na wachezaji wanaopendwa na mashabiki wengi. Umaarufu wa mastaa hao unaweza kuwa fursa kubwa ya kibiashara kwa vilabu kupitia uuzaji wa jezi zenye majina yao, lakini bado inaonekana fursa hiyo haijatumika kikamilifu.

Baadhi ya Mashabiki huenda wako tayari kununua jezi za wachezaji wanaowafuatilia na kuwaona kama alama ya kujivunia timu zao, jambo ambalo linaweza kuongeza mapato ya vilabu na kuimarisha uhusiano kati ya timu, wachezaji na mashabiki.
 
Watu wa masoko walifanya tafiti wakagundua Tanzania watu wanapenda kuandika Majina yao,ya watoto wao au ya wenza wao,.

Sio kwa sababu ulaya zinauza zikiwa na majina ya wachezaji ukafikiri na hapa itakua hivyo,.Hapa ukiandika Jezi Pacome,Chama,watu hawanunui..
 
Ni ushamba na kutojua masoko yanafanyaje, Madrid walikuwa wananunua mchezaji bei mbaya halafu wanachapisha jezi yenye jina lake muda mfupi wanskuwa wamerudisha pesa za manunuzi.
 
Back
Top Bottom