Kwanini viongozi na wanachama wa CCM hawashangilii ushindi mkubwa wanaoupata Serikali katika kesi ya Mbowe? Ukimya wao unamaanisha nini kwa Serikali?

Ni wanachama wa chadema ndiyo huwa wana kawaida ya kushangilia mabaya yanapowakuta wanachama wa vyama vingine!
Kwa nini watanzania hawashangilii gaidi linapokutwa na kesi ya kujibu? Sidhani kama gaidi limekutwa na mabaya.. Hawa magaidi wangewadhuru viongozi wa serikali wewe ungependa? Wangechoma vituo vya mafuta wewe ungependa?

Hawa hawajakutwa na mabaya.
 
Kurasa 1500 kwa siku mbili haiwezekani ndugu zangu
Huyu Jaji ametuona wa Tz vilaza sana.
 
Mbona Mimi namuonea Huruma mbowe,, Mimi CCM ,,kiukweli mbowe Siyo gaidi hili liko wazi.Mimi naona tunfanya Dhambi kumtesa Mbowe!!!
Wakubwa wako wa CCM wanauona ugaidi wa Mbowe na wenzake watatu. Lengai Ole Sabaya ndiye alikua wa kwanza kuuona ugaidi wa Mbowe, ACP Kingai anaujua ugaidi wa Mbowe, IGP Sirro anaujua ugaidi wa Mbowe.........
 
Rais ni mwajiriwa. Kudharauliwa, kusemwa, kutukanwa na kupingwa ni jambo la kawaida. Wewe unalishwa, unaveshwa, na kulindwa kwa kodi za wenye nchi, ukibali pia yanayokuja na hiyo nafasi.

Samia ni mtu wa kawaida sana. Na akicheza ataishia pabaya kuliko mtangulizi wake.
 
Usimsingizie Mama yetu. Hana hiyo akili chafu. Kesi ilishatungwa kabla hajawa Rais.
Akaunti,Mashamba na vitega uchumi mbalimbali vya Mbowe vilishahujumiwa.
Mungu huamua ni hukumu gani ampe muonevu,ila sisi binadamu hupenda sana uongo kujisafisha tukifikiri Mungu haoni!
 
Waache waandae kizazi cha waasi na wauaji. Hata kama watakuwa wamejikusanyia mali, hazitawafaa kitu. Ndugu zao watakuwa wanauliwa kama kuku. Hata wakimbilie ulaya, bado huko kutakuwa ni kunyanyaswa mpaka mwisho wa dahari.

Civilization haina option. Ni ya lazima, na mbadala wake ni mateso ya karne, vizazi na vizazi. Mkondo wa matamanio ya umma hauzuiliki kamwe.
 
Huyu bibi anajiona kawa rais anaona kafika... Bado safari ni mbichi sana. Hata 2025 anayojipigania kuivuka salama akiwa kwenye hiyo nafasi huenda asiivuke
 
Ifahamike kuwa huyu aliyetoa hii hukumu siyo jaji, ni ofisa wa TISS, sawa na alimtengulia, ambao wamepachikwa ndani ya mahakama kama kituo chake cha kazi. Huyu core profession yake ni huko TISS. Mahakamani ni mahali anapojifichia. Hawezi kuwa na weledi kwenye masuala ya mahakama.

Ifahamike marehemu aliibadilisha kabisa mahakama, kutoka kuwa chombo cha kutoa haki, na kuifanya ofisi ya TISS ambayo anaweza kuutumia kuongoza nchi kidikteta.

Kwa sasa, msajili wa mahakama ni TISS, Jaji kiongozi ni TISS, na kuna majaji 16, wote ni maofisa wa TISS. Kesi ya Mbowe na wenzake, hakuna jaji atakayeigusa, itashughulikiwa na maofisa wa TISS, ndio waliopangwa.

Wakitoa hukumu, ya haki, mjue kuwa ndivyo Rais alivyoelekeza, lakini siyo utashi wao.
 
@BeatriceKamugisha

[emoji871]CCM Hawana Tabia za kufurahia matatizo ya wenzao.
Hiyo ni tabia yenu Chadema.
Ushahidi umo humu humu JF.

[emoji871]CCM Hawana tabia za kufurahia vifo vya mahasimu wao wa kisiasa.hiyo ni tabia na hulka yenu chadema.Ushahidi uko humu humu JF.
Wakiwafungulia kesi na kuwaombea wakamatwe na kufungwa.

[emoji871]Ushahidi ni kada mkongwe wa chadema Saed Kubenea na kesi yake dhidi ya Paul Makonda.

[emoji871]CCM Hawana tabia ya kufurahia au kusakama mahasimu wao wa kisiasa wakiwafuatilia kila asubuhi mpaka usiku kucha.
Ushahidi ni wewe #Beatrice Kamugisha na wenzako dhidi ya kina #Halima mdee na wenzake.


[emoji871]CCM Wanaamini kuwa siasa ni utofauti wa itikadi na mitizamo na kuna wakati hali huweza kubadilika na hao hao waliokuwa mahasimu wakajiunga na kufanya nao kazi pamoja.ushahidi ni mawaziri na wabunge kadhaa wa sasa waliowahi kuwa makada wa chadema hapo awali kabla ya kuhamia CCM.

[emoji871]CCM Hawana tabia ya kukusanya mashabiki na kuwakodishia magari kwenda mahakamani kuzomea.
Kama tulivyoona pale Arusha kwa Sabaya.

[emoji871]CCM ina wanachama ambao wana majukumu mengi ya kifamilia.
Hawawezi kupata muda wa kwenda kushabikia mambo yasiyo na tija kwa familia zao.

[emoji871]Mbowe anashitakiwa na Jamhuri na sio CCM.
Iweje sasa kwamba wana CCM waingie mitaani kushabikia au kufurahia Mbowe kukutwa na kesi ya kujibu?

[emoji871]Hiyo ingetokea kama angekuwa ni mwenyekiti wa CCM.
Ndie amekutwa na hayo masahibu.
Chadema leo ungewaona wakifurahi kila kona.Kuanzia kwenye nyama choma mpaka huku mitandaoni.

[emoji871]Ila nimalizie kwa neno moja......

[emoji871]Mama anajua kucheza karata zake.

[emoji871]Aliwafurahisha sana!
kwa kumtumbua na kisha kumuacha hewani Sabaya.

[emoji871]Kisha akawasikitisha sana kwa kumuachia Mbowe nae Sheria ifuate mkondo wake.

[emoji871]Amewafurahisha sana kwa kukubali kukutana na Makamu mwenyekiti wa chadema.
Mh Lissu kule Ubelgiji.

[emoji871]Lakini amewasikitsha sana kwa kukataa ombi la kumuachia mwenyekiti wa chadema Mh Freeman Aikaeli Mbowe..

[emoji871]CCM ni wastaarabu na wanawachukulia watanzania wote kama ndugu.
Ushahidi ni jinsi wanavyoshughulika na Mbunge mstaafu wa Chadema aliyelazwa ICU huko Muhimbili kwa sasa.

[emoji871]Ingawa CCM sio malaika ni binadamu wenzetu na kila mmoja anayo hulka yake.hivyo sio wote ni wasafi.
Ndio maana kuna misuguano mikubwa ndani yake saa ingine kuzidi hata iliyopo baina ya CCM na vyama vingine.

[emoji871]Hivyo humo humo CCM kuna baadhi ya kundi la wenye Roho za kifedhuli na kifisadi ambao kwa ujumla wao.
Wanaweza kuwa wanaendesha mambo yasiyokuwa ya kistaarabu na kinyume na sheria za nchi.

[emoji871]Na hao wako radhi kumdhuru yeyote bila kujali ni wa chama chao CCM au ni wa upinzani.wako radhi kushirikiana hata na upinzani nje ya CCM ili tu watimize malengo yao.
Kwao ni maslahi yao kwanza...mengine baadae.

[emoji871]Na hao ndio maadui wakubwa wa nchi yetu .
Watu wa aina hii wako na wanapatikana katika vyama vyote nchini.

[emoji871]Ila ni rahisi kuwabaini walioko CCM,kwa sababu CCM inaongoza nchi na ni rahisi kuwa screen!
 
Kelele na ngojera nyingi za nn 2030 itaongea. Je kesi ya mbowe imewajenga Chadema au imeidhofisha Ccm saiv mnapoteza tu bando

Kuna Tanzania harisi na Tanzania ya Jamii forum sasa lazma piq mjue kuzitofautisha Tanzania ya wananchi na Tanzania ya magreat thinker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…