Kwanini viongozi pamoja na mishahara mizuri bado wanapewa nyumba na magari?

Kuwazuia na matamaa lakini kumbe tofauti kilakitu wanacho ufisadi kwao ni nguzo ya uongozi
 
Tulipokosea ni pale tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma
 
Nani mlikunywa nao ugimbi
 
Nani mlikunywa nao ugimbi
Yule dr alikuwa na degree nyingi mno sasa ni marehemu kikubwa hapa point yangu nafasi zao zinahitaji wapate hizo facility tusiwachungulie uongozi sio jambo rahisi ni mzigo wanatakiwa kukaa sehemu za utulivu
 
Nchi nyingi ipo hivyo,
Relax.
Nchi zote haziko hivyo, tuchukulie Ujerumani ambao kwa Pato wanatupita kwa kila kitu, mbunge analipwa 10,012.89 Euro kwa mwezi na Kanzela analipwa 351,552 Euro kwa mwaka ambayo ni sawa na29,296€ kwa mwezi. Hawa wote wanalipa nyumba kwa Pesa Zao, gari wanayotupia wanapewa leasing, maana yake wanakatwa kila mwezi kwenye mishahara yao
 
Iii wasiwapandishie watumishi wa umma mishahara.
 
Kama unaona ni rahisi na wewe kuwa kiongozi..ili upewe hayo magari na nyumba
 
Kumbuka alichofanya Kingwangala alipokuwa Waziri wa Afya, alifika ofisini alfajiri na kuwazuia getini wale wote waliofika baada ya saa 1:30
 
Stahiki za viongozi.Sema hivi hao viongozi ni wengi Sana kiasi kwamba imegeuka ni mzigo kwa walipa Kodi.
 
Mkuu; Hayo uliyotaja Inapewa OFISI sio mtu. Huyo mtu akiondoka (kwa Uhamisho, Kustaafu, Kifo n.k.) Vinabaki Ofisini na kazi inaendelea.
Wanatamba navyo tu lakini sio vyao.
Ofisi inapewaje nyumba ya kuishi au gari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…