Kwanini viongozi wa dini huwa hawakemei huu uonezi wa Polisi?

Bapalidako

Member
Joined
Aug 6, 2024
Posts
79
Reaction score
166
Naamini hawa Viongozi wa CHADEMA ni waumini, tena asilimia kubwa ni wakristo kwa nini Viongozi wa Dini wamekaa kimya au wanaona walichofanyiwa walistairi?
 
Kila siku nazidi kubaini kuwa hizi Dini kwa asilimia kubwa ni Matawi ya serikali kwa sababu viongozi wa serikali hata wafanye hujuma kali na nyingi kiasi gani, viongozi wetu wa Dini huwa hawana habari.

Nafikiri kuacha kabisa kwenda Kanisani kwa sababu huwezi ukawa na viongozi wa Dini ambao wakiwa Makanisani wanajifanya watu wema wakati yanapotokea madhulumu wanaona haya kutoa matamko ya kulaani.

Viongozi wetu wa Dini nawaasa tena kuwa, kuweni makini, mstake tu sadaka za waumini wenu.
 
Maaskofu Watetee Matapeli ya Kisiasa kwa mgongo wa Demokrasia waache kutetea mamilioni ya wananchi waliouziwa sukari ya Tsh1,900 kwa Tsh4,500 si utakuwa wendawazim.
 
Naamini hawa Viongozi wa CHADEMA ni waumini, tena asilimia kubwa ni wakristo kwa nini Viongozi wa Dini wamekaa kimya au wanaona walichofanyiwa walistairi?
Nadhani kosa wanalo hao Viingozi wa CHADEMA pamoja na Wapinzani wengine. Hivi ni kwa nini hao Wapinzani nao wasijiandalie "mechanism" ya wao kuweza kujitetea na kujihami na hizo dhuluma au hujuma ambazo wamekuwa wakifanyiwa na Jeshi la Polisi au Watawala waliopo???Wanasubiri nini kufanya hivyo???
 
Hakuna viongozi wa dini kuna wajasilia dini. Ni takataka tupu zinakula kwa mgongo wa Mungu who does not exist anyway!

On the other hand , hwa wa dini ile (siyo wote) wanasema huyu ni mwenzao katika dini kigugumizi kinakuwa kikubwa, lakini UOVU WA POLISIS WANAUONA FIKA!
 
Nadhani kosa wanalo hao Viingozi wa CHADEMA pamoja na Wapinzani wengine. Hivi ni kwa nini hao Wapinzani nao wasijiandalie "mechanism" ya wao kuweza kujitetea na kujihami na hizo dhuluma au hujuma ambazo wamekuwa wakifanyiwa na Jeshi la Polisi au Watawala waliopo???Wanasubiri nini kufanya hivyo???
Ni kweli kabisa. Haiwezekani kila mwaka kulia lia tu, walitakiwa wawe wameshaandaa utaratibu binafsi wa kujilinda. Miaka yote utasikia mara tumehujumiwa uchaguzi, lakini hakuna hatua kali wanazochukua ili kukomesha kabisa ujinga wanaofanyiwa.
 
Naamini hawa Viongozi wa CHADEMA ni waumini, tena asilimia kubwa ni wakristo kwa nini Viongozi wa Dini wamekaa kimya au wanaona walichofanyiwa walistairi?
Noma sana hizi dini ni kwa ajili ya kukusanyacSadaka tu
 
Back
Top Bottom