Uchaguzi 2020 Kwanini viongozi wetu wa Dini wanatusisitiza sana tudumishe amani yetu, lakini wanashikwa na kihoro kuwaambia wanasisiasa wetu watende haki?

Nilimsikia ask Mwakjibolwa Jana akiomba Mungu miaka mingine mitano tukiongozwa katika Haki na amani nikajiuliza hiyo miaka mitano iliyopita tulikuwa na amani ipi? Wakati waziri wa Mambo ya ndani hakuwahi kukemea hata Mara moja utekaji, uuwaji,na hata dhuruma iliyofanywa kwa vyama vya upinzani? Au wanafikiri wtz wamesahau? Mi naamini Haki ndo inazaa amani hata ktk nyumba Zetu.Huyu mama kiwanga Kama anastahili Haki mpeni vielelezo ambavyo amevitoa vinaonyesha kaonewa
 
Utashangaa nikikwambia zaidi ya 60% ya waislamu wenzangu watapigia kura CCM
Angalia miji kama Tanga. Pwani. Lindi n,k
Huko CCM oyeee
Tatizo la waislamu wenzangu wengi wetu ni ujinga na umaskini... Darasa la saba sio elimu
 
Those who use the name religious leaders are nothing but wolves in sheep skins.
 
Hata hivyo asimgeuze Mungu wetu kama mtani wake..........

Dawa.yake ni wananchi tujitokeze tarehe 28 mwezi huu kumpigia kura yule mwenye Sera ya maendeleo ya watu na tuimwage kabisa Pombe ambayo ni "unfit for human consumption"
Naunga mkono hoja
 
Ni dhahiri kuwa hata Mwalimu Nyerere ni shabiki wa sera ya CHADEMA.

Kwa kuwa wakati wa uhai wake alikuwa akiitangaza Sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.............

Nakumbuka aliwahi kusema kuwa Maendeleo ni lazima yawe Maendeleo ya watu.

Vile vile aliwahi kusema kuwa huwezi ukajiita upo huru, wakati huna uhakika ya maisha yako kesho yake yatakuwaje na akaendelea kusema kuwa mwananchi ni lazima awe "assured" na uhuru wa maisha yake.

Mwalimu Nyerere alikuwa mshabiki mkubwa wa Sera ya People's Power
 
Viongozi wa dini gani? Kama ni BAKWATA wanajulikana wazi kuwa ni vibaraka wa CCM, na kama ni CCT ndio wale wake tu viongozi waliojaa unafiki
Niliwasikia Jana wale viongozi wa BAKWATA wa mkoa wa Mtwara, wakitoa tamko la kumuunga mkono John Pombe Magufuli!

Fikiria angetokea kiongozi mwingine wa dini atoe tamko la kumuunga mkono Tundu Lissu, uone namna viongozi mbalimbali wa dini watakacyomshukia na kumwambia kuwa watenganishe siasa na dini
 
Hao ni makada wa ccm waliopachikwa kwenye Dini ili kulinda maslahi ya ccm
 
Ivi mkuu samahani nasikiaa Sana hii habari kwan Ivi mkuu samahani nasikia sana hyo habari ivi Wana kosa gani hao mashehe mpaka wakakamatwa?
 
Ivi mkuu samahani nasikiaa Sana hii habari kwan
Ivi mkuu samahani nasikia sana hyo habari ivi Wana kosa gani hao mashehe mpaka wakakamatwa?
Wanatuhumiwa makosa ya ugaidi lakini ukweli ni kwamba masheikh wengi wamekamatwa kwa sababu wametofautuana na taasisi moja ya kinafiki inayoitwa BAKWATA
Magufuli amewapa BAKWATA uezo wa kumfunga muislamu yeyote kwa tuhuma za ugaidi na ni kosa lisilo na dharma
BAKWATA wanafanya ubadhirifu na Mali ya waislamu ukiuliza mapato na matumizi unajikuta upo jela
Wallah magufuli ametesa Sana watu
 
Duu kwa hyo kumbe hao waliokamatwa inaonekana ni wakweli , hao walio kwenye BAKWATA ndo wanazingua
 
Imeandikwa kwenye Biblia takatifu, katika kitabu cha Mithali, sura ya 14:34 nanukuu kama ifuatavyo "Haki huliinua Taifa, Bali dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho.
Wale wachache wanaothubutu kutangaza uonevu na kutetea haki, tumeona yanayowafika. Kuandamwa, kutishwa na kunyooshewa vidole kuwa wanaleta uchochezi.
Huwezi kuhimiza amani ikiwa huenda haki. Tutajinasibu kuwa sisi ni kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa wa amani, lakini hatuna amani wala imani na tawala zetu hizi. Siku uvumilivu utakapowashinda wananchi na kuacha uoga, ndio tutajuwa kuwa amani yetu ni kidonge cha dawa kilichochovywa sukari na watu watakitema badala ya kuendelea **** na kumezea.
 
Yakaisari mwachie kaisari na ya mungu muachie Mungu.................Wahenga wanasema Usifuate matendo yangu fuata maneno yangu
 
Haki utafutwa mahakamani sio kwa viongozi wa serikali au wa dini.
 
Ni wanafiki wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…