Uchaguzi 2020 Kwanini viongozi wetu wa Dini wanatusisitiza sana tudumishe amani yetu, lakini wanashikwa na kihoro kuwaambia wanasisiasa wetu watende haki?

Uchaguzi 2020 Kwanini viongozi wetu wa Dini wanatusisitiza sana tudumishe amani yetu, lakini wanashikwa na kihoro kuwaambia wanasisiasa wetu watende haki?

Imeandikwa kwenye Biblia takatifu, katika kitabu cha Mithali, sura ya 14:34 nanukuu kama ifuatavyo "Haki huliinua Taifa, Bali dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.

Kwa maandiko hayo ya kwenye Biblia takatifu, maana yake ni kuwa huwezi kuitenganisha HAKI na AMANI na kwa maana nyingine vitu hivyo ni sawasawa na chanda na pete.

Hata hivyo tumekuwa tukiwasikia mara nyingi, viongozi wetu wa kidini wakituhimiza sana sisi waumini wetu tuidumishe amani ya nchi hii, tena wamekuwa wakienda mbali zaidi na kutuonya kuwa amani ya nchi hii ikitoweka, kuirejesha itakuwa ngumu sana!

Ndipo hapo ninapowauliza hao viongozi wa Dini, ambao naamini wao wanavisoma sana hivyo vitabu vya dini na wana uelewa mkubwa zaidi yetu sisi waumini wa madhehebu hayo, kuwa ni kwanini wanatusisitizia sana sisi waumini wao tudumishe amani ya nchi hii, lakini wanashikwa na "kigugumizi* kuwasisitizia sana viongozi wetu wa kisiasa, nao watimize wajibu wao muhimu sana wa kutenda haki, pale wanapolitumikia Taifa hili?

Hivi ni nani asiyejua kuwa viongozi wetu wa kisiasa, wanaziminya waziwazi HAKI za wananchi, wanapotekeleza majukumu yao?

Tunafahamu pia nchi yetu imepata msamiati mpya, katika utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 ya " watu wasioujulikana" ambao haukuwepo katika awamu za serikali zilizopita!

Tunaambiwa na Jeshi letu la Polisi, kuwa waliomwua aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, miaka zaidi ya 4 iliyopita, ni WATU WASIOJULIKANA.
Kwa kuwa hadi Leo hawajapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Tunaelezwa pia na Jeshi letu la Polisi kuwa watu waliomteka, msaidizi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeaman Mbowe, BenSaanane, zaidi ya miaka 4 iliyopita, ni WATU WASIOJULIKANA!

Tumejuliishwa pia na Jeshi letu la Polisi nchini, watu waliomteka, mwandishi wa habari maarufu nchini, Azory Gwanda, zaidi ya miaka 3 iliyopita, ni WATU WASIOJULIKANA!

Tunaelezwa pia na Jeshi letu la Polisi nchini kuwa watu waliomminia risasi mfululizo zaidi ya 15 mwilini mwake, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, eti na wao, ni WATU WASIOJULIKANA!

Tunaambiwa na Jeshi letu la Polisi nchini kuwa watu waliomteka, mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, eti na hao ni WATU WASIOJULIKANA!

Matukio ya kuuawa watu, kutekwa na kupotea, ni mengi sana, katika utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 na umevunja rekodi ya serikali zote za awamu zilizopita, tokea tupate Uhuru wetu!

Tumeshuhudia pia Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, akitamba kuwa chama chake, kitaendelea kutumia vyombo vya dola vilivyopo nchini, ili kuendelea kubaki kwenye dola!

Hivi hayo ni maneno aliyoyatamka Dkt Bashiru Ally ni ya kuyatamka hadharani au ni ulevi tu wa madaraka?

Ni dhahiri kuwa maneno hayo aliyoyatamka Dkt Bashiru Ally hadharani, ndiyo yanayochochea kwa kiasi kikubwa, uvunjifu wa amani hapa nchini na kutaka kuikimbiza amani tuliyo kuwa nayo hapa nchini tokea tupate Uhuru wetu toka kwa mkoloni
Nilimsikia ask Mwakjibolwa Jana akiomba Mungu miaka mingine mitano tukiongozwa katika Haki na amani nikajiuliza hiyo miaka mitano iliyopita tulikuwa na amani ipi? Wakati waziri wa Mambo ya ndani hakuwahi kukemea hata Mara moja utekaji, uuwaji,na hata dhuruma iliyofanywa kwa vyama vya upinzani? Au wanafikiri wtz wamesahau? Mi naamini Haki ndo inazaa amani hata ktk nyumba Zetu.Huyu mama kiwanga Kama anastahili Haki mpeni vielelezo ambavyo amevitoa vinaonyesha kaonewa
 
Huwa nashangaa Sana muislamu kumshabikia mtu anaewatesa na kuwanyanyasa Sana waislamu, musiba angekuwa ni muislamu siku nyingi Sana angeshaozea ndani, lakini wengine wakitoa maoni yao jela zinawahusu.
Kwann mnaendekeza Sana njaa ya vitu vidogovidogo hata kwa kuzidhalilisha dini zenu?
Utashangaa nikikwambia zaidi ya 60% ya waislamu wenzangu watapigia kura CCM
Angalia miji kama Tanga. Pwani. Lindi n,k
Huko CCM oyeee
Tatizo la waislamu wenzangu wengi wetu ni ujinga na umaskini... Darasa la saba sio elimu
 
Those who use the name religious leaders are nothing but wolves in sheep skins.
 
Hata hivyo asimgeuze Mungu wetu kama mtani wake..........

Dawa.yake ni wananchi tujitokeze tarehe 28 mwezi huu kumpigia kura yule mwenye Sera ya maendeleo ya watu na tuimwage kabisa Pombe ambayo ni "unfit for human consumption"
Naunga mkono hoja
 
Ni dhahiri kuwa hata Mwalimu Nyerere ni shabiki wa sera ya CHADEMA.

Kwa kuwa wakati wa uhai wake alikuwa akiitangaza Sera ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.............

Nakumbuka aliwahi kusema kuwa Maendeleo ni lazima yawe Maendeleo ya watu.

Vile vile aliwahi kusema kuwa huwezi ukajiita upo huru, wakati huna uhakika ya maisha yako kesho yake yatakuwaje na akaendelea kusema kuwa mwananchi ni lazima awe "assured" na uhuru wa maisha yake.

Mwalimu Nyerere alikuwa mshabiki mkubwa wa Sera ya People's Power
 
Viongozi wa dini gani? Kama ni BAKWATA wanajulikana wazi kuwa ni vibaraka wa CCM, na kama ni CCT ndio wale wake tu viongozi waliojaa unafiki
Niliwasikia Jana wale viongozi wa BAKWATA wa mkoa wa Mtwara, wakitoa tamko la kumuunga mkono John Pombe Magufuli!

Fikiria angetokea kiongozi mwingine wa dini atoe tamko la kumuunga mkono Tundu Lissu, uone namna viongozi mbalimbali wa dini watakacyomshukia na kumwambia kuwa watenganishe siasa na dini
 
Hao ni makada wa ccm waliopachikwa kwenye Dini ili kulinda maslahi ya ccm
 
Mimi sijui Sana Habari za viongozi wa dini ya Kikristo ila kwa viongozi wetu wa kiislamu tatizo ni UNAFIKI na NJAA
Mfano ::Mwanaharakati mkubwa wa kiislamu Sheikh Issa Ponda kabla kidogo ya kampeni alitoa '' waraka wa maimamu' wenye kurasa 30!!! Pomoja na mambo mengine alizungumzia mamia ya masheikh waliopo jela bila dhamana wala kupelekwa mahakamani na akazungumzia mateso wanayo tapata mpaka wengine wamehasiwa kabisa na wengine kua vichaa kwa sababu ya mateso makali kama haitoshi kaelezea vizuri kuhusu wale 72 walikamatwa na SMZ kabla ya JPM kua rais na jinsi gani walivyoletwa Tanganyika.. Vile vile ameeleza Kwa ufasaha jinsi wimbi la kamatakamata lilivyo anza kila mkoa Tanganyika mpaka kufika kuonyesha takwimu ya mamia waliopo jela na namba za kesi zao... Utafiti unaonyesha kuanzia mwaka 2016 Tanzania pamekamatwa watu wengi kwa tuhuma za ugaidi kuliko Afghanistan!!!!!!
Matokeo yake Sheikh Ponda alikamatwa na kupelekwa sehemu isiojulikana baada ya muda akaonekana anaendesha BMW mpya na mambo yake Safi Sana
Hivi Sasa yeye na jopo lake ni wanaharakati mkubwa wa JPM na hata ile michango ya kuwasaidia Familia za waliopo jela imepigwa stop 🛑 maana wanaamini inaweza kuleta hisia za kumchukia JPM
Hawa ni "viongozi wa dini'' we have long way to go
Hapo bado BAKWATA ukisikia vituko utashangaa
Ivi mkuu samahani nasikiaa Sana hii habari kwan

Ivi mkuu samahani nasikia sana hyo habari ivi Wana kosa gani hao mashehe mpaka wakakamatwa?
 
Ivi mkuu samahani nasikiaa Sana hii habari kwan
Ivi mkuu samahani nasikia sana hyo habari ivi Wana kosa gani hao mashehe mpaka wakakamatwa?
Wanatuhumiwa makosa ya ugaidi lakini ukweli ni kwamba masheikh wengi wamekamatwa kwa sababu wametofautuana na taasisi moja ya kinafiki inayoitwa BAKWATA
Magufuli amewapa BAKWATA uezo wa kumfunga muislamu yeyote kwa tuhuma za ugaidi na ni kosa lisilo na dharma
BAKWATA wanafanya ubadhirifu na Mali ya waislamu ukiuliza mapato na matumizi unajikuta upo jela
Wallah magufuli ametesa Sana watu
 
Duu kwa hyo kumbe hao waliokamatwa inaonekana ni wakweli , hao walio kwenye BAKWATA ndo wanazingua
 
Imeandikwa kwenye Biblia takatifu, katika kitabu cha Mithali, sura ya 14:34 nanukuu kama ifuatavyo "Haki huliinua Taifa, Bali dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho.
Wale wachache wanaothubutu kutangaza uonevu na kutetea haki, tumeona yanayowafika. Kuandamwa, kutishwa na kunyooshewa vidole kuwa wanaleta uchochezi.
Huwezi kuhimiza amani ikiwa huenda haki. Tutajinasibu kuwa sisi ni kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa wa amani, lakini hatuna amani wala imani na tawala zetu hizi. Siku uvumilivu utakapowashinda wananchi na kuacha uoga, ndio tutajuwa kuwa amani yetu ni kidonge cha dawa kilichochovywa sukari na watu watakitema badala ya kuendelea **** na kumezea.
 
Yakaisari mwachie kaisari na ya mungu muachie Mungu.................Wahenga wanasema Usifuate matendo yangu fuata maneno yangu
 
Haki utafutwa mahakamani sio kwa viongozi wa serikali au wa dini.
 
Ni wanafiki wakubwa

Back
Top Bottom