Kwanini vitu vinapanda bei sana siku hizi?

mgendege

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2020
Posts
322
Reaction score
388
Pole na majukumu wa Tanzania wenzangu kwa kulijenga taifa letu.

Jamani huku kwetu mkoa wa Songwe sasa ndoo ya mafuta ya kupikia elfu themanini nayo ni Toka nchi jirani ya kwetu ni elfu themanini na tatu na hayapatikani .sukari ya Tanzania Hamna kabisa napo ukibahatika ni tsh 3,500kg.

Cement ndo usiseme elfu kumi na nane na kuendelea. Sabuni mche family 1,200tsh na huku hela ni Kilimo mahindi, karanga, maharage.

Bei za mazao ziko chini hazipandi mfano mahindi debe 7,300 toka mwaka Jana ndo yamepanda sasa msimu wa kupanda Bei ya mbolea iko juu na mbegu. Mwenye kununua mzao lazima uwe na mashine za TRA,

Vipi huko kwenu Hali Ipo Kama huku?
 
Sababu zinaweza kuwa nyingi zinazoweza kupelekea hali hiyo kama uhitaji kuwa mkubwa kuliko uzalishwaji, gharama za uendeshaji, kupungua kwa uzalishaji hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, uchaguzi, athari za corona nk

Hali inaweza kudumu kwa kipindi cha muda hivi ikaja kustabilize hapo baadaye. Cha kufanya anza kutumia vitu vya bajeti ukiweza nunua uweke akiba huku ukipima hali
 
Tatizo ni pesa hakuna kabisaaa
 
JPM saaaaasfiiiii,saaafiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hatuhitaji uchambuzi wako
Ni mitano tena
Kula Tano🖐
 
Wanasema mitano tena 🤸🦹
 
Wewe unalalamika vitu vidogo namna hiyo. Huku kwetu hotel ya chumba Cha dola Mia tano inakodishwa kwa wanafunzi kwa chini ya dola kumi kwa siku. Ma suplaya wa hoteli wamepigwa chini,
Wafanyakazi wa hoteli chali
Kodi iliyokua inalipwa hamna hata walinzi hawana kazi.
Nasikia eti ndio uchumi wa Kati unavyokua. Watu kukosa kazi, biashara kufungwa, Bei ya mazao kudorora na bidhaa za viwandani kupaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…