Kwanini VVD,Alison Becker na Salah na sio Bernardo Silva?

Ngumbaru

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2018
Posts
495
Reaction score
677
VVD Alison Becker na Salah wameshinda taji moja tu msimu uliopita,wameshinda UEFA Champions League wakiwa na klabu ya Liverpool.
Bernardo Silva ameshinda mataji yafuatayo akiwa na Man City pamoja na timu ya taifa ya Ureno:
1) F.A Cup
2) Carabao Cup
3) Ngao ya Hisani
4) EPL
5) European Nations League. Kombe hili ameshinda akiwa na timu ya taifa ya Ureno,pia yeye ndio mchezaji bora wa mashindano.
Kwahiyo Bernardo Silva amekuwa na msimu wenye mafanikio akiwa na klabu pamoja na timu ya taifa.
Naomba kuuliza,sababu zipi zinawafanya VVD,Alison Becker na Salah kupewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon D'or?
Kwanini Bernardo Silva azungumziwi kabisa?
 
Sa huoni bernaldo silva kama ameshinda kombe moja tu la epl na mauchafu kibao. Wengine hao wameshinda kombe safi uefa bila uchafu
Ha ha ha!
Sneijder alibeba UEFA na bado Ballon D'or ikachukuliwa na Messi.
Ribery alibeba UEFA na bado Ballon D'or akabeba Ronaldo.
Nahitaji facts sio pumba mkuu.
 
Mchango wake binafsi kwenye mafanikio ya ckub sio mkubwa kiasi cha kupewa tuzo hiyo. Alson barker kwa timu na taifa kachukua uefa na kaingia fainali copa amerika ila binafsi amechukua golden gloves epl , kachukua golden gloves uefa na golden gloves copa America. The same to van dyke pamoja na mafanikio club na taifa ila yy binafsi kachukua mchezaji bora epl. Bernardo Silva sioni mafanikio yake binafsi ni kama anabebwa na taifa na club.
 
Kuwa serious basi mkuu.
VVD amepata mafanikio gani timu ya taifa?
Kombe walilobeba Ureno Bernardo Silva ndio mchezaji bora wa mashindano.
Bernardo Silva ndio mchezaji bora wa msimu katika timu ya Man City.
Halafu naona umewazungumzia VVD na Alison Becker tu.
Salah vipi,mbona haujataja alichomzidi Bernardo?
Mchango wa Bernardo Silva kwenye mafanikio ya Man City ni mdogo!?
Mimi naamini unatania ndugu, wala haupo serious.
 
UCL > EPL + FA + Carabao +.....n

UCL = Euro

WC > UCL

therefore.....

WC > UCL = Euro > EPL + FA + Carabao +....n

kapish??
 

Unaulizia mchango binafsi wa Silva? Mkuu hua unatizama Mpira?
 
UCL > EPL + FA + Carabao +.....n
UCL = Euro
WC > UCL
therefore.....
WC > UCL = Euro > EPL + Carabao +....n
kapish??
Nilijua tu watakuja watu wa aina yako.
Sneijder ameshinda kombe la UEFA na Inter Milan pia bila kusahau akaifikisha Uholanzi fainali kombe la Dunia,lakini tuzo ya Ballon D'or akabeba Messi.
Ribery ameshinda kombe la UEFA na Bayern Munich,lakini Ronaldo akabeba tuzo ya Ballon D'or.
Leta hoja nyingine ndugu.
 
plus personal stats.,
 
Mafanikio binafs ndio hoja kuu,pale city asingecheza Silva bado city angekuwa na nafas kubwa ya kubeba EPL, na hizo cups nyingine ,ndio hichi kilichomnyima rahim tuzo mbele ya VVD, pale liver ukimtoa vvd sidhan kama wangebeba UCL, hivo ni rahisi sana BEKER AU VVD Kutwaa balloon dor , kuliko silver maana wao binafs mchango wao umeonekana , wangekosekana wabadala wao wangefanya kama wao? Kwa city asingecheza Silva Bernardo , bado mahrez , de bruyne hata rahim au Jesus wangekava vzr hiyo namba na city isingeonekana dhaifu.

Hivo wanamichezo tuna prefer VVD AU BEKER kuchukua balon dor ,
 
Kwahiyo Bernardo Silva hastahili tuzo kwasababu timu yake ina kikosi kipana,sio?
 
Umeleta mada tujadiri

Au tukuunge mkono ?

Tuambie mkuu [emoji3]
 
Usiwapangie watu wazungumze nini na wamzungumzie nani, hata wewe na wenzako mnaweza kumzungumzia mnayemtaka, tatizo umeleta mada huku umechagua upande kwahiyo na wewe usiwapangie watu upande wautakao, vvd ana mechi nyingi sana ambazo liver wangemkosa pengine wangepoteza lakini huyo jamaa yako mtafutie mechi mbili ambazo angekosa basi cty wangepoteana
 
Umeleta mada tujadiri
Au tukuunge mkono ?
Tuambie mkuu [emoji3]
Nimeileta mada ambayo tayari nina upande.
Naamini una elimu kidogo mkuu,hivyo unajua maana ya ninachokiongelea.
Ni mada ambayo nimeileta katika mtindo wa swali.
Katika mada hii,mimi naamini Bernardo Silva alikuwa na msimu bora kuliko VVD na Salah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…