Kwanini VVD,Alison Becker na Salah na sio Bernardo Silva?

Kwanini VVD,Alison Becker na Salah na sio Bernardo Silva?

Nimeileta mada ambayo tayari nina upande.
Naamini una elimu kidogo mkuu,hivyo unajua maana ya ninachokiongelea.
Ni mada ambayo nimeileta katika mtindo wa swali.
Katika mada hii,mimi naamini Bernardo Silva alikuwa na msimu bora kuliko VVD na Salah.
Kabisa mkuu

Elimu yangu ni ndogo ngoja tuwaache nyie wenye elimu mkubwa [emoji28]
 
VVD Alison Becker na Salah wameshinda taji moja tu msimu uliopita,wameshinda UEFA Champions League wakiwa na klabu ya Liverpool.
Bernardo Silva ameshinda mataji yafuatayo akiwa na Man City pamoja na timu ya taifa ya Ureno:
1) F.A Cup
2) Carabao Cup
3) Ngao ya Hisani
4) EPL
5) European Nations League. Kombe hili ameshinda akiwa na timu ya taifa ya Ureno,pia yeye ndio mchezaji bora wa mashindano.
Kwahiyo Bernardo Silva amekuwa na msimu wenye mafanikio akiwa na klabu pamoja na timu ya taifa.
Naomba kuuliza,sababu zipi zinawafanya VVD,Alison Becker na Salah kupewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon D'or?
Kwanini Bernardo Silva azungumziwi kabisa?
UEFA Value yake ni kubwa kuliko hivo vijikombe vingine
 
Usiwapangie watu wazungumze nini na wamzungumzie nani, hata wewe na wenzako mnaweza kumzungumzia mnayemtaka, tatizo umeleta mada huku umechagua upande kwahiyo na wewe usiwapangie watu upande wautakao, vvd ana mechi nyingi sana ambazo liver wangemkosa pengine wangepoteza lakini huyo jamaa yako mtafutie mechi mbili ambazo angekosa basi cty wangepoteana
Ha ha ha!
Ulitaka mtu akinipa jibu nikubali tu,bila hata kuchallenge jibu lake.
Mechi mbili ambazo Bernardo asingecheza Man City angepoteza ni mechi dhidi ya Liverpool na mechi dhidi ya Spurs.
Narudia tena,simpangii mtu nini cha kusema,isipokuwa nahoji ukweli wa anachokisema.
 
Haujanielewa ndugu.
Wala sijakudharau,kwangu hakuna mwenye elimu kubwa zaidi ya Mungu.
Umesema una dhani nna elimu kidogo mkuu wangu na kiongozi

Mi nimechukulia poa tu [emoji28]

Maana hata haunijui ! [emoji28][emoji28][emoji41]
 
Ha ha ha!
Ulitaka mtu akinipa jibu nikubali tu,bila hata kuchallenge jibu lake.
Mechi mbili ambazo Bernardo asingecheza Man City angepoteza ni mechi dhidi ya Liverpool na mechi dhidi ya Spurs.
Narudia tena,simpangii mtu nini cha kusema,isipokuwa nahoji ukweli wa anachokisema.
Kweli mkuu.
Mechi aliyocheza B silva dhidi ya liverpool alihustle sana bila yeye city asingeshinda. Hata mechi dhidi ya man u nayo pia
 
Alison ni kipa bora

UEFA

EPL

Copa America

Kachukua UEFA

saivi wanaongoza 1 fainali copa america

Acha kufananisha upuuzi
 
UEFA Value yake ni kubwa kuliko hivo vijikombe vingine
Kwani Ballon D'or ni tuzo kwaajili ya wachezaji walioshinda kombe la UEFA tu?
Ha ha ha!
Kwa majibu mepesi kama haya halafu mtu anataka nikubali tu,nikihoji nakuwa nakupangia nini cha kujibu.
 
Alison ni kipa bora
UEFA
EPL
Copa America
Kachukua UEFA
saivi wanaongoza 1 fainali copa america
Acha kufananisha upuuzi
Hivi umemuona Alisson tu katika uzi huu?
Nimemzungumzia Alisson peke yake?
 
Kwani Ballon D'or ni tuzo kwaajili ya wachezaji walioshinda kombe la UEFA tu?
Ha ha ha!
Kwa majibu mepesi kama haya halafu mtu anataka nikubali tu,nikihoji nakuwa nakupangia nini cha kujibu.
Add hapo na mchango wako binafsi,ubora wako,Allison becker anabeba hio bila mjadala.achana na masuala ya kombe la FA,leo anaongeza na Copa America na Golden glove ya 3
 
Umesema una dhani nna elimu kidogo mkuu wangu na kiongozi
Mi nimechukulia poa tu [emoji28]
Maana hata haunijui ! [emoji28][emoji28][emoji41]
"Naamini una elimu kidogo mkuu,hivyo unajua maana ya ninachokiongelea"

Kama uneona dharau katika hiyo sentensi,basi nina mashaka na uwezo wako wa kuitumia lugha ya Kiswahili mkuu,huenda ni lugha ambayo hauitumii mara kwa mara.
Sina muda wa kumdharau mtu nisiyemfahamu.
 
Add hapo na mchango wako binafsi,ubora wako,Allison becker anabeba hio bila mjadala.achana na masuala ya kombe la FA,leo anaongeza na Copa America na Golden glove ya 3
Vipi kuhusu VVD na Salah?
Sijamzungumzia Alisson Becker peke yake mkuu.
 
Vipi kuhusu VVD na Salah?
Sijamzungumzia Alisson Becker peke yake mkuu.
VVD ana tuzo ya mchezaji bora kwenye ligi nae ana golden medal ya Uefa,anachuana na Alison becker,salah mtoe hapo kabisa
 
Alisson Becker for Ballon D'or.
Ballon D'or itakuwa hivi.
1) Alison Becker
2) VVD
3) Salah
 
"Naamini una elimu kidogo mkuu,hivyo unajua maana ya ninachokiongelea"

Kama uneona dharau katika hiyo sentensi,basi nina mashaka na uwezo wako wa kuitumia lugha ya Kiswahili mkuu,huenda ni lugha ambayo hauitumii mara kwa mara.
Sina muda wa kumdharau mtu nisiyemfahamu.
Mkuu sijasema unanidharau kiongozi !

Mbona wawa mgomvi kiongozi [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom