HOJA Kwanini Vyuo Vikuu havifungwi kwa ajili ya El Niño iwapo Shule za Msingi na Sekondari zinafunga?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

51-999

New Member
Joined
Jun 21, 2026
Posts
1
Reaction score
3
Naomba kuuliza Wizara ya Elimu na TCU, imekaaje kuhusu kutofungwa kwa vyuo wakati wa El Niño, wakati wanafunzi wa shule za msingi hadi kidato cha sita wamefungiwa shule?

Naona hili linaweza kuwa changamoto, kwa sababu wanafunzi wengi wa vyuo husafiri kwenda Dar es Salaam na maeneo ya jirani, ambayo ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kuathirika. Wanafunzi wengi pia wanaishi katika maeneo hatarishi, ikiwemo mabondeni, kutokana na uwezo wao wa kifedha.

Hata hivyo, TCU na vyuo vinaonekana kutokuwa na tahadhari kuhusu hali hii. Maswali yangu ni, kwa nini tahadhari zinazochukuliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi kidato cha sita hazitumiki pia kwa wanafunzi wa vyuo?
 
Pale Udsm sasa kule yalikuwa Mashamba ya mpunga miaka ya zamani kidogo.. si ndo siku hizi wameweka Hosteli..Sijui itakuwaje😀
 
Hao ni watu wazima. They can handle themselves.
 
Watu wazima wao hawapaswi kuzingatiwa kwenye tahadhari? Kwamba wao wakifa fresh tu kwakuwa ni watu wazima?

Mbona serikali imetoa ufafanuzi kwamba kufungwa kwa shule ni kuhakikisha usalama wa wanafunzi na walimu.

Sasa walimu nao ni watoto? Pia unaposema vyuoni ni watu wazima, unajua wanafunzi wanaosoma chuo ngazi ya cheti na diploma ni wadogo kuliko wanafunzi wa sekondari kidato cha tano na sita?
 
Suggestion Yako ni ipi?
 
basi na kazi zote za ujenzi wa taifa wafanyakazi wote wasiende makazini, wanajeshi wasilinde nchi wakae majumbani, madaktari wasiende hospitali, ofisi za serikali zote zifungwe,ofisi binafsi zifungwe...kisa tunaogopa kufa na elnino..
yaan watu wengine sijui huwa mnafikiria kwa kutumia nini?
 
Mkuu hakuna Elnino,ni utapeli wa TMA na washirika wake,hii october itaisha bila mvua ya maana tofauti na vitisho vya TMA
 
Naomba kuuliza Wizara ya Elimu na TCU, imekaaje kuhusu kutofungwa kwa vyuo wakati wa El Niño, wakati wanafunzi wa shule za msingi hadi kidato cha sita wamefungiwa shule?

Naona hili linaweza kuwa changamoto, kwa sababu wanafunzi wengi wa vyuo husafiri kwenda Dar es Salaam na maeneo ya jirani, ambayo ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kuathirika. Wanafunzi wengi pia wanaishi katika maeneo hatarishi, ikiwemo mabondeni, kutokana na uwezo wao wa kifedha.

Hata hivyo, TCU na vyuo vinaonekana kutokuwa na tahadhari kuhusu hali hii. Maswali yangu ni, kwa nini tahadhari zinazochukuliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi kidato cha sita hazitumiki pia kwa wanafunzi wa vyuo?

Wanafunzi wa vyuo vikuu ni watu wazima....huwezi kuwalinganisha na watoto wa shule za msingi/sekondari
1. Wanajitambua
2. Wanakaa huko huko vyuo viliko hivyo hawahitaji kusafiri kila siku kwenda vyuoni
 
Back
Top Bottom