Unajuaje wamekuwa brainwashed na hawajasema hivyo kwa kuelewa mambo?
Hii hoja yako ina logical fallacy inayoitwa non sequitur. Umeunganisha mambo yasiyo na muungano wa moja kwa moja.
Logic yake ni sawa na hii hapa chini.
1. Rais wa Tanzania ni mwanamke Mzanzibari. Hii ni fact inayojulikana.
2. Fatma Karume ni mwanamke Mzanzibari. Hii ni fact inayojulikana.
3. Hivyo, kwa vile rais wa Tanzania ni mwanamke Mzanzibari, na Fatma Karume ni mwanamke Mzanzibari, basi, Fatma Karume ni rais wa Tanzania.
Umefanya logical non sequitur hiyo hiyo.
1. Kuna nchi zina watu wengi.
2. Kuna nchi tajiri zenye watu wengi.
3. Hivyo, ili tuwe tajiri, tuongeze watu.
Hujaangalia factors nyingi sana, kama vile, kuna nchi zenye watu wengi ambazo si tajiri, kuna nchi zenye watu wachache tajiri, hujaangalia uwezo wa nchi kutumia watu wake, hujaangalia population and resources, technology etc.
Hujaangalla "correlation is not causation".
Hujaangalia economic sustainability.
Hujaangalia the probkem of induction. Inawezekana katika dunia ambayo hizo nchi zikiendelea, dunia ya ujima na mercantilism, ilikuwa kweli ukiongeza watu unaongeza ufanisi wa uchumi, lakini je, kika kilichokuwa kweli jana ni lazima kiwe kweli leo?
Katika dunia ambayo ardhi na resources haziongezeki, utaongeza watu mpaka wapi ili usije kuleta madhara?
Kama tatizo lako si watu -watu unao wengi ambao huwatumii vizuri, hawana kazi, au wako underemployed- hujui kutumia hawa watu waliopo na wanaishia kukisa huduma za jamii, elimu na lishe bora, ukiongeza watu bila kujua kuwatumia utataua vipi matatizo yako? Utahakikisha vipi huongezi tatizo?