Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,515
- 6,230
Mungu akupe maisha marefu . Ikiwezekana utunge kitabu kuwaeleza watoto na wajukuu zetu ukweli.
Wasomi wetu ni tatizo sana wanapoingia kwenye madaraka.
Wanakwapua Mali haraka haraka wanajijenga utajiri mkubwa kwa muda mfupi huku wakiwadanganya watu kuwa maendeleo ya nchi ni mchakato na kutoa mifano kuwa Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Yaani wao wanatajirika kwa sekunde lakini nchi inachukua karne nzima kujenga vyoo vya shimo mashuleni.
Mtu anateua miss aliyeishi Huko Marekani kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya za vijijini. Hivi Maisha ya Marekani yanaendana na Vijiji vya bongo vyenye migogoro ya ardhi na watoto wanakaa chini darasani.
Kwa nini usimpandishe Cheo Afisa Elimu au OCD au DSO au Afsa Utumishi wa Wilaya Au Afsa kilimo wa Wilaya mwenye sifa anayejua kwa undani changamoto za Vijijini ?
Watu wanapeana madaraka kirafiki ili watafune nchi na kulimbikiza Mali. Wakoloni walijenga Taasisi nyingi bila kujilimbikizia Mali. Leo roho ya ubinafsi ni kubwa mno kwa Waafrika Mpaka ndani ya taasisi za dini. Kiongozi wa dini ananunua ndege binafsi na familia yake badala ya kujenga shule au chuo hata cha ufundi cherehani na kuwafundisha watoto wa maskini bure. Wakoloni walijenga shule wakawafundisha akina Nyerere na Mkapa Mpaka wakawa marais kupitia taasisi za dini.
Leo watawala badala ya kuwaelekeza vizuri wale mabilionea wa kidini wanawatumia kwenye siasa kuiba kura na kuhalalisha maovu yao.
Kuna Mikoa kama Shinyanga , Dodoma kuna wafugaji wenye ngombe wengi sana. Huo ni utajiri mkubwa sana mana ngombe 2000 ni zaidi ya sh.BIL.1.3 ,lakini wanaletewa mkuu wa Wilaya anasema CCM itawajengea vyoo na kuwaletea umeme kwenye nyumba zenu za nyasi mana nyie ni wanyonge. Blalifuul.
Badala ya kuwaambia nyie ni matajiri wakubwa na Taifa linawategema kuinua uchumi.
Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Wanyonge, hili neno linawakera wengi 🤣
Kwakweli inackitisha sana mkuu1000 digits