Kwanini waafrika siyo wabaguzi?

Sasa inakuwaje Muhindi, Mwarabu au hata Mzungu anashinda Uchaguzi Afrika? Mfano unafikiri Mwafrika anaweza kugombea Ubunge India au China na akashinda ?
Tatizo sisi tunajifanya wakalim sanaaa
 
Iddy amini aliwafanya nini wahindi, Nyerere hakutaifisha mali za wageni, Mugabe na mashamba ya wazungu?

Kataifisha majengo ya wahindi, sawaa! Nae yukwapi leoo, ameshakufa, dhuluma mbaya sanaa,, na huko alipo atapata anachositahili.
 
Jirani yangu mmoja alikwenda kuoa mhindi, huo mtafuluku alio kumbana nao we acha tuu..
Kwa kuwa bint alikolea basi akampa kibendi na kumzalisha mapacha wawili..
Walikasilika lkn sasa amanj na kwa jamaa hawaendi... Dadadekii
 
ukienda China ukiwa siyo Mchina watakutenga, Uarabuni ukiwa siyo Mwarabu watakutenga vivyo hivyo Wazungu.

Kwanini sisi waAfrika tunalilia kupendwa?

Jamii zingine huwa hawana hali hii ya kungangania kupendwa.

Mfano jamii za ma Buddhist kama waChina wala hawamualiki au kushawishi mtu wa jamii nyingine kuingia ktk mahekalu ili wawe ma Buddhist maana waChina wanakubali dunia hii tupo jamii tofauti tofauti hivyo hawajali kupoteza muda ujiunge na imani yao.

WaAfrika inabidi tulikubali hilo na kupenda vilivyo vyetu kuanzia tamaduni, desturi, imani za miungu ya mababu zetu, kujitegemea badala ya kuwazia kupewa vitu au haki kutoka jamii zilizo za huko mbali Asia, Mashariki ya Mbali, Ulaya na Marekani ya kaskazini.
 
Sasa inakuwaje Muhindi, Mwarabu au hata Mzungu anashinda Uchaguzi Afrika? Mfano unafikiri Mwafrika anaweza kugombea Ubunge India au China na akashinda ?
Kuna wabunge wahindi, waafrika, waarabu Uingereza.
Upande mwengine hapa kwetu ubaguzi ni watanzania wenyewe kwa wenyewe. Vivo hivyo Zanzibar. Wamefikiya kuwavuwa Uzanzibari wenye asili ya huko kwa kigezo cha kutoishi Zanzibar.
 
Sisi ndiyo superior human beings, we are more human than the rest.
 
Sisi ndiyo superior human beings, we are more human than the rest.
Tunakata viungo binadamu wenzetu (maalbino), tuna uchunaji ngozi. Yote haya ni kwa imani za kijinga. Bado sisi ni "binadamu" zaidi.
 
Sehemu ambazo zimeelimika huwezi kukuta Mwarabu, Mhindi au Msomali ni kiongozi, Moshi, Mbeya, Bukoba, Mwanza au Arusha.
 
Tunakata viungo binadamu wenzetu (maalbino), tuna uchunaji ngozi. Yote haya ni kwa imani za kijinga. Bado sisi ni "binadamu" zaidi.
Hao wengine waliteka ma mababu zako wakawafanya watumwa na kuwapiga mijeledi, wakatawala nchi zetu na kutesa na kubagua raia, copy that
 
Lakini Waafrika matajiri ndiyo hupenda kuwa karibu na Wazungu au Waarabu kuliko yoyote yule, Mwafrika tajiri hupenda kuwa karibu zaidi na wageni, hivyo bado siyo mbaguzi, …
Nikifikiria CCM inavyowabagua Watanzania wenzao, duh! Eti kama hukubaliani nao uhame nchi na ole wako usikubaliane nao halafu ubaki nchini, utakiona!

Heri hata hao wanaobagua wageni, ubaguzi hapa Tanzania unaoratibiwa na CCM ni wa hatari! Unaweza kuta unawekwa ndani ya kiroba mzima mzima!
 
Mfano unafikiri Mwafrika anaweza kugombea Ubunge India au China na akashinda ?
Ndiyo na mifano ipo.
Obama.....rais US
Mtanzania.....diwani Uingereza
Kamala ..... Makamu rais US
Tatizo waafrika huwa hatuniini tu
 
Ubaguzi upo sana Afrika,
Sema ukilinganisha na hao weupe utaona kwa sababu sisi ni inferior dhidi Yao.

Ukiwa kabika Fulani kutaka kuoa kabika Fulani utapata upinzani tokea kwenu Hadi kwao.

Baadhi ya makabila huwaita makabila mengine kua ni watu wa kuja.

Nyerere akitumia nguvu kubwa mno kujaribu kuvunja ukabila.

Kuna baadhi ya nchi ni wanabaguana kwa makabila wao kwa wao.
Sema tu ni udhaifu wetu.
 
Ndiyo na mifano ipo.
Obama.....rais US
Mtanzania.....diwani Uingereza
Kamala ..... Makamu rais US
Tatizo waafrika huwa hatuniini tu

Lakini hao wote uliwataja kuna jitihada za makusudi zilifanyika kwanza ili hata tu wakubalike na wengi kama hao wa Uingereza utakuta hata wanaongoza maeneo ambayo wapiga kura wengi ni wageni au kuna special treatment wamepewa lkn kwetu Muhindi au Mwarabu anashinda uchaguzi kwa kishindo sehemu ambayo > 99% ya wapiga kura ni Waafrika, Muhindi, Mwarabu hahitaji special treatment yoyote ile kuchaguliwa Tanzania jambo ambalo ni unique hapa Duniani kwa jamii nyingine, I mean unafikiri wewe unaweza kugombea uchaguzi mfano Irani au India au hata Saudia na ukashinda kwa kishindo ?
 
Mwafrika ni mbaguzi kwa mwafrika mwenzie
 

Lakini ndicho ninachomaanisha, hakuna Ubaguzi dhidi ya watu waliotofauti kimuonekano na sisi wakati jamii nyingine karibia zote ukiwa una muonekano tofauti utabaguliwa au hata tu utajisikia mwenyewe kwamba wewe siyo sehemu ya hiyo jamii lkn Tanzania na Afrika ni kinyume chake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…