Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k?

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k?

Jina ni neno au maneno anayopewa mtu au kitu au hali Fulani

Nataka kujikita kwenye jina tunalopeana watu.

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k., lakini sisi tuna maneno katika lugha za Kiafrika.

Kwanini usumbuke uingie kwenye mtandao na penginepo.

Tanzania tuna lugha nyingi maana tuna maneno ambayo tungetumia kuwapa watoto wetu.

Hatuwi wa maana ati kwa kuitwa Zebedayo au Hasani au Rebecca au Salha nk

Hatuwi wacha Mungu wazuri kwa majina hayo.

Mtu akiishi au akafuata ya huko nje tunamkandia, vipi kuhusu jina mwanao.

Natamami tubadilike, kama wewe ni Mgogo au Mfipa au Mmakua nk tumia neno ambalo unalijua maana take na unalifurahia.

Tuache ushamba wa kupenda tusivyovijua
Majina ya kiafrika mengi hayana maana nzuri.
 
Nashkuru sisi wanyakyusa tunamajina ambayo Yana maana kwenye biblia lakini tunatamka kwa kilugha chetu

Atuganile - anatupenda
 
Ni ushamba na ndio race pekee isiyojitambua tofauti na races zingine.

African have inferior Mind.

Naona huku wapo wanaosema eti ni sababu ya kuJa kwa dini. Ni kweli lakini ni kwa asilimia ndogo sana. Mbona ukristo ulifika mapema zaid yetu nchi za Spain, Argentina na Brazil na bado wamesimama na majina yao.

Je na wao wangesema hayana mvuto majina yao ya Armando Maradona, Leone Mesi, Ronaldinho, Morinho.

Hata India Uislam upo kiasi chake lakini asilimia kubwa wameendelea kudumisha majina yao ya kina Rajvi Khan nk.


Ninachoamini mimi ni kwamba Ubora wa binadamu aliyekamilika ni yule anayesimamia na kutetea asili yake.

Wengine kwetu unakuta mtoto kapewa jina la Makoye lakini eti anabatizwa na jina la Brian.
Sasa jina kama Sikujua lina maana gani au Sikuzani au Kaundime ?

Acha yabakie majina ya ukoo ila ya wana,tuna ujinga mwingi sana.

Leo wapo wazungu kibao wanaitwa Muhammad,wengine Adam na mfano wa hayo.

Kingine waafrika hawakuidhibiti bistoria yao. Leo hii huwa nawapa watoto wangu majina ya watu wema walio tangulia,sasa mfano nikisema nitafute historia ya wajawema wa kwetu Afrika wengi utawakuta wana majina ya kidini,yaani hata wao walitambua ufyongo wa majina yao.
 
Ni dhana ambayo imejengwa toka kipindi cha ukoloni. Africans ni primitive creature(mwafrika awezi kutengeneza kitu kizuri au kufanya jambo zuri). Dhana iyo inatutafuna hadi leo. Hongereni sana watu wa Mbeya majina mengi ni ya asili, Gwakisa, gwamaka, yametawala mkoa wenu. Pia hata hoteli kubwa mmeita majina yenu Mdope hotel, Mkulu hotel pia hata mabasi majina yenu.
 
Jambo lingine kujiita majina yenu ya asili hakuna ubaya ila kuyaponda ya kidini ni ujinga ulio pea.

Ndiyo maana leo hii unakuta mtu anaitwa "Anthony Edward" lakini ni Muislamu,cha msingi majina yawe na maana ila kaeni mkijua ya kuwa majina mazuri yapo,na hakuna majina mazuri kuzidi ya mitume na waja wema.
 
Nashkuru sisi wanyakyusa tunamajina ambayo Yana maana kwenye biblia lakini tunatamka kwa kilugha chetu

Atuganile - anatupenda
Lusubilo.
Gwalugano
Tupokigwe
Tuntufye
Lusajo
Ambakisye
Ambangile
Ambonisye
Atupakisye

Na mengine...

Unyakyusani kupo vizuri.

Lakini siyo kila jina la kiafrika ni la kuchukuliwa.
 
Lusubilo.
Gwalugano
Tupokigwe
Tuntufye
Lusajo
Ambakisye
Ambangile
Ambonisye
Atupakisye

Na mengine...

Unyakyusani kupo vizuri.

Lakini siyo kila jina la kiafrika ni la kuchukuliwa.
[emoji106][emoji106]
 
UNAJUA WAKATI WA UUMBAJI, MUNGU ALISAHAU KUWEKA UBONGO KWA MTU MWEUSI.
KILA KITU TUNAIGA IGA NA SABABU ZA KUHALALISHA ZIPO,
 
Jina ni neno au maneno anayopewa mtu au kitu au hali Fulani

Nataka kujikita kwenye jina tunalopeana watu.

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k., lakini sisi tuna maneno katika lugha za Kiafrika.

Kwanini usumbuke uingie kwenye mtandao na penginepo.

Tanzania tuna lugha nyingi maana tuna maneno ambayo tungetumia kuwapa watoto wetu.

Hatuwi wa maana ati kwa kuitwa Zebedayo au Hasani au Rebecca au Salha nk

Hatuwi wacha Mungu wazuri kwa majina hayo.

Mtu akiishi au akafuata ya huko nje tunamkandia, vipi kuhusu jina mwanao.

Natamami tubadilike, kama wewe ni Mgogo au Mfipa au Mmakua nk tumia neno ambalo unalijua maana take na unalifurahia.

Tuache ushamba wa kupenda tusivyovijua
Umeleta mada ya maana sana, hakuna kinachoniudhi mimi kama majina ya sijui John, Ally, Emmanuel, Hamza, sijui blah blah! kisa eti dini fulani!! ni ujinga wa kiwango cha lami
 
Kiukweli majinaya kibantu hayavutii masikioni.

Si kitu,tuntufye, kokumanyisa, kigwangala, pinda, tundu, kinabo nk.
We Sunderland nini!??? Majina mazuri kama hayo unayakandya kweli we mtumwa
 
Mbona wewe mkuu unavaa chupi, boxer, jeans, suti pensi. Kwenye jina tu ndo unaona. Kwa nini usindie mizizi na mchwa? Kwanini usiishi chini ya mti na mpango? Kwa nini usitembee uchi
we lofa kweli, kwani wazungu na waarabu ndio walipoleta nguo wakakwambia ubadili na jina!!?
 
Kwa majina ya waislam hapa bongo Sawa Ni Dini lakini majina mengi ya wakristo Ni ya kizungu sio ya kikristo ... George,Kevin,Brian,April,June,Stella,Stan,Danford,Datius,Derick, Diana,Janeth,William,Wilson,....nk. nk. Machache ndo ya kidini Paul,Peter,John,Joseph,Mary, .
Sasa we nenda msikitini useme naitwa George John Brian uone majambia ya msumbiji yatavyochomolewa!!
 
Mkuu Utumwa ni fikra yako (zako). Hilo unaloamini ni ww na uoga wako.

Umpe mtoto jina aitwe NGUVU YA NYANI, SUNGURA etc , eti useme ni kuukumbatia Uafrika.

Siyo kila kitu cha kiafrika kizuri vile vile cha kizunngu.


N.B fanya unacho ona kwako ni sahihi.
Na wewe ukimwita Hamza unamaanisha nini kwa mfano?
 
Ushamba. Wazungu wakija watakuwa wanashangaa sana. Ni sawa na mtu leo uende ulaya ukute mtu anaitwa Zamoyoni, utashangaa sana.
Vya kushangaa ni vingi hata tukimuona mzungu anaongea kiswahili huwa tunashangaa vilevile, kuna vitu lazima tuvikubali tu kutokana na huu muingiliano wa watu kama ambavyo kuvaa nguo za wazungu au tiba za wazungu ilivyokuwa imekubalika kama si huu muingiliano na tungekomaa na vitu vyetu basi pengine tusingekuwa tunatumia hata panado ni mwendo wa mizizi tu na wala hakuna jeans wala boxer.
 
Back
Top Bottom