Kwanini Waandishi wa habari Tanzania hawaongelei rushwa?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tumekuwa na taifa la ajabu hasa kwenye waandishi wa siku hizi.

Hakuna hata blog mmoja au youtube channel ambayo ni ya rushwa! Wakati ndiyo kitu kikubwa sana wananchi hawakipendi. Tume baki kuangalia tu idadi ya wanawake wa wasanii! 🤔 na umbeya kila siku

Nashauri wana habari tengeni muda na kutupa habari za uhakika za rushwa ili tupunguze hili janga.
 
Rushwa ni suala mtambuka linamuhusu kila mmoja hivyo sio lazima waandishi wa habari pekee walizungumzie.

Kwa kuwa ni suala linalomuhusu kila mmoja kwa ukubwa wake suala hili ni muhimu likapata mjadala mpana wa kitaifa .

Watu waoga na wenye hofu kama wewe mleta mada hawana ujasiri wa kulizungumzia suala la Rushwa na wanatupia mzigo watu wengine
 
Tumekuwa na taifa la ajabu hasa kwenye waandishi wa siku hizi.

Hakuna hata blog mmoja au youtube channel ambayo ni ya rushwa! Wakati ndiyo kitu kikubwa sana wananchi hawakipendi. Tume baki kuangalia tu idadi ya wanawake wa wasanii! 🤔 na umbeya kila siku

Nashauri wana habari tengeni muda na kutupa habari za uhakika za rushwa ili tupunguze hili janga.
Wataongeleaje na wenyewe ni wala rushwa, unaweza kuukata mkono unaokulisha wewe?
 
Wala siyo rushwa tu. Akina Balile wanajitoa ufahamu kuongelea Mambo ya Ihefu lakini huwasikii kuongelea mapungufu ya uongozi wa rais Samia kama kukopa kuliko pitiliza, kubinya uwanja wa siasa, kushamiri kwa rushwa, n.k.. Hii ni kwasabb hivi sasa waandishi wa habari wanapewa trip na posho za kisafiri kwenda nchi za nje na viongozi mbalimbali.

In short hutasikia waandishi wakiiponda hii awamu kwasabb wanapewa bahasha.

Ukimsikiliza Balile kwenye clip ya bonde la Ihefu anaongelea madhaifu ktk mambo yaliyotokea miaka 6 iliyopita
 
Embu tutulie kwa umakini kabla tujaendelea kukemea huku wakitutazama
IMG_0346.jpg
 
Tumekuwa na taifa la ajabu hasa kwenye waandishi wa siku hizi.

Hakuna hata blog mmoja au youtube channel ambayo ni ya rushwa! Wakati ndiyo kitu kikubwa sana wananchi hawakipendi. Tume baki kuangalia tu idadi ya wanawake wa wasanii! 🤔 na umbeya kila siku

Nashauri wana habari tengeni muda na kutupa habari za uhakika za rushwa ili tupunguze hili janga.
Kuna rushwa za aina 2.
1. Petty Corruption
2.Grand Corruption

Petty corruption ni rushwa yetu ya kawaida, tumeizoea and its order of the day, wengine tunaitoa wenyewe bila kuombwa ili tupate preferential treatment and sometimes just to save time and money, kama una haraka zako, una overspeed ukipigwa mkono, unaachia Msimbazi fasta na kuendelea kuliko kusubiri notifications ni msimbazi 3!. Polisi wanalipwa mishahara kiduchu sana hivyo let's support them kama jamii inavyotusupport sisi waandishi wa habari. Hii sio rushwa mbaya kivile wala haihitaji kuandikwa saana kivile.

2. The grand Corruption ndio rushwa mbaya inayohitaji waandishi mahiri wa IJ, kuiandika ila huku nako kuna changamoto zake. Kuna issues tunazifuatilia taratibu na strategic, zikiifa nawapakulia.

JF ya zamani was doing a good job kwenye hili kuliko JF hii. EPA, IPTL, TANGOLD, Meremeta, Escrow, DCP, Radar, Richmond ziliibuliwa humu JF na kufanyiwa kazi. Siku hizi sijui tumekuwaje?!. Kuyaandika haya kwataka moyo Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
P
 
P,

Nafikiri hata hiyo ya petty corruption isiwepo mfano hii ya kucheleweshewa card za NIDA mpaka wahogwe ni petty au grand?
 
Petty Corruption ni vijirushwa vidogo vidogo vya kufanya mambo yaende fasta, nyingine haziombwi ni wewe tuu mwenyewe unajiongeza, mfano hilo la Nida, kati ya my 10 kids, 5 ni over 18, kwenye vitambulisho vya Nida unakuta foleni ya ajabu!. Nikajiongeza, 'unawaona watu', nilipata vitambulisho vyangu 7 within one week!. Passport 4 days, sehemu yenye foleni ndefu na hakuna jinsi ya kuikatisha ni appointment ya US visa, nayo nikagundua mbinu, unaomba visa type I multiple entry, unalipa US $ 500 per visa pale City Bank. Kwenye attachment badala ya kuatach flights bookings, unalipia kabisa flights multiple flights kujulisha una haraka kweli na ndio maana ume risks kulipia flights before visa. Take it from me unapewa early appointment!.

Sehemu nyingi tuu najiongeza, foleni za hospital, ukishikwa law traffic offences zinazohitaji notifications, you just do them away by ten fasta you save time and money!.

Kama zile huduma tunalipia na kuhudumiwa willingly, unashindwaje kutoa kitu kidogo ukahudumiwa fasta?.

Grand Corruption ni rushwa kubwa za wakubwa zile za 10%. Blaza aliruhusu polisi na traffic kupata hela ya kiwi!.
P
 
Back
Top Bottom