Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
- Thread starter
- #21
Kinkunti El PerdedoTasnia ya habari Tanzania ni pasua kichwa mkuu hii inachangizwa na sababu mbalimbli ambazo kwa namna moja ama nyingine zinafanya waandishi kuogopa kufanya investigative journalism ( Habari za uchunguzi)
Mosi,waandishi wamepoteza dira kwa kuacha maadili ya kazi yao na kusaka nafasi za uteuzi hii imepelekea wengi kuwa makasuku mfano ni Mwandishi nguli Pasco mayalla.
Pili,Kupotea na vifo vya utata kwa waandishi wa habari ndani ya nchi hii nani asiye jua juu ya kupotea kwa Bwana Azori ngwanda wa Mwananchi communication limited? Bado tasnia ya habari haija sahau kifo Cha Daudi Mwangosi wa channel Ten mkoa wa Iringa vipi kuhusu kifo Cha utata Cha bwana Stani katabalo
Tatu,sheria kandamizi zipo bado tusijitoe ufahama kujisaulisha kwamba sheria zimebadilika zipo mfano ni The Media Service Act of 2016.licha kwamba sheria hii imetoa mwanga mzuri kwa kutambua Journalism Kama professional lakini Kuna vipengele ni hatari kwa ustawi wa tasnia ya habari nchini.
Nne,Kuto zingatia taaluma (unprofessionalism) Kuna watu mpaka Leo wanaamini kwamba uandishi ni kipaji(talent) na sio taaluma(professional) ndio maana kwenye media nyingi wamejaa vilaza mfano wakina Mwijaku,Baba levo nk
Tano, Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yameleta kitu kinacho itwa "Citizen Journalism" hii kitu imekuwa challenge kwa waandishi wengi maana kila mtu ana share habari hivyo Mwandishi lazima afanye jambo la ziada kuonesha utofauti wake na watu ambao sio waandishi.
Kwa uchache naomb niishie hapa GT wataongeza madini muhumu
Umenena vyema kabisa.
Hongera kwako🤝