Kwanini waandishi wa habari Tanzania hawaripoti taarifa zenye maslahi mapana kwa Taifa letu?

Kwanini waandishi wa habari Tanzania hawaripoti taarifa zenye maslahi mapana kwa Taifa letu?

Kwa taarifa yako rais ni muajiriwa wa wananchi na sio boss wa wananchi. Kwa bahati mbaya kwa katiba ya nchi hii na vimelea vya ujamaa vilivyopo, rais amegeuka mungu mtu hawezi kuhojiwa. Kwenye nchi za wenzetu kiongozi anaagizwa na anaweza kuhojiwa hadi kuondolewa madarakani ikibidi. Huku rais ndio anaamua nani awe kiongozi, hata viti kama ubunge na udiwani ambao huchaguliwa na wananchi kikatiba, siku hizi yeye ndio anaamua nani akalie kiti, kisa cha yote haya ni chawa wa aina yenu mnaomtukuza rais.

Sikiliza kijana, kwa sisi wabobezi wa comparative and philosophy of law, democracy is imbedded in culture. You will never have a democracy which is not going along with the culture. If you have one, that is a fake democracy. Sasa ninyi mnataka muige western democracy which is according to their culture. Unataka eti watu wawe huru kumtukana rais, halafu unaiita hiyo ni democracy. Kulingana na mila zetu hiyo ni laana. Au kutengeneza lisanamu kama walivyo fanya kwa Trump na kulivuta matiti. Kwa upande wetu hiyo haipatani na akili. Kwa kuhitimisha, demokrasia haiigwi, haigezwi, bali inajengwa kwa misingi ya mila, desturi na amali za jamii husika. Hakuna universal democracy. Kila watu wana demokrasia ya kwao.
 
Tatizo la Waandishi wetu, ama kwa makusudi ama kwa kutojua, wanadhani Serikali na Taifa ni kitu moja!! Bora basi hayo yangekuwa yanafanywa na Uhuru, Habari Leo, na Daily News lakini hata magazeti binafsi, wao nao ni watu wa ku-advocate serikali zaidi kuliko taifa!!

But kwa upande mwingine, now am sick na watu wanaojitambulisha kama Waandishi wa Habari!! Hii ni taalamu inayohitaji watu wenye uelewa mpana kuliko watu wanaoenda huko kwa sababu tu walishindwa kuchaguliwa kusoma LL.B na kozi pendwa zingine!!

Bro huko kote tisa, kumi ni hizi radio stations. Kule ndiyo utakoma, kuna watangazaji au waongoza vipindi. Wanaongea upotovu wa mambo tena kwa kujiamini mpaka unakoma. Halafu cha kusikitisha wanapotosha, wala hakuna mtu wa kurekebisha, matokeo yake vijana wa kizazi kipya ambao ndiyo wengi wanasikiliza radio hizo wanakuwa na uelewa uliopinda kuhusu mambo mengi ya msingi.
Sisi kipindi chetu, tulikuwa tunawasikiliza akina Abdul Ngalawa, David Wakati, Jacob Tesha, Othman Miraji, Ben Wazir kuwataja kwa uchache, hiki kizazi kilikuwa kinahabarisha mpaka mioyo inakuwa haina wasiwasi kabisa na habari kutoka kwao. Walikuwa wakitafiti, licha ya kuwa nyenzo za utaiti zilikuwa haba tofauti na sasa, ukiuliza tu kwa professor gugo kila kitu kiko hapo. Lkn walihabarisha vitu makini, amini na kweli. Aina ile ya waandinshi ni nadra sana kuwaina. That's sad side of it.
 
Sikiliza kijana, kwa sisi wabobezi wa comparative and philosophy of law, democracy is imbedded in culture. You will never have a democracy which is not going along with the culture. If you have one, that is a fake democracy. Sasa ninyi mnataka muige western democracy which is according to their culture. Unataka eti watu wawe huru kumtukana rais, halafu unaiita hiyo ni democracy. Kulingana na mila zetu hiyo ni laana. Au kutengeneza lisanamu kama walivyo fanya kwa Trump na kulivuta matiti. Kwa upande wetu hiyo haipatani na akili. Kwa kuhitimisha, demokrasia haiigwi, haigezwi, bali inajengwa kwa misingi ya mila, desturi na amali za jamii husika. Hakuna universal democracy. Kila watu wana demokrasia ya kwao.

Rais anayepaswa kuheshimiwa ni aliyeingia madarakani kwa uchaguzi wa heshima, sio uchaguzi wa kihayawani kama ule wa 2020. Ukitaka heshima ingia madarakani kwa njia za heshima, bila kujali ww ni wa Afrika au Western. Labda useme zile njia za kishenzi kwenye chaguzi zetu ndio hizo mila zenu.
 
Watafungiwa au kubambikiziwa kesi za uchochezi...
 
Ungeuliza kwanini wananchi hawapendi kufatilia taarifa / habari zenye masilahi mapama ya nchi hii badala yake wanaendeshwa kwa trends za ajabu?
Waandishi washajua Watz hupenda taarifa za bongofleva, Mandonga au Simba/ Yanga au Manàra kapokewa bungeni..... kaazi kwelikweli.
 
jambo la kushangaza Sana, kuwa hdkuna chombo cha habari, kilichoripoti habari hiyo

Jambo jingine linalostaajabisha aina ya waandishi ni wanapokaribishwa badala ya kuuliza maswali utaona wanapiga kofi viganja vyao kwa kuunga maneno anayosema kiongozi wa serikali yaani mkutano wa waandishi badala ya kuhoji, wao wanapiga makofi kila baada ya dakika kama vile sauti ya mawimbi ya bahari yanavyotua pwani kwa kukunwa na uongo wa wanasiasa wa CCM.
 
Bro huko kote tisa, kumi ni hizi radio stations. Kule ndiyo utakoma, kuna watangazaji au waongoza vipindi. Wanaongea upotovu wa mambo tena kwa kujiamini mpaka unakoma. Halafu cha kusikitisha wanapotosha, wala hakuna mtu wa kurekebisha, matokeo yake vijana wa kizazi kipya ambao ndiyo wengi wanasikiliza radio hizo wanakuwa na uelewa uliopinda kuhusu mambo mengi ya msingi.
Sisi kipindi chetu, tulikuwa tunawasikiliza akina Abdul Ngalawa, David Wakati, Jacob Tesha, Othman Miraji, Ben Wazir kuwataja kwa uchache, hiki kizazi kilikuwa kinahabarisha mpaka mioyo inakuwa haina wasiwasi kabisa na habari kutoka kwao. Walikuwa wakitafiti, licha ya kuwa nyenzo za utaiti zilikuwa haba tofauti na sasa, ukiuliza tu kwa professor gugo kila kitu kiko hapo. Lkn walihabarisha vitu makini, amini na kweli. Aina ile ya waandinshi ni nadra sana kuwaina. That's sad side of it.
Huko kwenye Radio Stations huko, dah!!

To be honest, kwenye hizo radio huwa tu nasikiliza vipindi vya michezo na burudani lakini sio eti serious issues na serious analysis nitarajie kupata huko!!

Na kinachonitisha zaidi, hata huko kwenye michezo ambako binafsi sijabobea bado nikisikia uchambuzi wao, una-feel kabisa uhaba wa maarifa especially pale wanapojaribu kuchambua mambo ya off-pitch!!

Na cha kushangaza ndo hicho ulichotaja... Google University!! Watu wana full access to wide ranges of info lakini wanashindwa kabisa kutumia hiyo fursa!!

Yaani unakuta Mwandishi anahoji top executive kwenye field husika, na mada yenyewe ni serious lakini ukisikia maswali yenyewe, dah!! Sidhani hata kama wanafanya maandalizi....

I wish akina Pasco wangerudi kwenye electronic media!!
 
Nimekuwa nikifuatilia waandishi wa habari wa nchi hii, nikagundua kuwa zile habari muhimu sana, zenye maslahi mapana kwa Taifa hili hawaziandiki na badala yake, wao Kila siku ni kuandika "mapambio" ya kusifu na kuabudu viongozi walioko madarakani!
Makanjanja na wachumia tumbo ndio wamejaa tasnia hiyo now days ndugu!
 
Mkuu semtawa, thanks for this, waelimishe madogo humu kuhusu kitu kinachoitwa responsible journalism, media tukiitwa press conference, haturipoti kama kasuku, tunatumia objectivity kuamua turipoti nini kwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.
P
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari ambaye ni mwandishi wa habari huru na wa kujitegemea kwa kujitolea na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo huru cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari kwa media zetu za Tanzania yetu.

Nawatakia maadhimisho mema ya siku yetu hii ya leo na uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu
Hili ni kosa la kiufundi ktk lugha. Huwezi kusema/kufanya jambo kwa niaba yako mwenyewe.

Kwasabb wewe ndiye unayelitenda hilo jambo halafu unaueleza umma kuwa unajiwakilisha mwenyewe.
 
Back
Top Bottom