Uchaguzi 2020 Kwanini Wabunge wazoefu wa Upinzani hawajaenguliwa?

Uchaguzi 2020 Kwanini Wabunge wazoefu wa Upinzani hawajaenguliwa?

Hoja yako imejibiwa na paragraph hii;

"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
hapa unasema uongo.
Mwanasheria angesimamia ujazaji wa form ya Gwajima asingekula kiapo tarehe 26 while form imesainiwa tarehe 20.

MaCCM wanaogopa kuwaengua kimizengwe wabunge wazoefu wa CDM kwasababu wanajua wanaushawishi wa kuingiza raiya barabarani.
 
Kwani kujaza hizo fomu inahitaji uwe na degree ngapi?!

Mnawakata hao wapinzani makusudi, kama ni makosa, hawawezi kuwa wanakosea peke yao, hata CCM na wanakosea.
 
Hoja yako imejibiwa ndani ya mada na paragraph hii;
"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
Si kweli, tume ni yao hata wakikosea wanaitwa yanafanyika marekebisho.
 
Hoja yako imejibiwa na paragraph hii;

"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
mgombea wa bukene ni mwanasheria kwa taaluma au hizo fomu ni kwa wanasheria wa ccm tu?
 
Kwani wageni ni wapinzani peke yao, hakuna ccm mgeni uchaguzi huu?!

Mbona hawajaenguliwa ccm hata mmoja?!
Wamesaidiwa na wanasheria wa Chama kujaza fomu zao, Wakati Chadema ikiendelea na ule mchakato wa kusaka wadhamini, CCM Wao na vikao vya kujaza fomu n.k,

Ule Wakati wamejikalia kimya kumbe ndani yake kilikuwa kishindo, Uchaguzi ni mipango mkuu
 
Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao.
Mimi mwanasheria wangu kuna form zangu za biashara kazikosea na nishazifikisha ofisi ya serikali ndio nikajua kama alikosea. Kwahio wanasheria wa ccm hawakosei?

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hoja yako imejibiwa na paragraph hii;

"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
Wewe jamaa ni kilaza kweli sijui una njaa ya muda gani kichwani mwako?

Unaamini kwamba mgombea wa upinzani akijaza form peke yake ndo hajui Sheria.?
 
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake
Hivyo unataka kusema kujaza form za kugombea ubunge na udiwani zinapaswa kujazwa na wanasheria tu, usipokuwa mwanasheria au bila kujaziwa na mwanasheria huwexi kujaza form ya uchaguzi?!

Kweli mtaji wa ccm ni wajinga.

ccm hawajazoea ushindani na tunaliona miaka yote popote palipo na uchaguzi.

Hawa ccm wamezoea kuteuliwa ndio maana kuna mijinga inashinda kura za maoni, inaenguliwa wanawekwa wenye chama yenyewe yana ahidiwa kuteuliwa yanakubali.

Eti aliyekuengua usigombee ubunge anakuahidi kukuteua una kenua meno.

ccm wanafahamu hawawezi kupigiwa kura, hivyo kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi wanawaondoa washindani kwa hila.

Hakuna kasoro isiyorekebishika, kukosea kujaza form sio sababu kumzuia mtu asishiriki uchaguzi, hili lilipaswa kuwa jukumu la wasimamuzi wa uchaguzi, kuwaelekeza na kuwasaidia wagombea kujaza form kwa usahihi ili kuwe na uchaguzi wa haki.

Siyo kumuengua mgombea kwa hila ili ccm washinde.
 
Hoja yako imejibiwa ndani ya mada na paragraph hii;
"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
Unamsaidia mtu kujaza fomu ambayo mjukuu wangu wa grade 2 anaweza kuijaza vyema,tena huyu mtu anagombea nafasi ya kwenda kutunga sheria na kupitisha bajeti!.
CCM mpo serious kweli na maendeleo ya hii nchi?
Kule bungeni anaenda kufanya nini?
Wanasheria hao wa CCM ndio hao hao waliowasaidia kuingia mikataba ya "kimangungo" na "mabeberu"?
 
Hoja yako imejibiwa na paragraph hii;

"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
Hahaha yani ujinga nayo sifa, hivyo hata Magufuli na PhD yake kajaziwa form ya kugombea na mwanasheria?!

Nini kinahitaji mwanasheria kujaza form ya kugombea?!

Kujaza jina la mgombea, mahali unapoishi, kujaza mali zako, na taarifa zako binafsi unahitaji mwanasheria?!
 
In simple language "Lazima mwaka huu turekebishe akili zenu liwake jua au inyeshe mvua"

Msije mkalaumu maana mchezo mumeuanza nyie!
Comment na mada zako huwa zinaburudisha!

Nakumbuka wakati wa kile kilichokuwa kinaitwa Janga la Corona ulivyokuwa ukileta mada na idadi ya "vifo" huku ukijiapiza kuhusu hatima ya Rais Magufuli! Kwa sasa uko kimya kama vile hukuwa wewe!

Kwa sasa umeanza tena kujiapiza kuhusu Uchaguzi Mkuu lakini baada ya muda utazimika tena!

Tanzania kuna vituko!
 
Huhitaji kufanya uchunguzi wa kina kugundua kama wapinzani nchini hawajajipanga

Ukiangalia utagundua wabunge wote wa upinzani wa kuchaguliwa ambao wana uzoefu bungeni hawajakutana na "panga" la kuwaengua kwa sababu kuu moja ambayo ni kujua vizuri taratibu za mchakato wa kuchukua fomu, kujaza kwa usahihi na kurudisha kwa wakati unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Uchaguzi.

Baadhi ya Wabunge waliokuwa wa viti maalum pia wameenguliwa kwa sababu nao hawana uzoefu katika mchakato kutokana na kuwa hawakuwahi kujaza fomu za kugombea ubunge bali walipewa ubunge kupitia vyama vyao.

Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao.

Wapinzani wataendelea kulalamika wakati tatizo na ufumbuzi wa tatizo uko ndani ya uwezo wao kama watajipanga vizuri.

Wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii wakati masuala ya muhimu kwenye "ground zero" hawayafanyi kwa umakini.

Uchaguzi Mkuu ni mchakato na sio tukio

Ikumbukwe kuwa Sheria hazina Siasa

Kilichobaki kwa sasa ni kuhesabu maumivu
Hivi kwa nini wagombea wote wa upinzani katika mkoa mmoja baada ya kuchukua fomu wasikusanyike kwa pamoja na kuelekezwa na mwanasheria pamoja na mbunge mzoefu ndani ya mkoa huo kwa pamoja amvapo wangetumia sample form moja iliyojazwa tayari? Kisha fomu walizojaza zikaguliwe kwa pamoja ndipo kila mmoja airudishe tena kwa kusindikizwa.

Inawezekana kabisa baadhi wanazikosea makusudi kama kule Misungwi. Kama kuna wabunge waluhama vyama je haiwezekani pia wagombea kuhama vyama?

Nafikiri suala la kujaza fomu na kurudisha kila chama kingelifanya ni jukumu la uongozi wa chama ngazi ya jimbo na asiachiwe mgombea.

Itafika mahali watu watakuwa wanapambana ndani ya vyama wateuliwe kugombea kwa lengo la kwenda kuuza fursa ya kugombea kwa mpinzani wake ili mpinzani apite bila kupingwa.
 
Anayewadanganya kuwa huu uchaguzi mtaenda nao katika uhuni huu mnaoonyesha mwambieni akaje upya. Nasema mwambieni akaje upya. Endeleeni na utoto wenu huo huo! Sisi kwa sasa tumeinamisha vichwa chini kama kobe. Muda ukifika tutavinyanyua
Dogo kwahiyo unakubali hata pingamizi la Tundu dhidi ya mgombea wa CCM na CUF ni utoto.
 
Huhitaji kufanya uchunguzi wa kina kugundua kama wapinzani nchini hawajajipanga

Ukiangalia utagundua wabunge wote wa upinzani wa kuchaguliwa ambao wana uzoefu bungeni hawajakutana na "panga" la kuwaengua kwa sababu kuu moja ambayo ni kujua vizuri taratibu za mchakato wa kuchukua fomu, kujaza kwa usahihi na kurudisha kwa wakati unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Uchaguzi.

Baadhi ya Wabunge waliokuwa wa viti maalum pia wameenguliwa kwa sababu nao hawana uzoefu katika mchakato kutokana na kuwa hawakuwahi kujaza fomu za kugombea ubunge bali walipewa ubunge kupitia vyama vyao.

Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao.

Wapinzani wataendelea kulalamika wakati tatizo na ufumbuzi wa tatizo uko ndani ya uwezo wao kama watajipanga vizuri.

Wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii wakati masuala ya muhimu kwenye "ground zero" hawayafanyi kwa umakini.

Uchaguzi Mkuu ni mchakato na sio tukio.

Ikumbukwe kuwa Sheria hazina Siasa.

Kilichobaki kwa sasa ni kuhesabu maumivu.
Kwa hiyo unataka kusema Magufuli aliyekosea hakuenguliwa kwa vile ni mzoefu?
Acheni ujinga wenu na kujadili ujinga ni kuwa wajinga.
Dawa yenu kiwake tuu, na mkiua watu The Hague ipo itawanyoa kwa chupa. Mwaka huu mtashika adabu tuu.
Eti sie tunapendwa sana tumefanya makubwa yanaonekana, sasa ujambazi wa nini kama mmefanya makubwa?
Ndugai kweli wa kutuma watu wakampore mgombea fomu? Au Majaliwa wa kuagiza vipigo kwa wengine ili tuu wapite bila kupingwa?
Huo ni upumbavu wa hali ya juu ambao awamu ya 5 isiyokubalika kwa wengi inautumia na hautakubalika this 2020.
 
Wamesaidiwa na wanasheria wa Chama kujaza fomu zao, Wakati Chadema ikiendelea na ule mchakato wa kusaka wadhamini, CCM Wao na vikao vya kujaza fomu n.k,

Ule Wakati wamejikalia kimya kumbe ndani yake kilikuwa kishindo, Uchaguzi ni mipango mkuu
Hahaha uongo huu unadhani unaweza kujustfy uovu unaofanywa na ccm na serikali yake?!

Yani mbunge mtarajiwa ajaziwe form ya kugombea?!

Magufuli, Mpango, Kabudi, Ndalichako, nao wamejaziwa form hizo na tume au wanasheria?!
 
Hahaha uongo huu unadhani unaweza kujustfy uovu unaofanywa na ccm na serikali yake?!

Yani mbunge mtarajiwa ajaziwe form ya kugombea?!

Magufuli, Mpango, Kabudi, Ndalichako, nao wamejaxiwa form hizo na tume au wanasheria?!
Mkuu! Kusaidiwa sio mpaka ujaziwe!
 
Back
Top Bottom