Kwanini Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania Bado Wanaishi Kambini?

DidYouKnow

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,229
Reaction score
1,950
Hili jambo hunitatiza sana. Kwanini wachezaji wawekwe kambini? Tutasema hawana nidhamu, lakini kama mchezaji hana nidhamu itakayomfanya awe kwenye kilele cha kucheza mpira basi huyo hastahili kuwa mchezaji tena.

Binafsi naamini kambi zinaongeza gharama zisizohitajika.
 
mbon hat ulaya wanaish kambin
Acha uongo Ulaya mchezaji anatoka kwake anaenda mazoezini wakimaliza anarudi nyumbani

Siku za mechi ivo ivo anatokea kwake wanakutana kwenye training ground au popote wanapopangiana wanapanda basi wanaelekea uwanjani , japo kuna tim kama Man U huwa wanakutana usiku mmoja kabla ya mechi wanalala hotelini

Mechi za away nazo ni ivo ivo tu. Nashangaa sana huku kuwaweka kambini aisee inamaana huwa hawaendi kusalimia familia au?
Kambini inatakiwa mkae national team tu
 
. Hata siku moja nayo nikambi refer ishu ya bakrey kutoroka Chelsea kambini kwenda klabu
 
Wachezaji wa kibongo uwezo wa kujisimamia, kujielimisha,nidhamu binafsi ni ndogo.
Naamini mpaka sasa wengi wameshindwa kujifunza kwa Mbwana Samatta.
Nakumbuka kuna wakati Samatta akiwa TP Mazembe, kila akirudi nyumbani wachezaji alikuwa anashangaa wenzie wanamuulizia radio(portable radio),wala sio namna ya kutoka hapo walipo na kufikia njia za kuwafikisha timu kubwa nje ya nchi.

Nishauri wachezaji kupitia chama chao waombe mafunzo ya kuwafanya wawe 'professional players':
Wakipata fedha waweke wataalamu wa kuwasimamia mambo yao(mfano wakala,msemaji na meneja).
Wakiyafanya hayo,natarajia wachezaji wengi watabadilika,
Labda,sasa watajitambua kama wanamuziki wa Bongo flavour(wana watu wanasimamia mambo yao).
KAMA MCHEZAJI,NI STAA NA YUPO TIMU KUBWA,basi angalau
1.mwisho wa msimu awe na CD yenye matukio yenye kuonyesha uwezo wake.
2.awe na mwanasheria wake,kwa ajili ya kuchambua haki na swahili zake.
3.atafute shule ya kujiendeleza,aidha lugha(kifaransa,kispanish,au kiingereza),au taaluma nyingineyo.
4.awe na wakala atakaye kuwa anafuatilia maendeleo yake.
5.kuepuka kuonyesha vitendo vya ukosefu nidhamu awapo uwanjani.
Wakati mwingine vilabu vimekuwa chanzo cha kushindwa kulea ubora na maisha ya wachezaji kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi uendeshaji vilabu.
 
John Boko


Umewahi kumsikia na hayo maskendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…